Hata bibi yangu anaipenda sana CCM, nimewahoji pia baadhi ya wanawake wa uswahilini pia wanaipenda sana CCM. Nilipotaka kujua nikwanini wanaipenda sana CCM bibi yangu alikuwa na haya "Unajua mjuu wangu mimi nakupenda wewe kwasababu unanijali unapokuja kijijini unaniletea sukari, sabuni, mafuta na mavazi hiyo yoote unafanya kwasababu unanijali bibi yako, vivyohivyo hata CCM naipenda sana kwasababu kila wakija hapa kijijini huwa wanatuletea mavazi ona ile Tisheti na kanga zile walitugawia wao lakini wakija hapa chadema kazi yao ni kuzungumza tuu hata hawatupi Tshirt na kanga kama wanavyo fanya CCM" Mwanamke duni wa uswahilini nilipomuuliza kwanini unaipenda CCM? pia alikuwa na haya "Unajua kakaangu mimi nisikufiche sisiemu nawazimia sana unajua hapa mtaani kwetu kila wakija wanatupatia elfu tanotano za bureee kwa kazi ndogo tuu ya kuvaa Tshirt na kofia kisha kuwashangilia na baada ya kumaliza kazi tunajichana miwali, mikuku na bia hebu niambie Chadema wanaweza hayo? wao kazi yao ni kutangaza sera tuu hata wewe kakaangu unafahamu mkono mtupu haulambwi" Lakini kwa upande mwingine wanawake wasomi, vijana ambao tuko nao maofisini wengi wao hawaipendi CCM kwasababu wanafahamu CCM ni nini? na wanahusika vipi na umasikini unalolikumba Taifa lao. Ukitaka kuthibitisha haya kila kwenye mkutano wa CCM lazima utakuta wanawake wengi wamevalishwa khanga na Tshirt za bure na ukiwahoji baadhi watakueleza wamelipwa bei gani kwenda kushangilia, mimi siwezi kuwalaumu kama CCM imeweka mazingira ambayo zaidi ya nusu ya watanzania hawana uwezo wa kutengeneza hata dola moja kwa siku, kwanini wasipokee dola tatu kwenda kushangilia tuu?