Kwa ongezeko hili la kodi kwenye Mafuta ya Petroli na Dizeli tutarajie maisha ya wanyonge kuwa magumu sana

Kwako ni ndogo lakini kwangu kubwa, nakatwa Kodi kwenye mshahara, VAT Kodi za majengo na biashara, bado na mafuta pia wakati hao wabunge wengine wamelala tu bungeni, hawakatwi chochote
Nani ambae hakatwi hizo kodi? Ulitaka huduma zinazotakiwa kutolewa na ujenzi wa miundombinu nani alipie? au serikali itoe wapi pesa? kuna mjomba au baba wa kugharamia hizo huduma na miradi amabayo wewe na mimi tutakuwa wanufaika?
 
Nani amabe hakatwi hizo kodi? Ulitaka huduma zinazotakiwa kutolewa na ujenzi wa miundombinu nani alipie? au serikali itoe wapi pesa? kuna mjomba au baba wa kugharamia hizo huduma na miradi amabayo wewe na mimi tutakuwa wanufaika?
Just compare dogo unazokatwa na hayo mambo unayoyasifia yanalingana?
 
Ndiyo; kama ulikuwa hujui huo ndio ukweli wenyewe. Hiyo inayoitwa jet fule, na paradffil au kerose ambayo kwa kiswahili ni mafuta ya taa.
Nilikua najua hiyo paraffin, kerosene ndio nimejua hapa nayo sio hiyo nnayojua ya kuwasha taa...
 
Sisi ni wananchi ambao pato letu halifiki elf 20 kwa siku.
Hata sisi ni wananchi ambao pato letu ni zaidi ya elfu 200 kwa siku ila tuko wachache ukilinganisha na nyie wa pato lisilofika elfu 20 kwa siku.
 
Hata sisi ni wananchi ambao pato letu ni zaidi ya elfu 200 kwa siku ila tuko wachache ukilinganisha na nyie wa pato lisilofika elfu 20 kwa siku.
Hivyo sisi wote ni wananchi na sio "wanyonge" mnyonge alishadanja....
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Hivyo sisi wote ni wananchi na sio "wanyonge" mnyonge alishadanja....
Mnyonge ni neno la kiswahili linalomaanisha mwananchi mwenye kipato cha chini. Ni unyonge wa kipato tu, kwenye masuala mengine anaweza kuwa ngangari kinoma kumpita hata huyo mwenye kipato kikubwa. Wote wanategemeana. Hakuwezi kuwa na matajiri wa kipato kama hakuna masikini wa kipato.
 
TANGU TANZANIA IUMBWE TUME KUWA NA MAWAZIRI WA FEDHA VICHWA KAMA EDWIN MTEI, AMIR JAMAL, STEVEN KIBONA, CLEOPA MSUYA SIJAWAHI KUONA HATA MMOJA WA HIVI VICHWA AKIPUNGUZA KODI YA BEER NA KUONGEZA KODI YA MAFUTA. MAAJABU HAYA NIMEKUJA KUYAONA JANA KWA HUYU CHA AJABU ZAIDI WABUNGE WALIOPO WATAIPITISHA HII BAJETI KAMA ALIVYOAHIDI NDUGU YAI.
KILA MTU ANAJUA KWAMBA UKIONGEZA BEI YA MAFUTA BEI YA KILA KITU KINGINE LAZIMA IPANDE KWA NCHI INAYOYEGEMEA MAFUTA KWA UZALISHAJI MALI.
WHERE ARE WE GOING.
UNASHUSHA BEI YA BEER NA KUONGEZA BEI YA DAWA, MAZIWA, UMEME.
Kuna umuhimu hii wizara apewe mtoto wa mjini hususan Dar au Ariusha maana ukizaliwa Dar tayari Ni form six na ukizaliwa Arusha tayari Ni fomfoo.
Mtu ana degree ya uchumi hajui hata concept ya multiplier effect?
 
Just compare dogo unazokatwa na hayo mambo unayoyasifia yanalingana?
Kama mafuta yameguswa lazima kila kitu kitapanda,sijui kwa ni nviongizi Wengi hasa kutoka zanzibar wanapenda sana kucheza na mafuta kuna yule mwingien sijui saada mukya Naye kodi zake zilikuwa za mafuta mafuta
 
Hivi Ni Kweli tumeshindwa Kabisa Kubuni Sehemu zingine za Malipo ya kodi zaidi ya kusukuma Mikodi Mikubwa Mikubwa Kila Budget kwenda kwenye mafuta???

Mama Samia Angalia hili Ni Hujuma kwanza tayari bei ziko juu Mnoo..Mkiongeza na hii inaenda kuumiza zaidi watu...Tafadhali Mama Kataa Hii Nyongeza ya kodi kwenye Mafuta....
 
Yaani natural resources zipo lakini mzigo anabebeshwa mwananchi kila kitu. Badilini basi natural resources mziweka kwenye pesa. Ni lini mtaweza kufanya hivyo kupunguza mzigo kwa raia? Sasa hivi ndo vyuma vitakaza mpaka basi
 
Hili wanashindwa nini kufanya au kwa vile wafanyabiashara wa mafuta ndio hao hao wabunge?

Swali laki ni sahihi kabisa. Sheria zote za kodi nchi hii ni rafiki katika maeneo wakubwa na wabunge wako! Usafirishaji, mafuta, mahoteli na tenda za serikali! Maeneo ambayo udhibiti ni hafidu au hakuna!

Kama waingizaji wa mafuta hawajalipa hii VAT kabla hawajauza - kodi hiyo inakwepwa kwenye pump! Moja ya vitu mataifa yaliyoendelea yamefanya, ni kuthibiti mianya ya kukwepa kodi. Sisi tunashindwa vyote, kudhibiti makusanyo na hata matumiz!!
 
Kipato cha chini (less than 3 lakis per month) hakikatwi kodi kwa mujibu wa sheria. Kinachozidi hapo hadi 6 lakis pm kinakatwa hiyo 8% PAYE. Kipato/mshahara unaozidi 6 lakis pm unakatwa 30% PAYE. Mimi mshahara wangu ni 10m per month ninakatwa sh 3.3 million per month kama PAYE. Hiyo inayotangazwa kwamba serikali imepungunguza PAYE kwa wafanyakazi kutoka 9% hadi 8% ni kwa wafanyakazi wa chini ambao mishahara yao haizidi laki 6 kwa mwezi aka wanyonge. Ila serikali kwa makusudi huwa haitoi ufafanuzi huo.

Sisi tunaolipa kodi kubwa, hizo zahanati na health facility zote za serikali hazituhusu, tunatibiwa kwenye hospitali za juu zilizo ndani au nje ya nchi yetu kwa kujilipia wenyewe. Hizo hospitali za serikali tunazozichangia kupitia kodi ni kwa ajili yenu wenye vipato vidogo - wanyonge. Hiyo ndiyo dhana ya kodi.
Watu wana salary ya laki 7 hawataki kuitwa wanyonge. Wakati wengine payee tu ni zaidi ya hiyo laki 7. Hizi kodi za awamu hii ni mzigo mkubwa kwa wenye kipato cha chini..
 
Wewe kama tajiri mbona hujajitokeza hasharani kulipia wanyonge kadhaa?
Ninakatwa kodi ya PAYE ya sh 3.5 million kila mwezi na TRA kutoka kwenye mshahara wangu kila mwezi kwa mjibu wa sheria. Pesa hizo serikali inapaswa kuzipeleka kuboresha maisha ya wanyonge hususani kupata maji safi na salama, kutoa elimu bora kwa watoto wao, huduma ya afya, barabara bora na kadhalika. Hapo hakuna hiari, ni sheria : sasa nitajitangaza kwa lipi?
 
Mnyonge ni neno la kiswahili linalomaanisha mwananchi mwenye kipato cha chini. Ni unyonge wa kipato tu, kwenye masuala mengine anaweza kuwa ngangari kinoma kumpita hata huyo mwenye kipato kikubwa. Wote wanategemeana. Hakuwezi kuwa na matajiri wa kipato kama hakuna masikini wa kipato.
Ni jina baya....
 
Kwa ongezeko hilo la kodi la Tsh. 100 kwa kila lita moja ya Mafuta ya Petroli na Dizeli tutarajia maisha hasa ya wanyonge yatakuwa magumu sana. Waziri mwenyewe wa fedha analitambua hilo na ndiyo maana kawaambia watanzania kuwa itabidi wafunge mikanda, mambo ya kula bata wasahau. Ongezeko la kodi hii itasababisha yafuatayo:

1. Nauli ya daladala na bodaboda itapanda. Hivyo hata hilo punguzo la PAYE la 1% kwa watumishi wa serikali litamezwa na hilo ongezeko la nauli ya daladala. Kwa mama ntilie na wajasiliamali wadogo itabidi waongeze bei ya bidhaa zao kufidia ongezeko la nauli za daladala na bodaboda.

2. Nauli ya mabasi na malori kusafirisha abiria na bidhaa itapanda. Hivyo bidhaa zote zitapanda bei kufidia gharama za kuzisafirisha. Ndege huwa zinatumia mafuta ya taa. Kwa kuwa mafuta haya ya taa nayo yamepandishwa kodi, basi tutarajie nauli za ndege nazo zitapanda.

3. Mashine nyingi za viwanda vya kuzalisha bidhaa mbali mbali hutumia mafuta haya au umeme. Hivyo ongezeko la bei kwenye baadhi ya bidhaa haliepukiki kwani hata bei ya umeme nayo itapanda kwani kodi ya majengo itatozwa kwenye umeme ie kwenye bill ya umeme kutakuwa na VAT, Ewura na Building!

4. Na kadhalika. Yaani multiplier effect ya ongezeko la bei ya nishati kama ya Mafuta ya Petroli, Dizeli na Umeme huwa ni kubwa sana na kuwahusu wananchi wote. Hiyo a bei ya mitandao kama data, miamala nk inawahusu wananchi wachache sana wenye uwezo na ni ya hiari. Mtu wa kawaida data za mb hazimuhusu kwani haziliwi.

5. Ongezeko la kodi ya mafuta ya petroli na dizeli litasababisha mfumuko wa bei na kuteremka kwa thamani ya pesa yetu. Hii itasababisha hata bidhaa zinazotoka nje ya nchi (imports) nazo kupanda. Pato la mtanzania na taifa kwa ujumla litapungua na si ajabu tukajikuta tunaondolewa kwenye orodha ya nchi za uchumi wa kati wa chini (low middle income countries). Zanzibar wako makini, wao hawakupandisha bei za nishati hii. Si ajabu nishati hii ikawa inaingizwa kwa magendo kupitia Zanzibar.


Uko sahihi, kila bidhaa inasafirshwa. Na hivyo bei ya mafuta ikipanda, anayeumia ni mlaji wa mwisho. Hapa kuna utata mkubwa sana. Bei za bidhaa zote huwa zinapanda kwasababu ya gharama za usafirishaji.
 
Wanyonge hawapaswi kuchangia. Duniani kote kodi hulipwa na matajiri. Masikini aka wanyonge hawalipi kodi. Maana ya kodi ni matajili kuchangia ustawi na huduma za wanyonge. Wanyonge michango yao ni nguvu yao (labour) wenyewe.
US matajiri walikuwa hawalipi kodi, sahi kunaundwa sheria waanze kutozwa. Tena nyingi kuliko raia wa maisha ya wastani na chini. Na ndivyo inavyopaswa kila pahali, sio kufinyiliana.
 
Ili nchi kuendelea achana propaganda za mwendazake ....rufanye kazi bidiii tuzalushe na tulupe kodi.....acha peyeol mafuta etc...tuchape kazi bla bla za donor country ni upuuzi uze tufanye kaxi lipa kodii
 
Inakuwaje hii nchi inajiendesha kwa kodi zinazozidisha mzigo kwa wanyonge ili hali tuna rasilimali nyingi za madini ya dhahabu, almasi, tanzanite, gesi asilia including gesi ya helium, bandari ambazo zinapokea mizigo ya land-locked countries tunazopakana nazo nk. nk. Kushindwa kutumia gesi yetu kama nishati ya kupikia majumbani na kuendesha magari ya abiria, mizigo, treni, na yale ya watu binafsi kunazidisha mzigo wa kuagiza mafuta toka nje ambayo yanatozwa kodi na kuyafanya yawe juu sana.......huyo waziri ni lini atabuni mapato mengine nje ya kodi za mafuta ambayo yanamwongezea mnyonge ugumu wa maisha? au ni kukaa tu hapo kucheza mdundiko.....
 
Back
Top Bottom