Kwa ongezeko hili la kodi kwenye Mafuta ya Petroli na Dizeli tutarajie maisha ya wanyonge kuwa magumu sana

Wanyonge hawapaswi kuchangia. Duniani kote kodi hulipwa na matajiri. Masikini aka wanyonge hawalipi kodi. Maana ya kodi ni matajili kuchangia ustawi na huduma za wanyonge. Wanyonge michango yao ni nguvu yao (labour) wenyewe.
Wewe kama tajiri mbona hujajitokeza hasharani kulipia wanyonge kadhaa?
 
Bado kuna shida kubwa sana kwenye ukusanyaji wa kodi itokanayo na mafuta. Bado serikali inapoteza zaidi ya asilimia 70 ya VAT ambayo mnunuzi wa mafuta kwenye pampu anamlipa muuzaji. Matokeo yake ni serikali kuona kodi ndogo ikikusanyaa kutoka VAT na wakaamua kuongeza tozo zaidi. Itafikia mahala iwe sheria anayemiliki chombo cha moto anunue mafuta kwa kutumia kadi na sio cash! Au mwingizaji wa mafuta nchini alipe hiyo VAT kabla hajauza kwa wasambazaji na wauzaji vituoni.

Biashara ya mafuta haijadhibitiwa kabisa! Na ni muhimu sana kwa uchumi kwa sababu ina athari kwa KILA bidhaa na huduma!!!
Hili wanashindwa nini kufanya au kwa vile wafanyabiashara wa mafuta ndio hao hao wabunge?
 
Kwa ongezeko hilo la kodi la Tsh. 100 kwa kila lita moja ya Mafuta ya Petroli na Dizeli tutarajia maisha hasa ya wanyonge yatakuwa magumu sana. Waziri mwenyewe wa fedha analitambua hilo na ndiyo maana kawaambia watanzania kuwa itabidi wafunge mikanda, mambo ya kula bata wasahau. Ongezeko la kodi hii itasababisha yafuatayo:

1. Nauli ya daladala na bodaboda itapanda. Hivyo hata hilo punguzo la PAYE la 1% kwa watumishi wa serikali litamezwa na hilo ongezeko la nauli ya daladala. Kwa mama ntilie na wajasiliamali wadogo itabidi waongeze bei ya bidhaa zao kufidia ongezeko la nauli za daladala na bodaboda.

2. Nauli ya mabasi na malori kusafirisha abiria na bidhaa itapanda. Hivyo bidhaa zote zitapanda bei kufidia gharama za kuzisafirisha. Ndege huwa zinatumia mafuta ya taa. Kwa kuwa mafuta haya ya taa nayo yamepandishwa kodi, basi tutarajie nauli za ndege nazo zitapanda.

3. Mashine nyingi za viwanda vya kuzalisha bidhaa mbali mbali hutumia mafuta haya au umeme. Hivyo ongezeko la bei kwenye baadhi ya bidhaa haliepukiki kwani hata bei ya umeme nayo itapanda kwani kodi ya majengo itatozwa kwenye umeme ie kwenye bill ya umeme kutakuwa na VAT, Ewura na Building!

4. Na kadhalika. Yaani multiplier effect ya ongezeko la bei ya nishati kama ya Mafuta ya Petroli, Dizeli na Umeme huwa ni kubwa sana na kuwahusu wananchi wote. Hiyo a bei ya mitandao kama data, miamala nk inawahusu wananchi wachache sana wenye uwezo na ni ya hiari. Mtu wa kawaida data za mb hazimuhusu kwani haziliwi.

5. Ongezeko la kodi ya mafuta ya petroli na dizeli litasababisha mfumuko wa bei na kuteremka kwa thamani ya pesa yetu. Hii itasababisha hata bidhaa zinazotoka nje ya nchi (imports) nazo kupanda. Pato la mtanzania na taifa kwa ujumla litapungua na si ajabu tukajikuta tunaondolewa kwenye orodha ya nchi za uchumi wa kati wa chini (low middle income countries). Zanzibar wako makini, wao hawakupandisha bei za nishati hii. Si ajabu nishati hii ikawa inaingizwa kwa magendo kupitia Zanzibar.

uliposema ndege inatumia mafuta ya taa nikajua mtoa mada hamna kitu hujui chochote
 
uliposema ndege inatumia mafuta ya taa nikajua mtoa mada hamna kitu hujui chochote
Waziri wa elimu, Prof. Ndalichako njoo huku uone tulivyoua elimu kwa vijana wetu. Enzi zetu somo la chemistry lilikuwa compulsory kwa wanafunzi wote hadi kidato cha nne. Ni vyema sasa tukarudi kwenye utaratibu huo.

Nitajaribu kukuelimisha: Kerosine (also spelled kerosene in some countries such as USA) is also called paraffin or paraffin oil. It was first discovered by a Canadian physician named Abraham Gesner in the late 1840s. It is a flammable hydrocarbon liquid with a chemical formula ranging C12H26 to C15H32. It is obtained from petroleum (crude oil) and is used as fuel for burning kerosine lamps, domestic cookers or heaters or furnaces as well as fuel for jet engines and others.
 
No Creativity, ni nwanatafuta kodi kwenye vyanzo vile vile badala ya kuongeza vyanzo vipya..

Wanafeli sana
 
Kwa ongezeko hilo la kodi la Tsh. 100 kwa kila lita moja ya Mafuta ya Petroli na Dizeli tutarajia maisha hasa ya wanyonge yatakuwa magumu sana. Waziri mwenyewe wa fedha analitambua hilo na ndiyo maana kawaambia watanzania kuwa itabidi wafunge mikanda, mambo ya kula bata wasahau. Ongezeko la kodi hii itasababisha yafuatayo:

1. Nauli ya daladala na bodaboda itapanda. Hivyo hata hilo punguzo la PAYE la 1% kwa watumishi wa serikali litamezwa na hilo ongezeko la nauli ya daladala. Kwa mama ntilie na wajasiliamali wadogo itabidi waongeze bei ya bidhaa zao kufidia ongezeko la nauli za daladala na bodaboda.

2. Nauli ya mabasi na malori kusafirisha abiria na bidhaa itapanda. Hivyo bidhaa zote zitapanda bei kufidia gharama za kuzisafirisha. Ndege huwa zinatumia mafuta ya taa. Kwa kuwa mafuta haya ya taa nayo yamepandishwa kodi, basi tutarajie nauli za ndege nazo zitapanda.

3. Mashine nyingi za viwanda vya kuzalisha bidhaa mbali mbali hutumia mafuta haya au umeme. Hivyo ongezeko la bei kwenye baadhi ya bidhaa haliepukiki kwani hata bei ya umeme nayo itapanda kwani kodi ya majengo itatozwa kwenye umeme ie kwenye bill ya umeme kutakuwa na VAT, Ewura na Building!

4. Na kadhalika. Yaani multiplier effect ya ongezeko la bei ya nishati kama ya Mafuta ya Petroli, Dizeli na Umeme huwa ni kubwa sana na kuwahusu wananchi wote. Hiyo a bei ya mitandao kama data, miamala nk inawahusu wananchi wachache sana wenye uwezo na ni ya hiari. Mtu wa kawaida data za mb hazimuhusu kwani haziliwi.

5. Ongezeko la kodi ya mafuta ya petroli na dizeli litasababisha mfumuko wa bei na kuteremka kwa thamani ya pesa yetu. Hii itasababisha hata bidhaa zinazotoka nje ya nchi (imports) nazo kupanda. Pato la mtanzania na taifa kwa ujumla litapungua na si ajabu tukajikuta tunaondolewa kwenye orodha ya nchi za uchumi wa kati wa chini (low middle income countries). Zanzibar wako makini, wao hawakupandisha bei za nishati hii. Si ajabu nishati hii ikawa inaingizwa kwa magendo kupitia Zanzibar.

Acha kulalamika, acha tujenge uchumi wa nchi yetu.
 
Acha kulalamika, acha tujenge uchumi wa nchi yetu.
Una uhakika hizo shillingi billion 300 zitakazotokana na kodi hiyo ya ongezeko kwa mafuta hayo itajenga nchi yetu? Kwanza pesa hiyo ni ndogo sana ila madhara yake kwenye uchumi wa nchi yetu yanaweza kuwa makubwa sana (disrupptive) kwa sababu ya negative multiplier effects zake nilizozitaja hapo juu. Hela hiyo inaweza kuishia kulipana honoraria na posho za vikao kwa watumishi wa serikali vya kupanga na kudadavua masuala yasiyo na tija kwa nchi yetu. Pesa hiyo ingaliweza kupatikana kwa njia zingine zisizo na madhara kwa jamii hususani kuwabana zaidi wafanyabiashara wakubwa na wale mafisadi wakubwa kama walivyokuwa wamebanwa hapo awali,
 
Mimi siyo mtaalamu wa uchumi, lakin kwa akili ya kujumlisha moja ongeza moja, naamini kabisa ukugusa mafuta unasababisha multiplying effect ya kila kitu. Vyakula, maji, nauli nk vitapanda bei:rolleyes:. Anyway, yote maisha!
 
Back
Top Bottom