Kwa nini wanawake hawaipendi chadema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wanawake hawaipendi chadema?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Tolowski, May 7, 2011.

 1. T

  Tolowski Senior Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unahudhuria mikutano na maandamano ya chadema utagundua kuwa watu wanaohudhuria wengi wao ni wanaume! Najiuliza ni kwa nini? Hata ukiwahoji wanawake m1 m1 wanasema hawaipendi chadema!nimeshafanya hivyo! Wenzetu amerika vyama vya siasa vinapigania sana kukubalika na wanawake. Lakini mikutano ya ccm wanawake huwa wanakuwa wengi sana!! Hata hao wanaume ambao huwa wanahudhuria mikutano ya chadema huwa ni vijana wadogo mapepe flani hivi!busara zero. Ama kweli rafiki wa muhuni ni wahuni wenzake!! Mungu aliwaumba wanawake na busara ya kimungu! Wanajua kipi chema and kipi uozo.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sio kweli.
  Mimi ni mwanamke na naipenda sana CHADEMA. Yaan iko kwenye damu. Peoplezzzzz!.... Power. Asikwambie mtu bana. Ukombozi uko njiani.
   
 3. T

  Tolowski Senior Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upo peke yako!!wale akina mdee wanataka ubunge tu,mioyoni wanamfeel jeikei
   
 4. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Kaka asante kwa kukutusi....Lakini nashangaa,sasa wewe busara yako iko wapi?Kwani maneno yako yanaonyesha una busara zero na ni muhuni tu...so nakuomba uje uunganie na sisi wenzio.....Ubarikiwe..
   
 5. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />

  Huyo Mungu uliyemtaja ktk thread yako ana amri zifuatazo ambazo unatakiwa uzifuate:
  Usiseme uongo - mkuu tujulishe utafiti wako mpaka ufike kwenye hilo hitimisho hapo juu umeufanya lini, wapi, sample size, nk.

  Anyway, mambo mengine husikumwa na hisia, na watu hutamani kuhalalisha hisia zao.
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  inaonyesha ww ni mwanamke na unaipenda sana cdm.
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hata bibi yangu anaipenda sana CCM, nimewahoji pia baadhi ya wanawake wa uswahilini pia wanaipenda sana CCM. Nilipotaka kujua nikwanini wanaipenda sana CCM bibi yangu alikuwa na haya "Unajua mjuu wangu mimi nakupenda wewe kwasababu unanijali unapokuja kijijini unaniletea sukari, sabuni, mafuta na mavazi hiyo yoote unafanya kwasababu unanijali bibi yako, vivyohivyo hata CCM naipenda sana kwasababu kila wakija hapa kijijini huwa wanatuletea mavazi ona ile Tisheti na kanga zile walitugawia wao lakini wakija hapa chadema kazi yao ni kuzungumza tuu hata hawatupi Tshirt na kanga kama wanavyo fanya CCM" Mwanamke duni wa uswahilini nilipomuuliza kwanini unaipenda CCM? pia alikuwa na haya "Unajua kakaangu mimi nisikufiche sisiemu nawazimia sana unajua hapa mtaani kwetu kila wakija wanatupatia elfu tanotano za bureee kwa kazi ndogo tuu ya kuvaa Tshirt na kofia kisha kuwashangilia na baada ya kumaliza kazi tunajichana miwali, mikuku na bia hebu niambie Chadema wanaweza hayo? wao kazi yao ni kutangaza sera tuu hata wewe kakaangu unafahamu mkono mtupu haulambwi" Lakini kwa upande mwingine wanawake wasomi, vijana ambao tuko nao maofisini wengi wao hawaipendi CCM kwasababu wanafahamu CCM ni nini? na wanahusika vipi na umasikini unalolikumba Taifa lao. Ukitaka kuthibitisha haya kila kwenye mkutano wa CCM lazima utakuta wanawake wengi wamevalishwa khanga na Tshirt za bure na ukiwahoji baadhi watakueleza wamelipwa bei gani kwenda kushangilia, mimi siwezi kuwalaumu kama CCM imeweka mazingira ambayo zaidi ya nusu ya watanzania hawana uwezo wa kutengeneza hata dola moja kwa siku, kwanini wasipokee dola tatu kwenda kushangilia tuu?
   
 8. T

  Tolowski Senior Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wanawake wasomi wa chadema mbona hawajitokezi kwenye mikutano yao?
   
 9. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  chadema hawatoi kanga, vilemba na mabazee kama chama cha magamba wanavyofanya.
   
 10. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Umeshawahi kujiuliza kati ya wanawake/wanaume au wazee/vijana ni wepi wanahama sana sehemu zao za kazi? Basi kwa taarifa yako hakuna kiumbe kinachoogopa mabadiliko kama wanawake au wazee, mind zao zimejitune kuridhika na walichonacho kiwe kibaya au kizuri.
  1.Kwenye ndoa ukishafikia umri wa uzee hata spouse wako akucheat mtalipeleka swala kwa wazee na mwisho mtaendeleza maisha (wakati kwa vijana mchezo umeishia hapo). Pia ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya wanaume kupenda kujaribu mabadiiko hasa kama hapati kile anachokitaka kutoka kwa spouse wake.
  2. Sehemu nyingi za kazi mtu ukishafikia umri fulani wa uzee hata boci wako akutukane vipi utaendelea kukaa ukisubiri kustaafu, vivyo hivyo kwa wanawake. Si tuliooa tunakutana na incidence za wife anakuja huku analia ooh boc kanitukana, mshahara nalipwa kidogo na mambo mengi mabaya ya kazini, ukimwambia hama anasema nimeshapazoea. Mpaka inabidi we mwanaume ndio ufanye initiative za kumtafutia kazi na umlazimishe sana kuhama.

  Kwa hiyo ukae ukijua vijana hawa wanaoenda kwenye mikutano wanarudi nyumbani kuwasimulia baba zao na wake zao walichosikia na wanachojua kuhusu CDM na CCM, ndio hawahawa wenye uwezo wa kuwaconvice wanawake zao waipende chadema na si kuconviciwa na hao wanawake zao. Mpaka kufika 2015 utshangaa idadi ya wanawake itakavyopungua kwenye hiyo mikutano ya Magamba.

  Wazee na wanawake wanachukua muda kuelewa jambo na kulifanyia kazi kuliko vijana wa kiume, ila siku wakielewa hata utumie mbinu hata za kujikata kichwa hawatarudi.
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wanakuwepo lakini huwezi ukawaona wanatoka mbele na kurukaruka kama wale mnao waajiri CCM, Naamini hata wewe unajua ni kwanini wakati wa mikutano ya CCM kunakuwa na watu wengi ambao ukiwauliza haraka haraka mwenyekiti wa Chama ni nani hawawezi kukujibu
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Jamaa anasema kweli na msimshambulie kabisa.

  Ila nimegundua kuwa WANAUME wa Chadema wana Vifua vimejaza MITINDI?  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  tunaipenda Chadema kwa nguvu zetu zote na hali zetu zote
   
 14. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  chama cha damu na magamba....
   
 15. T

  Tolowski Senior Member

  #15
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana wa kiume si ndio hao osama alikuwa anawavisha mabomu wakajilipue! Siku yake ilipofika yeye akajikinga mbele ya mwanamke!mzee osama ana busara sana!alijua kifo ni noma
   
 16. T

  Tolowski Senior Member

  #16
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So wanawake ni wadhaifu and wanahongeka kirahisi??au cjakuelewa vizuri?
   
 17. T

  Tolowski Senior Member

  #17
  May 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!hawa vijana waandamanaji hawaoneki kama wana wake au wazazi achilia mbali mahali pa kulala!kwa uelewa wao hata anachozungumza slaa kwao ni kama kiarabu
   
 18. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata baadhi ya wanaume kama wewe ninaweza nikakulipa elfu hamsini kwamba fungua akaunti hapa JF alafu kila kukicha wee post utumbo tuu ili kuishusha hadhi ya JF, mbona inawezekana!!
   
 19. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huna haki ya kuusemea moyo wa mtu.
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  msekwa anatoa elfu 50 tu?!!
   
Loading...