Kwa nini wawe wanapiga chenga…………? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wawe wanapiga chenga…………?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 28, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni akina nani wanaowashawishi au kuwabembeleza wenzao kuoa kati ya wanaume na wanawake? Ni swali rahisi sana kulijibu, kwani karibu kila mtu anajua jibu lake, labda anachoweza kushindwa kukijua ni sababu inayosababisha hali hiyo.

  Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inavyoongezeka. Wanaume katika karibu jamii zote duniani, wanaonekana kabisa kuwa hawako tayari kuoa kirahisi, ukilinganisha na wanawake.


  Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa watu kuhusu jambo hili. Kumekuwa na swali la ni kwa nini vijana wa kiume wamekuwa waongo sana, hasa linapokuja swala la kuoa. Wapenzi wanaambiana kwamba wamependana, na kwamba wataoana, lakini kinachotokea baada ya hapo ni kwa wanaume kupiga chenga kwa visingizio mbalimbali.


  Kwa nini hali hiyo hutokea?

   
 2. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwingiliano wa tamaduni yaani kuiga utamaduni wa Magharibi, ni moja ya sababu za vijana wengi kupiga chenga kuoa. Siku hizi ingawa watu wanaoana, lakini uwiano wa wanaooa na wanaopiga chenga umetofautiana sana. vijana wanakwepa majukumu ya ndoa, na wanpenda uhuru, kwa sababu kuna ile dhana kwamba kuoa ni kujinyina uhuru......... huenda maneno hayo yakana na Ukweli, lakini Je ndio watu wasioe au kuolewa?

  Wakati wanaume wanapiga chenga, wanwake nao kwa upande wao kuna baadhi yao hawapendi kusikia hilo neno kuolewa kabisaaa, na sababu ni hiyo hiyo ya usasa.............. Mitanndaop ya Intenet na Simu za mikononi, zimewafanya vijana siku hizi kuwa na ma-partner wa mitandaoni, ambao huwasikliana wakiwa mbali na kama ni kukutana huwa ni mara chache sana, kitu ambacho hakiwanyimi uhuru wao................
  Sababu ziko nyingi lakini nimetaja baadhi tu...............
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  @Tegelezeni.......... Uliyoyasema yana ukweli, lakini hudhani matatizo ya kiuchumi hayana mchango katika hili?
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  One thing ni guarantee....hakuna anaekufa bikira...
   
 5. M

  MyTz JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wadada wanapenda sana kuharakisha michakato ya ndoa...
  huu uharaka ndio unatushtua, tunaanza kuchenga ili tupate mda wa kujiridhisha kama kweli anafaa kuwekwa ndani/mkurupukaji tu...
  ishu ya uchumi nayo inachangia, koz ukioa una establish family ambayo inaongeza majukumu kwa kijana hii nayo inapelekea m2 kuchenga!
   
Loading...