Kwa Rais Magufuli tu - Must Read 2017

Kwa Rais Magufuli tu - Must Read 2017

Kwani na yeye anasomaga haya maneno ? Kwani hii anajua bado iko?
 
Kwani na yeye anasomaga haya maneno ? Kwani hii anajua bado iko?

Anasoma kurasa zaidi ya 600 kwa siku. Yaani kamzidi Warren Buffet kusoma.

Labda sasa aanze kusoma na mambo ya uongozi, mahusiano, watu n.k imsaidie kwenye uongozi wake. Maana unapokuwa "(Emotional + Mechanical )" utahitaji sana "people skills" na "leadership wisdom" kusonga mbele vinginevyo utabaki na nia njema na matunda sifuri.

"listening is not just hearing"
 
Hayo ni maoni yako ila kundi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ikawa ndio tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana mfano tu mdogo wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni kama miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.na wamekuwa hata ushauri wakiomba kwa wafanyakazi wa chini,

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni.

Piga kazi mkuu kila kitu utakiona sawa tu.
Sidhani kama wewe ni mfanyakazi, labda housegirl/ houseboy. Mawazo yako hayawezi kuwa ya mtu mwenye ufahamu
 
Sidhani kama wewe ni mfanyakazi, labda housegirl/ houseboy. Mawazo yako hayawezi kuwa ya mtu mwenye ufahamu
Ni mfanya kazi mkuu naendesha maisha kwa pesa ya mshahara toka kwa bwana Pombe kiongozi.ila sina mihemuko huwa ninasubira nikijua serikali ya mzee Pombe bado changa.(mwaka mmoja sasa)
 
Hayo ni maoni yako ila kundi linalompenda nikubwa sana kuliko uzaniavyo, usije ukawa unashinda hapa jf na ikawa ndio tathimin yako kuwa Bw Pombe hapendwi.

Kwa sisi wafanyakazi tunampenda sana mfano tu mdogo wakubwa wengi wa Idara zama zilee walikuwa ni kama miungu watu ila sasa wamekuwa wa kaida sana tuu.na wamekuwa hata ushauri wakiomba kwa wafanyakazi wa chini,

Kikubwa usijidanganye wala kudanganywa na story za vijiweni.

Piga kazi mkuu kila kitu utakiona sawa tu.
Nina wasiwasi na wewe! kama uu mfanyakazi kweli labda mpasua mbao misituni tena ya wizi! uandishi wako sio ya mfanyakazi bali kama mganja njaa wa Lumumba vile!
 
Nina wasiwasi na wewe! kama uu mfanyakazi kweli labda mpasua mbao misituni tena ya wizi! uandishi wako sio ya mfanyakazi bali kama mganja njaa wa Lumumba vile!
Ha ha ha ha ha sina elimu kama wewe mkuu ,mimi ni std 7 tu ila huo NI MTAZAMO TU
 
Mtoa mada hapa dah! Ungeangalia post yako kabla ya kutuma
 
Naomba namba ya JPM nijitoe mhanga nimfowadie haka ka walaka kazito sana, au nipe email take maana mimi sina cha kupoteza iwe milioni saba, kifungo au vyote viwili.
Kwa nn unasema huna cha Kupoteza? NIMECHEKA SANA.
Tunaweza kukukuta kwenye mfuko wa plastic kule mto ruvu. Ww huna chakupoteza lkn cc tutakuwa tumekupoteza uking'olewa kucha na meno
 
ukithubutu kusimama mbele yake, huku ukiwa unawaza kumshauli kitu. hahahahaahahahahaha
unaweza kugaili na kuishia kumsalimia tu.
 
ukithubutu kusimama mbele yake, huku ukiwa unawaza kumshauli kitu. hahahahaahahahahaha
unaweza kugaili na kuishia kumsalimia tu.

Na ndicho kinachowapata mawaziri wetu. Waulize mawaziri wakwambie.

Mmoja aliwahi kutoa mfano akisema "umewahi kusafiri na mtumbwi peke yako baharini usiku wa manane halafu ghafla unaona kama kivuli kinakujia kwa kasi kubwa kutoka mbali, na hujui ni binadamu au ni kitu gani" akasema ile hofu unayokuwa nayo ndiyo unayokuwa nayo unapokuwa mbele ya Magufuli ukitafakari namna ya kutamka jambo mbele yake.

Sijui kuna ukweli gani kwenye hilo. Na kama ni hivyo, sijui unatoaje ushauri au maoni au lolote la maana katika hali hiyo!.

Mkuu wa nchi "do not discourage opinions please! you need to be briefed, criticised, informed...e.t.c a lot more than you can think of..."
 
Makosa haya ya kimkakati yatasababisha umalize miaka 5 kwa mafanikio finyu sana

1. Una nia ya dhati ya kulipeleka taifa hili mbele, lakini unateua watu wenye uwezo mkubwa wa kutenda ila hawana nia ya kutenda na nitafafanua vizuri kwenye namba zinazofuata.

2. Unaruhusu vyombo vya dola kufanya baadhi ya matendo wakidhani wanatetea hadhi yako kumbe wanachochea chuki ya wananchi dhidi yako kwa matendo ambayo wewe hukuyaidhinisha kwa sababu kuna washauri wako wa kiusalama wamekuonya kuwa ukiingilia maamuzi ya vyombo vya dola, utawavunja moyo na hivyo utahatarisha usalama na ulinzi wa nchi. Wanakudanganya, kumbuka wewe ndiye amiri jeshi mkuu hivyo hawatakiwi kuchukua maamuzi yanayogusa maslahi ya taasisi ya Rais bila wewe kuridhia. Usikubali kuingizwa mkenge.

3. Mbona kwa vyombo vingine unatumbua, mfano 'Treasury Registrar', 'CEO NIMR', TANESCO n.k? au ndio ile mishahara inayozidi shs 15 mil, unatoa aliyezidi halafu anayeingia unampa 'ceiling price'.

4. Watumishi wa umma wana mishahara midogo kiujumla hivyo japo umefanya vema kufyeka madili yao kuanzia 10% ya manunuzi, safari za nje, safari za ndani pia, bajeti za matanuzi, watumishi hewa n.k, hata hivyo ujue hiyo ndiyo ilikua 'motivation' yao kufanya kazi, hivyo ukae ukijua asilimia zaidi ya 70% ya watumishi wa umma hawakupendi. Watatabasamu tu usoni lakini umewakata miguu hivyo wanakuchukia sana. Sio wao tu hata na ndugu zao wanaowategemea.

5. Asilimia kubwa ya wafanyabiashara masikini waliokuwa wanawategemea hawa watumishi wa umma ili biashara zao ziende hawakupendi kwa sasa. Haimaanishi umefanya vibaya mkuu wa nchi, hapana, bali umeng'oa jino bila ganzi hivyo kabla haya maumivu hayajaisha itakua 2020, usitegemee hawa watu watakuunga mkono.

6. Kimsingi mkuu wa nchi kwa sasa unapendwa na watu kama ndg Makonda na ndg. Polepole kwa kuwa umewapa kitu ambacho hawakuwahi kukiota maishani mwao, na sio kwa sababu ya mapenzi ya dhati hivyo usije kudhani wanakupeeenda hapana ni maslahi tu.

7. Pia unapendwa na watu kama mimi ambao tunaangalia nia yako ya dhati na sio maumivu haya ya muda mfupi. Hata hivyo mtazamo huu bado sana kwa nchi yetu, hivyo hata mimi nakua na mtazamo kama wako yaani mtazamo wa haki lakini sio mtazamo sahihi kwa wakati sahihi.

8. Hivyo ujue (rejea namba 1) umeteua PHD's ambao wanatetemeka sana kwamba watafanyaje kwenye hivyo vyeo ili na wao wasitumbuliwe. Pia umeonyesha kwao kuwa na 'micro-management' hivyo hawajui kama wanapoingia kazini wakae kimya na kuweka 'autopilot' kama Ryoba wa TBC kuogopa utumbuzi au wawe 'creative' lakini kwa kukusoma vizuri kama Makonda wa DSM, sasa sijui wakachukue kozi kwa Makonda? (how to understand JPM).

9. Kwa jinsi ulivyo Rais wa watu tena wanyonge, ulitakiwa usikilize ushauri wa washauri wako wasio na woga kisha ufanye maamuzi sahihi, lakini ujue kabisa mkuu wangu, umezungukwa na washauri waoga kuliko maelezo, na ndio maana wanakupa ushauri kikasuku kasuku kwa kuogopa kutumbuliwa, hawa washauri wa hivi ndio wanasababisha uonekane kwa baadhi ya watu kuwa 'dikteta'.

10. CCM niongelee kuhusu CCM mkuu au niishie hapa? Endelea kusoma mkuu tafadhali;

11. CCM imejengwa kuanzia miaka ya 95 na kuendelea na watu ambao walifuata maslahi ndani ya chama, pamoja na watu ambao wangependa CCM itawale milele kwa kuwa maslahi yao binafsi yanalindwa ( yaani biashara zao, hadhi zao, usalama wa mali zao, mambo ya mgao wakati wa chaguzi mbalimbali, ujumbe wa NEC/CC n.k. hata kama wanaugharimia lakini ile 'power' tu n.k.)

12. Mkuu CCM hiyo imeshakufa, hunayo tena mkuu. Sasa hivi kuna CCM 'Chama Cha Magufuli'. Ila CCM ya mwaka juzi ile ya 'Chama Cha Madili' haipo. Kwa kifupi ninamaanisha utajidanganya sana kama ukidhani kwa kuweka viraka kwenye CCM utakua na mafanikio, mkuu wangu hiyo CCM uliyo nayo haiendani na wewe hata kidogo, kuna manung'uniko mazito sana hata kwa walio karibu kabisa na wewe, yaani kwa CCM hiyo watu wanatamani 2020 ifike leo ili waondoe huu 'mzimu' wa JPM wapumue, maana wana miaka 4 ya kushindwa kupiga dili.

13. Sijui unawasaidiaje wananchi wanyonge ambao na wao wamefaidika siku zote na mfumo dhalimu ambao umewanyonya pale na kuwafaidisha hapa. Yaani ni kwamba huu mfumo unaopambana nao mkuu wangu kila unapoupiga pigo moja, mapigo kumi yanaenda kwa wale wale wanyonge unaowatetea. Huyo mama ntilie unayemtetea leo hii hana mauzo kwa sababu wateja wake ni hao hao wapiga dili kwa njia hii au ile.

14. Mtumiaji mkubwa katika uchumi wa nchi masikini ni serikali. Ukimwondoa mtumiaji huyu basi uchumi mzima unatatizika na hali hiyo ikiendelea uchumi wa nchi husika huanguka baada ya miaka 3 na kuendelea, maana yake ni kuwa wakati wa uchaguzi 2020 mkuu utadhaniwa kuwa umefeli kiuchumi, na kumbe kama ungepewa miaka zaidi uchumi ungekuja kujisahihisha baada ya miaka 4 baadae na kuwa imara. Hivyo ni hatua nzuri umechukua isipokuwa kwa siasa zetu itakupa shida 2020. Usipokubali kukataliwa unaweza kujiandikia historia ya kumwaga damu sana 2020, nakueleza ukweli mkuu, najua ninachoandika ila siwezi kuandika mengi, namna hii mkuu 2020 sijui!!!

15. Sitaki nikuchoshe

16. Sitaki nikuchoshe

17 Sitaki nikuchoshe na naishia hapa

17. maana nikiandika mengi huenda usisome, wakati nafikiri ni muhimu sana ukasoma haya mambo ili ufanye marekebisho kidogo ....kungaliko mapema.

SOLUTION/UTATUZI:

Ongeza bidii kwenye kuwasikiliza watu/washauri/wadau/walalamikaji/wapinzani/wote na punguza kusema, punguza kuadhibu nje ya utaratibu. Nina mengi sana ila.........

Heri ya mwaka mpya 2017 mkuu wangu.
Article za kinafiki km enzi ya JK, wao huwa hawakosei.Ila watendaji wao tuu,hata wakibadilishwa hadi mwisho na matataizo yakiwa palepale watendaji ndio wabaya. Hata km unaweka mafuta usiweke ya kuzidi na kupotosha wengine kwanza ndipo hoja yako ije.Mara nyingine hayo mafuta yanakuja chafua hoja yako.
 
Na ndicho kinachowapata mawaziri wetu. Waulize mawaziri wakwambie.

Mmoja aliwahi kutoa mfano akisema "umewahi kusafiri na mtumbwi peke yako baharini usiku wa manane halafu ghafla unaona kama kivuli kinakujia kwa kasi kubwa kutoka mbali, na hujui ni binadamu au ni kitu gani" akasema ile hofu unayokuwa nayo ndiyo unayokuwa nayo unapokuwa mbele ya Magufuli ukitafakari namna ya kutamka jambo mbele yake.

Sijui kuna ukweli gani kwenye hilo. Na kama ni hivyo, sijui unatoaje ushauri au maoni au lolote la maana katika hali hiyo!.

Mkuu wa nchi "do not discourage opinions please! you need to be briefed, criticised, informed...e.t.c a lot more than you can think of..."
hahahahahahahahah duh!
 
Article za kinafiki km enzi ya JK, wao huwa hawakosei.Ila watendaji wao tuu,hata wakibadilishwa hadi mwisho na matataizo yakiwa palepale watendaji ndio wabaya. Hata km unaweka mafuta usiweke ya kuzidi na kupotosha wengine kwanza ndipo hoja yako ije.Mara nyingine hayo mafuta yanakuja chafua hoja yako.
Sasa hapa tusemeje? kwamba unatoa hoja, au unapinga hoja, au unamjibia aliyeandikiwa?
Inaonyesha umeanza kusoma tu ukapata kizunguzungu, na kabla ya kuelewa kilichoandikwa ukakurupuka na kuropoka kwa maandishi.
Ukitaka kushinda vita weka hasira kando, vaa hekima kisha songa mbele.
 
Sihitaji jua km upo upande wangu au lah.ILA DHANA KWAMBA WATENDAJI NDIO HAWAN AUWEZO WA WAKOSEFU SIIPENDI INAPOTOSHA WATANZANIA SANA.BORA USIITUMIE KABISA KM HUONI HASARA YAKE.HAKUNA ALIYEKULAZIMISHA IWEKA. NI TABIA SIKU HIZI HATA WANASIASA KUONGEA VITU NYENYE UJUMBE MWINGINE NA KUINGIZA JINA LA MUNGU KIRAHISI TUU.HIYO DHANA YA WATENDAJI KUWA SHIDA IMESHAPOTOSHA SANA WATANZANIA NA WANAFIKI WANAIFAIDI SANA KUJIPENDEKEZA KWA WALENGWA.
 
Mleta post kapost nahungu tupu, sisi ndiyo wafanya kazi, tunampenda JPM kwa akili zetu na miyo yetu yote kwa 100% ikiwezekana mara 1000 ya zamani.

wewe ni mfanya kazi wa ofisi gani usiyejua hata kuandika? labda ni mfanya kazi wa Lumumba.
nahungu tupu ni nini? miyo yetu ndio nini?
 
Back
Top Bottom