Kwa nini Yesu haku kataza kuoa wake wengi?

Hassanjk

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2023
Posts
550
Reaction score
1,019
Nimekuwa najiuliza hilo swali kwa sababu zifuatazo;

vizazi vilivyo kuwepo kabla ya Yesu na hata Yesu akiwepo, walikuwa wanaoa wake wengi na Yesu hakuwahi kukemea au kusema kuna ubaya wowote.

Sheria ya kuwa taka Wakristo waoe mke mmoja ilitungwa na Papa Paul baada ya Yesu kuwa alisha nyakuliwa
Sasa najiuliza;
1. Kama kuoa wake wengi haimpendezi Mungu, kwa nini Yesu hakulikemea

2. Dunia tangu zamani wanawake ni wengi kuliko wanaume; Papa Paul alipopitisha hii sheria alikusudia hao wanawake wengine waolewe na nani?

3. Dunia inapita kipindi kigumu ambapo single mothers imekuwa kama fasheni, watoto wa mitaani wamejaa mijini, na hata magonjwa ya ngono yameongezeka nk ambapo ukifikiria vizuri unaweza kuona kuwa uwepo wa wanawake wengi wasio kuwa na wanaume inaweza kuchangia.
Mfano: Ukienda mji kama Mombasa ambapo Wakristo sio wengi, watoto wamitaani na single mother ni wa kutafuta ILA ukienda miji kama Kisumu, Nairobi nk ambapo wakristo ndio wengi, watoto wa mitaani na single mother ni kwa mamia

4. Nafikiri tunahitaji Papa mwingine aangalie vizuri hii sheria kwani inawezekana Papa Paul hakuwa amefikiria vizuri kwa kuangalia miaka mingi ijayo.
 
3. Dunia inapita kipindi kigumu ambapo single mothers, watoto wa mitaani nk ambapo ukifikiria vizuri unaweza kuona kuwa uwepo wa wanawake wengi wasio kuwa na wanaume inaweza kuchangia.

Yaani huyo papa kawaachia mzigo mzito wakristo ambao mpk leo unawatesa.
Kuoa mke mmoja alaf sheria inasema hakuna kuachana 😃
 
Mbona waislam wengi Sana wameoa mke mmoja,...Jaribu kutafiti utajua kuoa wake wengi Kwa waislam imebaki kwenye vitabu tu...Mimi naishi mtaa wenye waislam wengi Sana na Wewe tafiti...Kuoa mke mmoja ni kitu çommon Sana hata ukiacha dini.
 
Aliyeruhusiwa kuoa wake mpaka wanne huku ana utashi wa kuongeza vimada hata wafike kumi yupo Jamiiforums usiku huu wa sasa 00:55 analalamika Yesu inakuwaje hakukataza kuoa mke zaidi ya mmoja lakini watu hawaoi hivyo?

Sasa hao wake zako wanne ulioruhusiwa kuwaoa unawalomba saa ngapi?maana ilitegemewa mida hii huko uliko iwe show show kila siku wewe ni kusukuma mti tu ila umepata hadi wasaa wa kuwatetea wasiokuwa wenzako ina maana hilo hata huko uliporuhusiwa hakuna uhalisia huo,maisha ni zaidi ya kumiliki wanawake mlima.
 
Nimekuwa najiuliza hilo swali kwa sababu zifuatazo;

vizazi vilivyo kuwepo kabla ya Yesu na hata Yesu akiwepo, walikuwa wanaoa wake wengi na Yesu hakuwahi kukemea au kusema kuna ubaya wowote.

Sheria ya kuwa taka Wakristo waoe mke mmoja ilitungwa na Papa Paul baada ya Yesu kuwa alisha nyakuliwa
Sasa najiuliza;
1. Kama kuoa wake wengi haimpendezi Mungu, kwa nini Yesu hakulikemea

2. Dunia tangu zamani wanawake ni wengi kuliko wanaume; Papa Paul alipopitisha hii sheria alikusudia hao wanawake wengine waolewe na nani?

3. Dunia inapita kipindi kigumu ambapo single mothers, watoto wa mitaani nk ambapo ukifikiria vizuri unaweza kuona kuwa uwepo wa wanawake wengi wasio kuwa na wanaume inaweza kuchangia.

4. Nafikiri tunahitaji Papa mwingine aangalie vizuri hii sheria kwani inawezekana Papa Paul hakuwa amefikiria vizuri kwa kuangalia miaka mingi ijayo.
Aisee kasome Tena biblia
Soma Mathayo 19:8- na kuendelea utaelewa
 
Inaonekana ujawahi kuisoma biblia na kufuatilia habari kuoa,
 
Kuoa wake wengi ni Ukatiri na ni kitendo cha kukosa ustarabu. Lakini wanatwambia Mwanaume kumlala mwanaume mwenzake ni Kuwa Open Minded.....wasifiana kabisa, eti he has or she has open mind.....ni ustarabu.

Nilipogundua hii janja janja nikaongeza na mke wa pili.

Dini ni Utapeli
 
Mbona waislam wengi Sana wameoa mke mmoja,...Jaribu kutafiti utajua kuoa wake wengi Kwa waislam imebaki kwenye vitabu tu...Mimi naishi mtaa wenye waislam wengi Sana na Wewe tafiti...Kuoa mke mmoja ni kitu çommon Sana hata ukiacha dini.
Muislamu haswaa akiwa na uwezo ata kwa siku moja tu anakamilisha ndoa 4
 
B
Inaonekana ujawahi kuisoma biblia na kufuatilia habari kuoa,
Nimesoma Biblia kwa takriban 85% nikiwa shuleni/chuoni na nikiweka vifungu vinavyo kinzana ndani ya Biblia ambapo kitu kimoja kimeongelewa tofauti kabisa na mwanafunzi mwengine utashangaa....
Pengine nimalizie 15% iliyobakia
 
Aisee kasome Tena biblia
Soma Mathayo 19:8- na kuendelea utaelewa
Ndio maana wanakuja kwanza na hoja mfu za kuonesha baadhi ya maandiko ya Biblia ni feki ili watakapo-introduce mada kama hizo wakuambie; look, Injili ya Mathayo Ina kasoro nyingi!

Anti-Christ Covax ameipinga sana Injili ya Mathayo kwa ajenda za siri kama hizo. Nyaraka za Paulo zimepingwa sana kwa ajenda za siri kama hizo pia - maandalizi ya ushetani ujao.

Thanks kwa watumishi wa Yesu wasio na faida hamis77 na Setfree wamejitahidi sana kuilinda imani dhidi ya wafuasi wa shetani humu!
 
Wanaisoma biblia kimsikitimsikiti,uzuri kwa sasa hakuna mwenye akili timamu anayesoma biblia ataiacha awe muislamu dini ya juzi juzi
 
Ndio maana wanakuja kwanza na hoja mfu za kuonesha baadhi ya maandiko ya Biblia ni feki ili watakapo-introduce mada kama hizo wakuambie; look, Injili ya Mathayo Ina kasoro nyingi!

Anti-Christ Covax ameipinga sana Injili ya Mathayo kwa ajenda za siri kama hizo. Nyaraka za Paulo zimepingwa sana kwa ajenda za siri kama hizo pia - maandalizi ya ushetani ujao.

Thanks kwa watumishi wa Yesu wasio na faida hamis77 na Setfree wamejitahidi sana kuilinda imani dhidi ya wafuasi wa shetani humu!
Mkuu acha propaganda zisio kua na mashiko kuhamasisha wanna jf wajua ukweli wewe unaona ni kua ant Christo kweli, Bibulia Ina kinzana sana na sio ufunuo wa roho mtakatifu kama wanavo sema.
 
Aisee kasome Tena biblia
Soma Mathayo 19:8- na kuendelea utaelewa

Nilisoma Biblia Vizuri; nakumbuka kwenye hiyo Mathayo 19 kuna msingi mkuu sana wa ukristo (Amri kumi zilitajwa hapo) Laiti Wakristo wangezifuata hata robo tatu yake Dunia ingekuwa mahala pazuri sana ni kwa bahani mbaya waamini wamekengeuka
kuhusu kuoa; Yesu aliongelea TALAKA, hakuongelea idadi ya wake...
 
Hoja ni kuwa Je Yesu alikataza kuoa Mke zaid ya mmoja?.

Hapa Yesu anaongea.
Mathayo 19:4-5
"Yeye aliyewaumba hao kutoka mwanzo aliwafanya mwanamume na mwanamke na kusema, ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”

Hivyo Yesu alikataza.

Pamoja na dhima ya kujaza dunia Mungu hakumuumbia Adamu wanawake kadhaa, jambo ambalo lingesaidia katika kutimiza amri ya kuijaza dunia.
Bali Mwanamke mmoja.

1 Wakoritho 7:2.
"Kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.”
 
Kwa hiyo hao wanawake takribani milioni 20 duniani, wataishi maisha yao yote bila kuolewa au Mungu alikosea kuwaumba wawe wengi?
 
Idadi ya wanawake ni weng zaid duniani . Kwasababu nying na Risk ambayo inafanya wanaume wafe mapema.

Ila Mungu ameumba kila mwanamke na mwanaume wake.

Pia wanawake wakishafika age fulan hawaon tena haja ya kuolewa. Ndivyo walivyoumbwa.
Ndio maana mjane wa miaka 60 kwa mwanaume unaweza kuoa wakat mjane wa miaka 60 mwanamke hataman kuolewa tena.
 
Ukitaka kurejea Biologia ni vizuri uwe na elimu ya kutosha, sio kuandika tu kama hadithi....
Sijui kama ulisoma Biologia walau ya kidato cha nne, kwani ungeweza kujua uumbaji na possibility ya kupata mtoto wa Kike ni kubwa kuliko kupata mtoto wa Kiume...

Kusema wanawake wakifikisha Miaka 60 hawana haja ya mwanamme, sijui kama unamaanisha nini?
Au unamaanisha wanawake wakae bila mwanaume kwa miaka takribani 40 (kutoka miaka 20 hadi 60);
akili za wapi hizi? kwa miaka hiyo Arobaini unajua wanafanya nini?

Umeshasema kuna wanaume wanakufa mapema, bila kusahau wengine wanazaliwa Impotence nk inamaana waoaji wanazidi kupungua
 
Nimekuwa najiuliza hilo swali kwa sababu zifuatazo;

vizazi vilivyo kuwepo kabla ya Yesu na hata Yesu akiwepo, walikuwa wanaoa wake wengi na Yesu hakuwahi kukemea au kusema kuna ubaya wowote.

Sheria ya kuwa taka Wakristo waoe mke mmoja ilitungwa na Papa Paul baada ya Yesu kuwa alisha nyakuliwa
Sasa najiuliza;
1. Kama kuoa wake wengi haimpendezi Mungu, kwa nini Yesu hakulikemea

2. Dunia tangu zamani wanawake ni wengi kuliko wanaume; Papa Paul alipopitisha hii sheria alikusudia hao wanawake wengine waolewe na nani?

3. Dunia inapita kipindi kigumu ambapo single mothers imekuwa kama fasheni, watoto wa mitaani wamejaa mijini, na hata magonjwa ya ngono yameongezeka nk ambapo ukifikiria vizuri unaweza kuona kuwa uwepo wa wanawake wengi wasio kuwa na wanaume inaweza kuchangia.
Mfano: Ukienda mji kama Mombasa ambapo Wakristo sio wengi, watoto wamitaani na single mother ni wa kutafuta ILA ukienda miji kama Kisumu, Nairobi nk ambapo wakristo ndio wengi, watoto wa mitaani na single mother ni kwa mamia

4. Nafikiri tunahitaji Papa mwingine aangalie vizuri hii sheria kwani inawezekana Papa Paul hakuwa amefikiria vizuri kwa kuangalia miaka mingi ijayo.
Unasema, ambavyo sivyo, kwamba Papa Paulo ndiye alitoa agizo la kuoa mwanamke mmoja tu. Ni Papa Paulo yupi huyo unayemzungumzia? Kama unamaanisha Mtume Paulo aliyekuwa akiwaua Wakristu na baadaye akaja kuongoka akiwa njiani kwenda Damascus kuendeleza kazi hiyo ya kutaka kuliangamiza Kanisa, huyo hakuwahi kuwa Papa. Petro ndiye alikuwa Papa wa kwanza kuanzia Mwaka 33 A.D. mpaka Mwaka 67 A.D. na akafuatiwa na Papa Linus aliyekuwa Papa tangu Mwaka 67 A.D. hadi Mwaka 76 A.D. Hadi leo hii kumekuwa na Mapapa 6 wenye jina la Paulo. Wa kwanza alikuwa Papa kuanzia tarehe 29 Mei 757 hadi tarehe 28 Juni 767. Papa Paulo wa sita na wa mwisho kwa jina hilo alikuwa Papa kuanzia tarehe 21 Juni 1963 hadi tarehe 6 Agosti 1978. Wote hawa hawakutoa agizo hilo. Kwa sasa naishia hapa kwa kuwa huo ndio ulikuwa msingi wa hoja yako ya kuoa mke mmoja..
 
Back
Top Bottom