Kwa Rais Magufuli tu - Must Read 2017

Ninja

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
341
500
Makosa haya ya kimkakati yatasababisha umalize miaka 5 kwa mafanikio finyu sana

1. Una nia ya dhati ya kulipeleka taifa hili mbele, lakini unateua watu wenye uwezo mkubwa wa kutenda ila hawana nia ya kutenda na nitafafanua vizuri kwenye namba zinazofuata.

2. Unaruhusu vyombo vya dola kufanya baadhi ya matendo wakidhani wanatetea hadhi yako kumbe wanachochea chuki ya wananchi dhidi yako kwa matendo ambayo wewe hukuyaidhinisha kwa sababu kuna washauri wako wa kiusalama wamekuonya kuwa ukiingilia maamuzi ya vyombo vya dola, utawavunja moyo na hivyo utahatarisha usalama na ulinzi wa nchi. Wanakudanganya, kumbuka wewe ndiye amiri jeshi mkuu hivyo hawatakiwi kuchukua maamuzi yanayogusa maslahi ya taasisi ya Rais bila wewe kuridhia. Usikubali kuingizwa mkenge.

3. Mbona kwa vyombo vingine unatumbua, mfano 'Treasury Registrar', 'CEO NIMR', TANESCO n.k? au ndio ile mishahara inayozidi shs 15 mil, unatoa aliyezidi halafu anayeingia unampa 'ceiling price'.

4. Watumishi wa umma wana mishahara midogo kiujumla hivyo japo umefanya vema kufyeka madili yao kuanzia 10% ya manunuzi, safari za nje, safari za ndani pia, bajeti za matanuzi, watumishi hewa n.k, hata hivyo ujue hiyo ndiyo ilikua 'motivation' yao kufanya kazi, hivyo ukae ukijua asilimia zaidi ya 70% ya watumishi wa umma hawakupendi. Watatabasamu tu usoni lakini umewakata miguu hivyo wanakuchukia sana. Sio wao tu hata na ndugu zao wanaowategemea.

5. Asilimia kubwa ya wafanyabiashara masikini waliokuwa wanawategemea hawa watumishi wa umma ili biashara zao ziende hawakupendi kwa sasa. Haimaanishi umefanya vibaya mkuu wa nchi, hapana, bali umeng'oa jino bila ganzi hivyo kabla haya maumivu hayajaisha itakua 2020, usitegemee hawa watu watakuunga mkono.

6. Kimsingi mkuu wa nchi kwa sasa unapendwa na watu kama ndg Makonda na ndg. Polepole kwa kuwa umewapa kitu ambacho hawakuwahi kukiota maishani mwao, na sio kwa sababu ya mapenzi ya dhati hivyo usije kudhani wanakupeeenda hapana ni maslahi tu.

7. Pia unapendwa na watu kama mimi ambao tunaangalia nia yako ya dhati na sio maumivu haya ya muda mfupi. Hata hivyo mtazamo huu bado sana kwa nchi yetu, hivyo hata mimi nakua na mtazamo kama wako yaani mtazamo wa haki lakini sio mtazamo sahihi kwa wakati sahihi.

8. Hivyo ujue (rejea namba 1) umeteua PHD's ambao wanatetemeka sana kwamba watafanyaje kwenye hivyo vyeo ili na wao wasitumbuliwe. Pia umeonyesha kwao kuwa na 'micro-management' hivyo hawajui kama wanapoingia kazini wakae kimya na kuweka 'autopilot' kama Ryoba wa TBC kuogopa utumbuzi au wawe 'creative' lakini kwa kukusoma vizuri kama Makonda wa DSM, sasa sijui wakachukue kozi kwa Makonda? (how to understand JPM).

9. Kwa jinsi ulivyo Rais wa watu tena wanyonge, ulitakiwa usikilize ushauri wa washauri wako wasio na woga kisha ufanye maamuzi sahihi, lakini ujue kabisa mkuu wangu, umezungukwa na washauri waoga kuliko maelezo, na ndio maana wanakupa ushauri kikasuku kasuku kwa kuogopa kutumbuliwa, hawa washauri wa hivi ndio wanasababisha uonekane kwa baadhi ya watu kuwa 'dikteta'.

10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;

11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.)

12. Mkuu CCM hiyo imeshakufa, hunayo tena mkuu. Sasa hivi kuna CCM 'Chama Cha Magufuli'. Ila CCM ya mwaka juzi ile ya 'Chama Cha Madili' haipo. Kwa kifupi ninamaanisha utajidanganya sana kama ukidhani kwa kuweka viraka kwenye CCM utakua na mafanikio, mkuu wangu hiyo CCM uliyo nayo haiendani na wewe hata kidogo, kuna manung'uniko mazito sana hata kwa walio karibu kabisa na wewe, yaani kwa CCM hiyo watu wanatamani 2020 ifike leo ili waondoe huu 'mzimu' wa JPM wapumue, maana wana miaka 4 ya kushindwa kupiga dili.

13. Sijui unawasaidiaje wananchi wanyonge ambao na wao wamefaidika siku zote na mfumo dhalimu ambao umewanyonya pale na kuwafaidisha hapa. Yaani ni kwamba huu mfumo unaopambana nao mkuu wangu kila unapoupiga pigo moja, mapigo kumi yanaenda kwa wale wale wanyonge unaowatetea. Huyo mama ntilie unayemtetea leo hii hana mauzo kwa sababu wateja wake ni hao hao wapiga dili kwa njia hii au ile.

14. Mtumiaji mkubwa katika uchumi wa nchi masikini ni serikali. Ukimwondoa mtumiaji huyu basi uchumi mzima unatatizika na hali hiyo ikiendelea uchumi wa nchi husika huanguka baada ya miaka 3 na kuendelea, maana yake ni kuwa wakati wa uchaguzi 2020 mkuu utadhaniwa kuwa umefeli kiuchumi, na kumbe kama ungepewa miaka zaidi uchumi ungekuja kujisahihisha baada ya miaka 4 baadae na kuwa imara. Hivyo ni hatua nzuri umechukua isipokuwa kwa siasa zetu itakupa shida 2020. Usipokubali kukataliwa unaweza kujiandikia historia ya kumwaga damu sana 2020, nakueleza ukweli mkuu, najua ninachoandika ila siwezi kuandika mengi, namna hii mkuu 2020 sijui!!!

15. Sitaki nikuchoshe

16. Sitaki nikuchoshe

17 Sitaki nikuchoshe na naishia hapa

17. maana nikiandika mengi huenda usisome, wakati nafikiri ni muhimu sana ukasoma haya mambo ili ufanye marekebisho kidogo ....kungaliko mapema.

SOLUTION/UTATUZI:

Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila.........

Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.
 
NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
2,000
Hayo ni maoni yako ila kundi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ikawa ndio tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana mfano tu mdogo wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni kama miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.na wamekuwa hata ushauri wakiomba kwa wafanyakazi wa chini,

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni.

Piga kazi mkuu kila kitu utakiona sawa tu.
 
mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
4,061
2,000
Makosa haya ya kimkakati yatasababisha umalize miaka 5 kwa mafanikio finyu sana

1. Una nia ya dhati ya kulipeleka taifa hili mbele, lakini unateua watu wenye uwezo mkubwa wa kutenda ila hawana nia ya kutenda na nitafafanua vizuri kwenye namba zinazofuata
2. Unaruhusu vyombo vya dola kufanya baadhi ya matendo wakidhani wanatetea hadhi yako kumbe wanachochea chuki ya wananchi dhidi yako kwa matendo ambayo wewe hukuyaidhinisha kwa sababu kuna washauri wako wa kiusalama wamekuonya kuwa ukiingilia maamuzi ya vyombo vya dola, utawavunja moyo na hivyo utahatarisha usalama na ulinzi wa nchi. Wanakudanganya, kumbuka wewe ndiye amiri jeshi mkuu hivyo hawatakiwi kuchukua maamuzi yanayogusa maslahi ya taasisi ya Rais bila wewe kuridhia. Usikubali kuingizwa mkenge
3. Mbona kwa vyombo vingine unatumbua, mfano 'Treasury Registrar', 'CEO NIMR', TANESCO n.k? au ndio ile mishahara inayozidi shs 15 mil, unatoa aliyezidi halafu anayeingia unampa 'ceiling price'
4. Watumishi wa umma wana mishahara midogo kiujumla hivyo japo umefanya vema kufyeka madili yao kuanzia 10% ya manunuzi, safari za nje, safari za ndani pia, bajeti za matanuzi, watumishi hewa n.k, hata hivyo ujue hiyo ndiyo ilikua 'motivation' yao kufanya kazi, hivyo ukae ukijua asilimia zaidi ya 70% ya watumishi wa umma hawakupendi. Watatabasamu tu usoni lakini umewakata miguu hivyo wanakuchukia sana. Sio wao tu hata na ndugu zao wanaowategemea.
5. Asilimia kubwa ya wafanyabiashara masikini waliokuwa wanawategemea hawa watumishi wa umma ili biashara zao ziende hawakupendi kwa sasa. Haimaanishi umefanya vibaya mkuu wa nchi, hapana, bali umeng'oa jino bila ganzi hivyo kabla haya maumivu hayajaisha itakua 2020, usitegemee hawa watu watakuunga mkono.
6. Kimsingi mkuu wa nchi kwa sasa unapendwa na watu kama ndg Makonda na ndg. Polepole kwa kuwa umewapa kitu ambacho hawakuwahi kukiota maishani mwao, na sio kwa sababu ya mapenzi ya dhati hivyo usije kudhani wanakupeeenda hapana ni maslahi tu.
7. Pia unapendwa na watu kama mimi ambao tunaangalia nia yako ya dhati na sio maumivu haya ya muda mfupi. Hata hivyo mtazamo huu bado sana kwa nchi yetu, hivyo hata mimi nakua na mtazamo kama wako yaani mtazamo wa haki lakini sio mtazamo sahihi kwa wakati sahihi.
8. Hivyo ujue (rejea namba 1) umeteua PHD's ambao wanatetemeka sana kwamba watafanyaje kwenye hivyo vyeo ili na wao wasitumbuliwe. Pia umeonyesha kwao kuwa na 'micro-management' hivyo hawajui kama wanapoingia kazini wakae kimya na kuweka 'autopilot' kama Ryoba wa TBC kuogopa utumbuzi au wawe 'creative' lakini kwa kukusoma vizuri kama Makonda wa DSM, sasa sijui wakachukue kozi kwa Makonda? (how to understand JPM)
9. Kwa jinsi ulivyo Rais wa watu tena wanyonge, ulitakiwa usikilize ushauri wa washauri wako wasio na woga kisha ufanye maamuzi sahihi, lakini ujue kabisa mkuu wangu, umezungukwa na washauri waoga kuliko maelezo, na ndio maana wanakupa ushauri kikasuku kasuku kwa kuogopa kutumbuliwa, hawa washauri wa hivi ndio wanasababisha uonekane kwa baadhi ya watu kuwa 'dikteta'
10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;
11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.),
12. Mkuu CCM hiyo imeshakufa, hunayo tena mkuu. Sasa hivi kuna CCM 'Chama Cha Magufuli'. Ila CCM ya mwaka juzi ile ya 'Chama Cha Madili' haipo. Kwa kifupi ninamaanisha utajidanganya sana kama ukidhani kwa kuweka viraka kwenye CCM utakua na mafanikio, mkuu wangu hiyo CCM uliyo nayo haiendani na wewe hata kidogo, kuna manung'uniko mazito sana hata kwa walio karibu kabisa na wewe, yaani kwa CCM hiyo watu wanatamani 2020 ifike leo ili waondoe huu 'mzimu' wa JPM wapumue, maana wana miaka 4 ya kushindwa kupiga dili.
13. Sijui unawasaidiaje wananchi wanyonge ambao na wao wamefaidika siku zote na mfumo dhalimu ambao umewanyonya pale na kuwafaidisha hapa. Yaani ni kwamba huu mfumo unaopambana nao mkuu wangu kila unapoupiga pigo moja, mapigo kumi yanaenda kwa wale wale wanyonge unaowatetea. Huyo mama ntilie unayemtetea leo hii hana mauzo kwa sababu wateja wake ni hao hao wapiga dili kwa njia hii au ile.
14. Mtumiaji mkubwa katika uchumi wa nchi masikini ni serikali. Ukimwondoa mtumiaji huyu basi uchumi mzima unatatizika na hali hiyo ikiendelea uchumi wa nchi husika huanguka baada ya miaka 3 na kuendelea, maana yake ni kuwa wakati wa uchaguzi 2020 mkuu utadhaniwa kuwa umefeli kiuchumi, na kumbe kama ungepewa miaka zaidi uchumi ungekuja kujisahihisha baada ya miaka 4 baadae na kuwa imara. Hivyo ni hatua nzuri umechukua isipokuwa kwa siasa zetu itakupa shida 2020. Usipokubali kukataliwa unaweza kujiandikia historia ya kumwaga damu sana 2020, nakueleza ukweli mkuu, najua ninachoandika ila siwezi kuandika mengi, namna hii mkuu 2020 sijui!!!
15. Sitaki nikuchoshe
16. Sitaki nikuchoshe
17 Sitaki nikuchoshe na naishia hapa 17. maana nikiandika mengi huenda usisome, wakati nafikiri ni muhimu sana ukasoma haya mambo ili ufanye marekebisho kidogo ....kungaliko mapema.

SOLUTION/UTATUZI:

Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila.........

Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.
Sizonje hafanani na ushauri hata mmoja!! hapo. He is full of himself!! Much know!! Next to goddesses, A saint from h---.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,337
2,000
Hayo ni maoni yako ila kindi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ndio ikawa tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana maana wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni
Ni sababu hii tu mkuu au kuna zingine?
 
Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,019
2,000
Hayo ni maoni yako ila kindi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ndio ikawa tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana maana wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni
Hata wewe pia unaweza kuwa unajidanganya hapo unapofanya kazi. Kiukweli huyu mleta uzi amegusia mambo muhimu kwa huyu mkuu wa nchi yetu. Ni muhimu akawasikiliza washauri bora na sio bora washauri.
 
Ninja

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
341
500
Hayo ni maoni yako ila kindi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ndio ikawa tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana maana wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni
Hizo nyekundu zimenifanya nijue sio mlengwa aliyejibu,

Hata hivyo nakuomba urejee namba 6 na 7. Tuko tunaompenda ila kwa sasa tuko wachache sana na hali inaendelea vibaya.

Kama unampenda basi lazima utakua unamwombea, maana JPM hana jingine analotusisitizia tumsaidie zaidi ya kumwombea, sasa kwa mwombaji ambaye anadhani mambo yote ni shwari wakati kuna tatizo huyo ni hatari sana, maana sio mlinzi mzuri kwa JPM.

Kama kweli unampenda JPM, basi tambua ukweli halisi uliopo na kisha tafadhali muombee, na pia ukiweza mshauri kama unaweza lakini. Au wewe unaishi wapi ndugu yangu?
 
Ninja

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
341
500
Nawewe unaomba kirejareja? Lakini bahati mbaya huna sifa, elimu yenyewe kiduchu, labda ujaribu upande ule wa UKUTA.
hahaha mkuu una utani wa ngumi, si kweli kwamba naomba kireja reja, ila ni kweli nina elimu kiduchu maana sina PhD. Kwa maana hiyo tu ya kutokuwa na PhD na si kingine.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom