Kwa Prof Muhongo na Mwakyembe, Rais Kateleza kuwateua kwenye Baraza

kiweledi, Magufuli hapaswi hata kutamka jina Muhongo sidhani kama Ndugu yetu Mpendwa Mungu amlaze Pema Deo Filikunjombe leo angenyamaza kuona huyu ndg yuko kwny baraza hili la awamu ya 5.Asingenyamazaa kiukweliii.
 
Namuombea heri Mwanyamaki kwenye kesi yake ya uchaguzi dhidi ya mwakyembe.
 
Ni kitambo kidogo madereva halisi tulipaki gari pembeni kuwapisha madereva papara wafanye mbwembwe zao kisha wapite ilhali tukijua njia ina mikunjo na mawimbi mbele ila kwa kuwa madereva papara hujifanya wajuvi sana wawapo barabarani huwa tunawaacha wakakutane wenyewe na mikunjo....

Ni muda mrefu kidogo tangu bwana Magufuli ashike hatamu tumeona waliokuwa wakijiita wapinzani na wenye akili nyingi wakionekana kutekwa ama kujipendekeza dhahiri kwa bwana Mkubwa wakimtukuza kwa pambio nyingi za sifa...

Kadiri siku zisongavyo Magufuli ameanza kuonesha dhahiri mwenendo wake hasa baada ya uteuzi wa leo wale waliokuwa front line kumtetea naona wameingiwa baridi....

Ktk baraza wamechanganywa watu ambao ideologically wako tofauti kabisa na wapo wenye visasi hasa kwa lile sakata la ESCROW!!

Hivi Ole Sendeka leo anajisikiaje Muhongo kurudi Madini? Zitto je? Mwigullu? Kigwangala? Kitila Mkumbo?

Kigwangala atajisikiaje kuketi meza moja na aliyemwita mwongo?

Magufuli aligoma kumnadi Tibaijuka... Ngeleja... Chenge kwa sakata la ESCROW leo kampa uwaziri mhusika mkuu je waliomsifu Magufuli kuwakacha kuwanadi watuhumiwa wa ESCROW leo wanajisikiaje kuteuliwa Muhongo??

Waliojinadi wapinzani halisi wanajisikiaje Mwakyembe kuwa waziri ambaye ameshiriki ufisadi mzito wa mabehewa na bandari akiwa waziri wa uchukuzi??

Imekuwaje asimamishwe kazi katibu mkuu uchukuzi kwa tuhuma za kushindwa usimamizi ilhali aliyekuwa kiongozi wa sera Mwakyembe anarudishwa kwenye uwaziri??


Taratibu wanafiki wataanza kuelea juu ya maji kama mafuta coz Magufuli ameanza kuwaumbua....
Kwenu ninyi ni mpaka fisadi asafishwe na Mungu MTU Mbowe akisafishwa na mwingine haiswihi!!
 
Muwe mnajiongeza kidogo. Wananchi wamewachagua hao hao wenye ufisadi. Kulingana na katiba lazima mawaziri wawe wabunge. Wakuteua ni 10 tu sasa atachagua nani. So tumpe muda awasimamie
 
Kwanza Prof Muhongo kwenye mgao alipata shilingi ngapi? Mbona kwenye mgao aonekaniki jamani? Tuwaachie wafanye kazi tu
 
kiweledi, Magufuli hapaswi hata kutamka jina Muhongo sidhani kama Ndugu yetu Mpendwa Mungu amlaze Pema Deo Filikunjombe leo angenyamaza kuona huyu ndg yuko kwny baraza hili la awamu ya 5.Asingenyamazaa kiukweliii.
Sasa asingenyamaza ndo nini kingetokea?
 
Tuondolee ujinga wako nyie watoto wa mafisadi mwaka huu mtapata shida sana muhongo hakuna wa kumuhonga ndiyo maana mnapata shida.

sasa wizara ya nishati na madini imepata mwenyewe ni mwendo wa kukimbia tu mafisadi ndiyo mwisho kabisa tupa kule kamwambie na Lowasa limeunguruma tayari.

Muhongo nikikumbuka alivyotokwa povu kutetea wezi sina hamu naye
 
Mlikuwa mkimshabikia lowassa na mlitaka awe Rais wa JMT, sasa leo eti mnamtaja Mwakyembe na PROF Muhongo eti JPM amekosea kuwateua,inaonekana mnacheza ngoma msioijua leo hii eti kwenye taifa hili unamuita Prof Muhongo na Mwakyembe wachafu??? kweli watanzania hamna shukrani, sio kila linalotokea lazima likufurahishe na liwafurahishe mabwana zako.. Baraza la JPM Liko sawa tu na ni la wachapa kazi na wazalendo wote tulijua litakuwa hilo, au labda mngefurahi kama kwenye baraza angekuwepo Mdee,mnyika,na lissu?? hapana tuache unafiki tumuunge mkono JPM ameonyesha njia lazima aungwe mkono tuache maigizo!! Tanzania bila majungu na chuki inawezekana tu, tusisababisha wale maadui wa taifa wakaanza kumuhujumu JPM kama alivyokuwa akihujumiwa JK na marafiki zake wa zamani,, kuna watu wameukosa urais na bila shaka waliwekeza sana huko toka 2005 maana walikubaliana kuachiana vijiti wakijua nchi ni ya kwao hapo mmoja akaamua kuwa mzalendo na kujirudi akijua tanzania ni ya watanzania, nafikiri ule uzalendo na nidhamu aliyojifunza jeshini vilimsaidia, chuki imebaki kwa huyu mkuu na kila baya leo hii utasikia mkwere yaani watu kama hawaoni vita ni nini hapa, maslahi, ugonjwa mbaya sana sasa hivi tanzania hapa, chuki imehamia kwa wazalendo wote wanaopambana taifa lisiuzwe na kwenda kwa watu fulani hivi na hii chuki imehamishiwa kwa wananchi wanaoicheza ngoma wasioijua... Its the matter of time and time will tell, lets be patience, We will cross.
 
kwani magufuli hakuwahi kuwa na kashfa? mbona wanainchi wamemchagua hivo hivo kuwa rais pamoja na kashfa zake?????

we ni jipu subir kutumbuliwa tu. maana hamna namna tena.
Mwinyi alikuwa na kashfa na kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani. Mwisho alikuwa Rais wetu. Sioni la Mhongo kama ni issue maana kwa ESCROW Boss ndiye alitakiwa kuachia ngazi ila Ukimgusa nchi inasambaratika. Hivyo tumwache afanye kazi.
 
Wizara ambazo Rais amezikuta taabani kwa ufisadi hasa za uchukuzi na nishati na madini mawaziri watatu waliokuwepo wamerudishwa kuwa mawaziri. Tz haina watu wengine? au mheshimiwa Rais amejiridhisha kwa vigezo gani? ngoja tuone pengine chini yake watakuwa malaika kwa vigezo vyake.
 
Mi nilijua Ile sinema ya push-ups ndo ilikua kali kuliko zote kumbee...ndo kwanza staring anaanza kuonyesha kipaji chake ana vipande zaidi ya 100!

Eti juzi bale anakamatwa kama mujujumu uchumi jana Mwakyembe anakua waziri! Daaa nitaishi Tz ili mradi tu nione hiki kizazi je aliyetuloga atatuhurumia aturudishie vichwa vyetu? Maana nimegundua kumbe watanzania wengi tunatembea na viwiliwili kama misukule huku vichwa vikiwa vyeupeee....

Yaani mambo ni vululuvululu, juzi tukaamshwa asubuhi asubuhi na mafagio kufanya usafi kumbe vifaa vya kuzolea taka hakuna..hahahahahaha acha nicheke kidogo maana hii ni involuntary action nimeshindwa kujizuia!

Kwanza kikubwa ninachokiona kwenye hii sinema ni kwamba, katika episode ya pili utawala wa sheria ndo bye bye kila mwenye panga atakua anashusha tu litakapotua ndo hapohapo...I don't care kwani watanifanyaje?

Sasa hivi tayari migogoro Kati ya wakulima na wafugaji imepamba moto nani awaokoe? Migogoro kati ya wananchi na wawekezaji nayo imo si mimi ni TV zinaonyesha..hizo bomoabomoa sasa!

Yaani ninachokipenda ni kwamba kwenye hii sinema kila mmoja ni muhusika mkuu, uwe mpinzani au kwenye mfumo..kinachonisikitisha tu ni kwamba, wale wakuuza nyumba za serikali kiholela hawahusiki na wale wa kutuletea mabehewa ya mwaka 78!!.. Hapa kidogo move imeniboa tena
 
muhongo ameteuliwa kuwafurahisha wafanya biashara wa ndani, chini ya magufuli atakula matapishi yake, lazima vitalu wapewe wazawa, na hapo atajisikia vibaya sana ila han jinsi, serikali ya udalali imekwenda mapumziko.
 
Aheri kuwa masikini mfukoni kuliko kuwa masikini kichwani. Ni muda mfupi tu tushasahau tulipotoka na tumebaki kushabikia ujinga. Mijitu inakashfa za wazi kabisa leo tunawaona wengine kwenye Wizara ile ile.

Je, kuna umakini hapa?
 
kwahiyo kingereza ndo uthibitisho wa kiwango chako cha elimu? wewe Lowassa ndo kipimo chako kuwa hakuna mchafu zaidi yake? hiyo chuki unayoizungumzia ni tofauti na hii yako kwa Lowassa? kama unawaona wasafi usiwalinganishe toa facts za usafi wao. huko bandalini tangu rais aingie madarakani umesikia madudu aliyoyavumbua? nani alikuwa waziri huko? na kule TANESCO umesikia na ufunguliaji wa maji ya bwawa la mtera? nani alikuwa waziri huko? unyanyasaji wa wazi juu ya wazawa kuwekeza kwenye vitalu vya gesi aliouzungumza rais siku alipokutana na wafanyabiashara ulifanywa na nani? Tuishie kusema kuwa labda rais amewasainisha mkataba wa utekelezaji kutokana na uhitaji wa uzoefu wao hao wateule waliorudia kuwa mawaziri.
 
Back
Top Bottom