Kwa Rais Magufuli tu - Must Read 2017

Kwa Rais Magufuli tu - Must Read 2017

Hii kwangu mimi ni post bora ya mwaka....naomba inawezekana pia iingizwe kwenye kinyanganyiro cha kugombea post bora ya karne .
Najua washauri wa mkulu kumwamo wanasoma ila kwa hofu ya kuhofia kutumbuliwa hawatamuambia. ..MUNGU AKAUFANYA MOYO WE FARAO HUWA MGUMU ILI AJITWALIE UTUKUFU NA KUDHIHIRISHA UKUU WAKE KWA MAPIGO ATAKAYOWAPA WA MISRI.
Mimi pia mkuu 100%
 
Viongozi waliopita (waliosikiliza ushauri wa hao wataalamu) wamlitufikisha wapi? Tafakari, chukua hatua
 
Makosa haya ya kimkakati yatasababisha umalize miaka 5 kwa mafanikio finyu sana

1. Una nia ya dhati ya kulipeleka taifa hili mbele, lakini unateua watu wenye uwezo mkubwa wa kutenda ila hawana nia ya kutenda na nitafafanua vizuri kwenye namba zinazofuata.

2. Unaruhusu vyombo vya dola kufanya baadhi ya matendo wakidhani wanatetea hadhi yako kumbe wanachochea chuki ya wananchi dhidi yako kwa matendo ambayo wewe hukuyaidhinisha kwa sababu kuna washauri wako wa kiusalama wamekuonya kuwa ukiingilia maamuzi ya vyombo vya dola, utawavunja moyo na hivyo utahatarisha usalama na ulinzi wa nchi. Wanakudanganya, kumbuka wewe ndiye amiri jeshi mkuu hivyo hawatakiwi kuchukua maamuzi yanayogusa maslahi ya taasisi ya Rais bila wewe kuridhia. Usikubali kuingizwa mkenge.

3. Mbona kwa vyombo vingine unatumbua, mfano 'Treasury Registrar', 'CEO NIMR', TANESCO n.k? au ndio ile mishahara inayozidi shs 15 mil, unatoa aliyezidi halafu anayeingia unampa 'ceiling price'.

4. Watumishi wa umma wana mishahara midogo kiujumla hivyo japo umefanya vema kufyeka madili yao kuanzia 10% ya manunuzi, safari za nje, safari za ndani pia, bajeti za matanuzi, watumishi hewa n.k, hata hivyo ujue hiyo ndiyo ilikua 'motivation' yao kufanya kazi, hivyo ukae ukijua asilimia zaidi ya 70% ya watumishi wa umma hawakupendi. Watatabasamu tu usoni lakini umewakata miguu hivyo wanakuchukia sana. Sio wao tu hata na ndugu zao wanaowategemea.

5. Asilimia kubwa ya wafanyabiashara masikini waliokuwa wanawategemea hawa watumishi wa umma ili biashara zao ziende hawakupendi kwa sasa. Haimaanishi umefanya vibaya mkuu wa nchi, hapana, bali umeng'oa jino bila ganzi hivyo kabla haya maumivu hayajaisha itakua 2020, usitegemee hawa watu watakuunga mkono.

6. Kimsingi mkuu wa nchi kwa sasa unapendwa na watu kama ndg Makonda na ndg. Polepole kwa kuwa umewapa kitu ambacho hawakuwahi kukiota maishani mwao, na sio kwa sababu ya mapenzi ya dhati hivyo usije kudhani wanakupeeenda hapana ni maslahi tu.

7. Pia unapendwa na watu kama mimi ambao tunaangalia nia yako ya dhati na sio maumivu haya ya muda mfupi. Hata hivyo mtazamo huu bado sana kwa nchi yetu, hivyo hata mimi nakua na mtazamo kama wako yaani mtazamo wa haki lakini sio mtazamo sahihi kwa wakati sahihi.

8. Hivyo ujue (rejea namba 1) umeteua PHD's ambao wanatetemeka sana kwamba watafanyaje kwenye hivyo vyeo ili na wao wasitumbuliwe. Pia umeonyesha kwao kuwa na 'micro-management' hivyo hawajui kama wanapoingia kazini wakae kimya na kuweka 'autopilot' kama Ryoba wa TBC kuogopa utumbuzi au wawe 'creative' lakini kwa kukusoma vizuri kama Makonda wa DSM, sasa sijui wakachukue kozi kwa Makonda? (how to understand JPM).

9. Kwa jinsi ulivyo Rais wa watu tena wanyonge, ulitakiwa usikilize ushauri wa washauri wako wasio na woga kisha ufanye maamuzi sahihi, lakini ujue kabisa mkuu wangu, umezungukwa na washauri waoga kuliko maelezo, na ndio maana wanakupa ushauri kikasuku kasuku kwa kuogopa kutumbuliwa, hawa washauri wa hivi ndio wanasababisha uonekane kwa baadhi ya watu kuwa 'dikteta'.

10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;

11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.)

12. Mkuu CCM hiyo imeshakufa, hunayo tena mkuu. Sasa hivi kuna CCM 'Chama Cha Magufuli'. Ila CCM ya mwaka juzi ile ya 'Chama Cha Madili' haipo. Kwa kifupi ninamaanisha utajidanganya sana kama ukidhani kwa kuweka viraka kwenye CCM utakua na mafanikio, mkuu wangu hiyo CCM uliyo nayo haiendani na wewe hata kidogo, kuna manung'uniko mazito sana hata kwa walio karibu kabisa na wewe, yaani kwa CCM hiyo watu wanatamani 2020 ifike leo ili waondoe huu 'mzimu' wa JPM wapumue, maana wana miaka 4 ya kushindwa kupiga dili.

13. Sijui unawasaidiaje wananchi wanyonge ambao na wao wamefaidika siku zote na mfumo dhalimu ambao umewanyonya pale na kuwafaidisha hapa. Yaani ni kwamba huu mfumo unaopambana nao mkuu wangu kila unapoupiga pigo moja, mapigo kumi yanaenda kwa wale wale wanyonge unaowatetea. Huyo mama ntilie unayemtetea leo hii hana mauzo kwa sababu wateja wake ni hao hao wapiga dili kwa njia hii au ile.

14. Mtumiaji mkubwa katika uchumi wa nchi masikini ni serikali. Ukimwondoa mtumiaji huyu basi uchumi mzima unatatizika na hali hiyo ikiendelea uchumi wa nchi husika huanguka baada ya miaka 3 na kuendelea, maana yake ni kuwa wakati wa uchaguzi 2020 mkuu utadhaniwa kuwa umefeli kiuchumi, na kumbe kama ungepewa miaka zaidi uchumi ungekuja kujisahihisha baada ya miaka 4 baadae na kuwa imara. Hivyo ni hatua nzuri umechukua isipokuwa kwa siasa zetu itakupa shida 2020. Usipokubali kukataliwa unaweza kujiandikia historia ya kumwaga damu sana 2020, nakueleza ukweli mkuu, najua ninachoandika ila siwezi kuandika mengi, namna hii mkuu 2020 sijui!!!

15. Sitaki nikuchoshe

16. Sitaki nikuchoshe

17 Sitaki nikuchoshe na naishia hapa

17. maana nikiandika mengi huenda usisome, wakati nafikiri ni muhimu sana ukasoma haya mambo ili ufanye marekebisho kidogo ....kungaliko mapema.

SOLUTION/UTATUZI:

Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila.........

Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.
Bull sheet zile zile, hamna cha maana ulichoandika.
 
Kiukweli wafanya kazi sidhani kama atapata kura zao mwaka 2020
Uliyoyaandika hapo yameugusa moyo wangu KWA kuwa siyangu mwenye ujumbe wake atatolea kauli
 
Kwa hiyo Watanzania wote 45m ni wafanyakazi na wana wakuu wa idara? Naona hata yeye mwenyewe JPM anafikiri kuwa kila mtu ni mfanyakazi na anapiga dili tu. Thinking while living in a cubicle!
Huo ni mfano tu kiongozi sijasema wa tz wote ni wafanyakazi ila kiukweli alivyotukanwa na kudharauliwa Bw Kikwete zama zake ilitosha kupata hili jembe litunyooshee tu.

Ila wa Tz nomaa
Ukiwa mpole nongwa
Ukiwa mkali pia nongwa
Tz nini mnataka jamani..aje malaika najua naye atakuwa mpole na watu watasema tuu .
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hayo ni maoni yako ila kundi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ikawa ndio tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.
Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana mfano tu mdogo wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni kama miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.na wamekuwa hata ushauri wakiomba kwa wafanyakazi wa chini,

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni.

Piga kazi mkuu kila kitu utakiona sawa tu.

Watanzania sijui mtasaidiwa vipi.
 
Huo ni mfano tu kiongozi sijasema wa tz wote ni wafanyakazi ila kiukweli alivyotukanwa na kudharauliwa Bw Kikwete zama zake ilitosha kupata hili jembe litunyooshee tu.

Ila wa Tz nomaa
Ukiwa mpole nongwa
Ukiwa mkali pia nongwa
Tz nini mnataka jamani..aje malaika najua naye atakuwa mpole na watu watasema tuu .

Sasa ndugu yangu extreme moja huwa haiwi replaced na extreme ingine. Chakula kikiwa na chumvi sana hutii sukari nyingi sana kukifanya kiwe kitamu! JK alikuwa na mapungufu yake mengi sana na alikosolewa sana (sio kutukanwa kama unavyodai) ila na JPM ana mapungufu mengi tena na ya hatari zaidi ikiwemo kutoheshimu utawala wa sheria!
Katu usiseme kuwa JPM ni nafuu ya JPM...naye akikosea atakosolewa tu.
 
blah blah blah...
10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;

11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.).
Ndugu yangu Ninja, ninalo swalo moja tu kwako, je hii CCM iliyojengwa kuanzia miaka ya 95, Magufuli alikuwa ni sehemu yake au huyu Magufuli kashushwa tu kutoka mbinguni?
SOLUTION/UTATUZI: Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila..........
Ndugu yangu Ninja, hebu nipe ufafanuzi kidogo hapa...huyo unayemtaka aongeze bidii ni huyu huyu Magufuli wetu mtakatifu asiyejaribiwa? Hizo bidii unazotaka aongeze alizianza lini?
Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.
Na wewe nakutakia heri ya mwaka mpya ndugu yangu Ninja! Kalaghabaho!
 
Makosa haya ya kimkakati yatasababisha umalize miaka 5 kwa mafanikio finyu sana

1. Una nia ya dhati ya kulipeleka taifa hili mbele, lakini unateua watu wenye uwezo mkubwa wa kutenda ila hawana nia ya kutenda na nitafafanua vizuri kwenye namba zinazofuata.

2. Unaruhusu vyombo vya dola kufanya baadhi ya matendo wakidhani wanatetea hadhi yako kumbe wanachochea chuki ya wananchi dhidi yako kwa matendo ambayo wewe hukuyaidhinisha kwa sababu kuna washauri wako wa kiusalama wamekuonya kuwa ukiingilia maamuzi ya vyombo vya dola, utawavunja moyo na hivyo utahatarisha usalama na ulinzi wa nchi. Wanakudanganya, kumbuka wewe ndiye amiri jeshi mkuu hivyo hawatakiwi kuchukua maamuzi yanayogusa maslahi ya taasisi ya Rais bila wewe kuridhia. Usikubali kuingizwa mkenge.

3. Mbona kwa vyombo vingine unatumbua, mfano 'Treasury Registrar', 'CEO NIMR', TANESCO n.k? au ndio ile mishahara inayozidi shs 15 mil, unatoa aliyezidi halafu anayeingia unampa 'ceiling price'.

4. Watumishi wa umma wana mishahara midogo kiujumla hivyo japo umefanya vema kufyeka madili yao kuanzia 10% ya manunuzi, safari za nje, safari za ndani pia, bajeti za matanuzi, watumishi hewa n.k, hata hivyo ujue hiyo ndiyo ilikua 'motivation' yao kufanya kazi, hivyo ukae ukijua asilimia zaidi ya 70% ya watumishi wa umma hawakupendi. Watatabasamu tu usoni lakini umewakata miguu hivyo wanakuchukia sana. Sio wao tu hata na ndugu zao wanaowategemea.

5. Asilimia kubwa ya wafanyabiashara masikini waliokuwa wanawategemea hawa watumishi wa umma ili biashara zao ziende hawakupendi kwa sasa. Haimaanishi umefanya vibaya mkuu wa nchi, hapana, bali umeng'oa jino bila ganzi hivyo kabla haya maumivu hayajaisha itakua 2020, usitegemee hawa watu watakuunga mkono.

6. Kimsingi mkuu wa nchi kwa sasa unapendwa na watu kama ndg Makonda na ndg. Polepole kwa kuwa umewapa kitu ambacho hawakuwahi kukiota maishani mwao, na sio kwa sababu ya mapenzi ya dhati hivyo usije kudhani wanakupeeenda hapana ni maslahi tu.

7. Pia unapendwa na watu kama mimi ambao tunaangalia nia yako ya dhati na sio maumivu haya ya muda mfupi. Hata hivyo mtazamo huu bado sana kwa nchi yetu, hivyo hata mimi nakua na mtazamo kama wako yaani mtazamo wa haki lakini sio mtazamo sahihi kwa wakati sahihi.

8. Hivyo ujue (rejea namba 1) umeteua PHD's ambao wanatetemeka sana kwamba watafanyaje kwenye hivyo vyeo ili na wao wasitumbuliwe. Pia umeonyesha kwao kuwa na 'micro-management' hivyo hawajui kama wanapoingia kazini wakae kimya na kuweka 'autopilot' kama Ryoba wa TBC kuogopa utumbuzi au wawe 'creative' lakini kwa kukusoma vizuri kama Makonda wa DSM, sasa sijui wakachukue kozi kwa Makonda? (how to understand JPM).

9. Kwa jinsi ulivyo Rais wa watu tena wanyonge, ulitakiwa usikilize ushauri wa washauri wako wasio na woga kisha ufanye maamuzi sahihi, lakini ujue kabisa mkuu wangu, umezungukwa na washauri waoga kuliko maelezo, na ndio maana wanakupa ushauri kikasuku kasuku kwa kuogopa kutumbuliwa, hawa washauri wa hivi ndio wanasababisha uonekane kwa baadhi ya watu kuwa 'dikteta'.

10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;

11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.)

12. Mkuu CCM hiyo imeshakufa, hunayo tena mkuu. Sasa hivi kuna CCM 'Chama Cha Magufuli'. Ila CCM ya mwaka juzi ile ya 'Chama Cha Madili' haipo. Kwa kifupi ninamaanisha utajidanganya sana kama ukidhani kwa kuweka viraka kwenye CCM utakua na mafanikio, mkuu wangu hiyo CCM uliyo nayo haiendani na wewe hata kidogo, kuna manung'uniko mazito sana hata kwa walio karibu kabisa na wewe, yaani kwa CCM hiyo watu wanatamani 2020 ifike leo ili waondoe huu 'mzimu' wa JPM wapumue, maana wana miaka 4 ya kushindwa kupiga dili.

13. Sijui unawasaidiaje wananchi wanyonge ambao na wao wamefaidika siku zote na mfumo dhalimu ambao umewanyonya pale na kuwafaidisha hapa. Yaani ni kwamba huu mfumo unaopambana nao mkuu wangu kila unapoupiga pigo moja, mapigo kumi yanaenda kwa wale wale wanyonge unaowatetea. Huyo mama ntilie unayemtetea leo hii hana mauzo kwa sababu wateja wake ni hao hao wapiga dili kwa njia hii au ile.

14. Mtumiaji mkubwa katika uchumi wa nchi masikini ni serikali. Ukimwondoa mtumiaji huyu basi uchumi mzima unatatizika na hali hiyo ikiendelea uchumi wa nchi husika huanguka baada ya miaka 3 na kuendelea, maana yake ni kuwa wakati wa uchaguzi 2020 mkuu utadhaniwa kuwa umefeli kiuchumi, na kumbe kama ungepewa miaka zaidi uchumi ungekuja kujisahihisha baada ya miaka 4 baadae na kuwa imara. Hivyo ni hatua nzuri umechukua isipokuwa kwa siasa zetu itakupa shida 2020. Usipokubali kukataliwa unaweza kujiandikia historia ya kumwaga damu sana 2020, nakueleza ukweli mkuu, najua ninachoandika ila siwezi kuandika mengi, namna hii mkuu 2020 sijui!!!

15. Sitaki nikuchoshe

16. Sitaki nikuchoshe

17 Sitaki nikuchoshe na naishia hapa

17. maana nikiandika mengi huenda usisome, wakati nafikiri ni muhimu sana ukasoma haya mambo ili ufanye marekebisho kidogo ....kungaliko mapema.

SOLUTION/UTATUZI:

Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila.........

Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.

Umesema kweli mkuu na ukweli upo centred kwenye number 11...Na kisiasa kweli is a big blow kwake...Challenge kubwa aliyonayo ni kama Hayati baba wa Taifa aliyokuwa nayo by then....Wakati baba wa Taifa hakuwa na watu wenye uelewa sawa na yeye ki ideology na elimu...Mh. Kwa sasa anao hao uliowataja number 11...Its a challenging situation... If you ask Ame the solution is aamini taasisi kuliko indivuduals na akizitumia taasisi vizuri huku akiweka monitoring system nzuri inayompa feed back ya kweli anawrza kuwachuja hao walio kwenye number 11....Hao wengi wana kadi na kadi hizo si kingine zaidi ya maslahi waliyonayo aidha katika nafasi hizo au kwa watu waliowapachika hapa...Hao waliopachikwa wengine walitengenezewa CVs mpaka waka fika high ranks...Utaona kwenye tathmini ya uhakiki wa watumishi.. Grades za wengine ilikuwa vichekesho lakini ukiona CV zao na exposure utazimia mwenyewe....Kiuhalisia wengi wao wali assume hizo nafasi prematurely.... Inasikitisha! Ugonjwa huu unfortunately uliingia mpaka kwenye taaluma yaani vyuo vikuu...watu ambao wangeweza kulinda maslahi fulani walikuwa wanapanda kwaku serereka na pengine wenye efforts constraints wanazokumbana nazo zilikuwa si za kawaida.. Ki uhalisia elites karibu wote tume kuwa corrupted....

Lastly niongee kama mtumishi wa Mungu...all is not lost...Mh. Nakushauri tulia mbele za Mungu uombe ujazo wa roho mtakatifu akupe wisdom and understanding how to go in and out hatimaye uweze kuyashinda haya yote. Makwazo hayana budi kuja lakini ole wake yule ayasababishaye, ingekuwa heri kama angelifungiwa jiwe la kusagia na kutupwa baharini....Mimi kama mdau wa utawala huu nakuhakikishia hakuna kushindwa kwakua yote yawezekana kwake aaminiye...Mungu anaenda kutengeneza mazingira ya wewe kufanikiwa. Atakupa watu ambao watakuelewa, wenye nia na malengo sawa na yako na hao watakuwa na moyo wa kutenda ambao hawatatambua hali hiyo inatoka wapi...Usifadhaike wala usihuzunike, jipe moyo mkuu wewe ni amiri jeshi mkuu na kama una imani kwa Mungu huyu mimi ninayemtumikia na siyo mwingine tofauti tambua kuwa hakuna kushindwa kwakua tunaye wakuaminika, asiye na alama ya kubadilika badilika lakini tu anasema KUWA JASIRI...Hata kama ukikutana na bahari ya shamu hiyo bahari ndiyo ulinzi wako ambapo kwayo maadui zako wataangamia ili wewe uvuke salama nakuendelea na safari...

Heri ya mwaka mpya!
 
Nawewe unaomba kirejareja? Lakini bahati mbaya huna sifa, elimu yenyewe kiduchu, labda ujaribu upande ule wa UKUTA.
Nyie ndio wale wale unaweza kuwa naelimu kubwa lakini ukakosa ufaham wa uongozi na ukakosa elim ukawa naupeo mkubwa hivi raisi akipewa ushauri na mtu kama baghresa utasema asimsikilize kwakua hana elimu????
 
Watumishi stahiki zao wamelipwa? Malimbikizo yao yamelipwa?
2020 iyoo
Tume huru ya uchaguzi Tanzania idaiwe

Watalipwa kwa reserve ipi aliyoachiwa na hao wakombozi uchwara? They took everything puting them under their authorities...So sad wamechukua hadi confidence za wananchi kwakua tu waliwazoesha kuwatumikisha kwa faida zao binafsi...Mimi huyu hata wote mgeuke nitabaki peke yangu kupambana nao...Hata sasa nilishawavuruga wakavurugika....
 
Mkuu, sababu aliyotoa NI MTAZAMO TU, ni kubwa sana, labda kama wewe si mtumishi wa uma au ni kigogo ama una mahusiano makubwa na vigogo.

Wafanyakazi wa chini walinyanyasika sana, uhamisho wa ovyo, kunyimwa safari, seminars, ovetime nk.
Kulikuwa na watu maalumu waliokuwa wakisafiri, wengine hawafai. Kulikuwa na watu maalumu wanoenda semina, wanapewa vitengo maalum vya ulaji, ukihoji unapata uhamisho. Lakini tangu zama hii imeingia hakuna safari za hovyo, na ikitokea anaenda mtu wa kitengo husika tena aliye mpetent. Maana kwanza lazima ruhusa inayoombwa ieleze kwanini mtumishi asafiri, itagharimu shilingi ngapi? Nini manufaa ya safari hiyo kwa taifa?

Hivyo, sababu aliyotoa NI MTAZAMO TU. ina mashiko, hivi sasa mnajadiliana na mkuu na anakusikiliza.

Kwa upande mwingine hata utendaji, umebadilika KAMBAKU! Kwani husikii raia wanafurahia wakienda maofisini? Wanasema watumishi wamebadilika sana, wanajituma.

Wahivyo ni wale wafaidika wa mfumo fisadi....Walizoea kula makombo sasa meza zimekauka nothing falls down... Tunao mwelewa tuko wengi ila hatuna access kwenye kwakua hatuna senti za kununua bites....wao bado change wanazo....
 
Nani ampende wanavyoona wenzao wanavyodhalilishwa na kufukuzwa hadharani?
Acha urongo...mimi ni mtumishi wa umma na ninampenda mpaka wakati mwingine nakosa balance hata nisione makosa dhahiri yanayofanyika....Wasiompenda ni wale ma bwanyenye miungu watu waliokuwepo kwenye ofisi za umma...Be informed...Fanya utafiti uone!
 
Hata wewe pia unaweza kuwa unajidanganya hapo unapofanya kazi. Kiukweli huyu mleta uzi amegusia mambo muhimu kwa huyu mkuu wa nchi yetu. Ni muhimu akawasikiliza washauri bora na sio bora washauri.
Hivi mnaosema hasikilizi washauri mmejuaje?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
huyu jamaa alipotea siku ile alipompeleka yule mama kuwa spika. wengi tuliokuwa na imani naye tukakata tamaa.

kilichofuata. kilikuwa ni kituko eti watuhumiwa wa ufisadi wakateuliwa kuwa wenyeviti wa kamati za bunge.
akaendelea kuchemka akazima binge livu.

akavunja tatatibu za utumishi wa umma kwa kuteua makada.

kwaatukio yote naengineengi ya hpvyo sidhani ka atatoboa 2020
Mbona kuna mtuhumiwa wa ufisadi aliyethibitishwa na adhabu akapewa amekaribishwa kugombea ukuu wa nchi je angefanikiwa kuukwaa urais si naye angekuwa Rais Fisadi?
 
Back
Top Bottom