Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ni akina nani wanaowashawishi au kuwabembeleza wenzao kuoa kati ya wanaume na wanawake? Ni swali rahisi sana kulijibu, kwani karibu kila mtu anajua jibu lake, labda anachoweza kushindwa kukijua ni sababu inayosababisha hali hiyo.
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inavyoongezeka. Wanaume katika karibu jamii zote duniani, wanaonekana kabisa kuwa hawako tayari kuoa kirahisi, ukilinganisha na wanawake.
Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa watu kuhusu jambo hili. Kumekuwa na swali la ni kwa nini vijana wa kiume wamekuwa waongo sana, hasa linapokuja swala la kuoa. Wapenzi wanaambiana kwamba wamependana, na kwamba wataoana, lakini kinachotokea baada ya hapo ni kwa wanaume kupiga chenga kwa visingizio mbalimbali.
Kwa nini hali hiyo hutokea?