Kwa nini vijana wa kibongo hamfikiri?

Kwa nini vijana wa kibongo hamfikiri?

Yo Yo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Posts
11,210
Reaction score
1,743
Asilimia kubwa ya graduate wa kibongo muulize plan zake hata akiwa chuoni..ni kichekesho kudadadadeki....atakuambia anaomba kwa Mungu apate kazi nzuri yenye kuvaa tai posta mpya then anunue gari GX 100 safi ya kuuzia sura kitaa apange nyumba sinza kwa wajanja then atafute shori mkaliiii
awe anajipoza akishapata hayo ni mwendo wa bata kwa kwenda mbele leo kiwanja kile kesho hajui kama anazidi kuuchosha mwili kila siku anaona misifia kunywa mijipombe eti starehe pumbafu kabisa......later aje aoe si ana kila kitu alafu baabdae mke wake si yupo nyumbani yeye atafute hawala wa kujipooza pembeni wana kamseomo kao eti wanampunguzia wife majukumu pambafu kweri kweri......

Hapo plan zake zimekwisha ukimuuliza anafikiria nini? hana yeye anakuambia anakula maisha anakula bata mwanzo mwisho.....ni upuuzi mkubwa tofauti sana na wengiune.....mie najiulizaga kwanini hakuna vijana wanaofikiria zaidi ya hapo? hakuna creativity kabisa kwa kila jambo...hata maofisini ukienda ni yale yale rijamaa bado lina idea za chuoni kwake hana mpya...hajifunzi kitu kipya....hana knowledge yoyote mpya tangu aingie ofisini....hana kiherehere cha kujua kazi....yeye anakomaa na pale alipoambiwa na boss wake.....unakuta rimtu ni cashier yeye anachojua nji kuhesabu hela na kugawa hajiumizi kichwa kujua zikigawawiwa zinakwenda wapi? na kwanini ziende huko na sio huku.....jitu lingine rinajiita limesoma vema computer si likapata dream job yake benki ya crdb linasimamia networking....halitaki kabisa kujua mambo mengine limekomaa na hicho hicho tu...hajui ipo siku mambo yatabadilika kazi yake itauzwa nje kwa wahindi..yeye atakwenda wapi?...pambaafu kabisa.....majitu kama haya ndio yanayofanyaa mapoyoyo kama wakina nape waendele kutamba na kujua liwalo na waliwe lazima 2K15 lazima warudi kutawala.....majitu hayana creativity kabisa hayafikirii itakuwaje baadae....

JI sensa lenu linasema mko 44MIl naambiwa kati ya hao more than 20mil ni vijana ndio policy maker ndio nyie wenye uwezo wa kuamua uelekeo wa ka'nchi kenu pambafu kabisa......lakini sasa hivi wazee ndio wanaofikiri zaidi ya vijana....vijana wakishafikisha target zao basi wamemaliza.......

Siku hizi na hivi mmejua facebook na JF basi hamna kitu kingine cha kufanya online zaidi ya kuchat kutwa.....angalia hata matangaz ya redio yanalenga huko huko.....eti fikiria pumbafu moja linaweka tangazo kabisa la mtandao wa simu eti mimi nachat na tina kutwa nzima...pumbafu kweri kweri......yaaani walifikiria ndio kazi ya internet kutwa nzima??? badala ya kutumia net kunuoa bongo kufanya kutafiti nyie mnachat?? jinga kweri kweri......haya kusoma vitabu hamuwezi...eti hamna hobby hiyo...yaani mbwiga kabisa nyie......uliza rikijana lolote hobby yake nini? utasikia kichefu chefu....atakuwambia....movie,watch footbal,going out na kuongelea..ukiulizia kakulia shinyanga sijui kaogelea wapi? ukitaka kujua vijana hawana muelekeo na natabiiri kiama chao nenda hata sasa hivi posta mpya au ingia kwenye cafee za mtandao utajua......pita mlimani city....everyone is tryin to make aonekane anawakimbiza wenzake....akili na wadada ndio kabisa bongo zao zimejaa masalo.....

kwa sababu ya kulala kwenu pambafu nyie vijana wa bongo natabiri miaka ijayo raisi atakuwa toka india,waziri mkuu kutoka china mkuu wa majeshi mtutsi wa rwanda na wakuu wa mikoa watatoka bangladesh nyie mtabaki kulia lia na kugomgaania vihamba vya kupanga biringanya kariakoo.......

Nimesikia jana kuwa vijana wa tanga wanaongoza kwa kutembea na wamama watu wazima na mademu vile vile.....sibishi maana vijana siku hizi ndio maana wanaliwa tigo wanapenda vitu vya bure bure sana....nenda kinondoni pale kuna majaa yamevalia nadhifu na kujisugua uso siku nzima na kunyanyua chuma ili kuvutia wamama wawalee pambafu kweri kweri....na linajitapa eti kazi yake ni kutoa dozi kwa jimama....pumbafu kweri kweri ndio maana ukimwi unawamaliza......

Badilikeni mabwiga nyie
 
Yo Yo umeua, umemaliza kila kitu. Lakini sio vijana wote.
 
Last edited by a moderator:
Yo Yo duh balaaa umeua mbaya
Ila sio wote bana wapo wenye vision wanajipanga na wana kila juhudi kufikia malengo yao
Wanapambana kwa kila njia kuhakikisha kuwa malengo yao wanayatimiza na kufikia pale wanapopataka
 
Last edited by a moderator:
Yo Yo duh balaaa umeua mbaya
Ila sio wote bana wapo wenye vision wanajipanga na wana kila juhudi kufikia malengo yao
Wanapambana kwa kila njia kuhakikisha kuwa malengo yao wanayatimiza na kufikia pale wanapopataka
Yo Yo umeua, umemaliza kila kitu. Lakini sio vijana wote.
Yah najua ila walio wengi ni wale wale......mkuu wenye vission ndio hawa wanaolekea uzeeni wengi wao ninaowaona wana approach 40 huwezi kukaa na kijana under 30 mka share kitu cha maana zaidi ya kukuambia kala mademu wangapi wa ustawi wa jamii krisimasi na mwaka mpya...wengi vision zao ni kama zilivyoziandika hapo juu....
 
Yoyo haya uliyoyasema ni ya kweli kabisa. Ni nadra sana kukutana na msomi wa Tanzania ambaye anajisimamia kimawazo, wengi ni kuiga tu. Basi unakuta mtu ana degree yake hana kingine anachowaza zaidi ya ajira Voda (Vodacom). Akishapata basi hapo ndiyo mwisho wa maisha. Angalia hata sehemu kubwa ya majaribio ya kitafiti ama kada zingine kama sanaa kwa Afrika ya Mashariki utayasikia Kenya. Akina dada ndiyo wanatuangusha kabisa. Hadi wasomi sasa wanajichubua ngozi wawe weupe...maajabu!!

Siku hizi kuchat eti ni ujanja na ndiyo maana hata katika threads ambazo ni serious hapa JF utakuta watu wanatumia muda mwingi kusalimiana halafu hawahawa wanaishia kijipachika vyeo vya "u-Great Thinker" na kuwaponda akina Michuzi kana kwamba wao kuna cha maana sana wanachofanya.

"Kila" kijana ni Mwanasiasa.
"Kila" kijana ni Mwanamuziki.
"Kila" kijana ni Mwigizaji filamu. Kila mwigizaji ni Mwongozaji.

Mbona hakuna wavumbuzi? Tumeshindwa kutengeneza Ndege za kijeshi, jamani hata simu tu hatuwezi?

"Man U ana mechi leo?"
 
Yah najua ila walio wengi ni wale wale......mkuu wenye vission ndio hawa wanaolekea uzeeni wengi wao ninaowaona wana approach 40 huwezi kukaa na kijana under 30 mka share kitu cha maana zaidi ya kukuambia kala mademu wangapi wa ustawi wa jamii krisimasi na mwaka mpya...wengi vision zao ni kama zilivyoziandika hapo juu....


lizard_lover_5sfw.jpg
 
Yo Yo nakubaliana na wewe bado mawazo ya wengi ni yale ya kichuo chuo
Na tatizo kubwa ni ile wanawaona wale ambao may be wamemaliza chuo wakapata nafasi wameweza kunua hayo magari na may be kupangisha nyumba mtaani wanajua kuwa na wao yatakuwa so easy wanaweza pata kazi wakanunua gari wakapangisha nyumba na kutembea na madem kwa namna watakavyo bila kuwaza baada ya hapo nini kinafuata. Je kuna maisha baada ya hayo yaani baada ya kula starehe kwa namna atakavyo je kuna maisha mengine

Na jingine ni kuwa makundi nayo yanadanganya sana sana maana wanavyokutana hakuna story nyingine zinazoendelea zaidi ya hizo za idadi ya madem waliotembea nayo au wana mpango wa kutembea na wangapi au ni dem gani anamfukuzia
Hii ndo hali halisi ya maisha ya vijana wengi ambao wanamaliza chuo na hata ukiwa nae kwenye maongezi mengi ya anayoyaongea ni club, madem, gari nzuri na namna anavyopenda kula bata kila siku bia kadhaaa na kiwanja kipya kilichofunguliwa mjini
 
Last edited by a moderator:
Yah najua ila walio wengi ni wale wale......mkuu wenye vission ndio hawa wanaolekea uzeeni wengi wao ninaowaona wana approach 40 huwezi kukaa na kijana under 30 mka share kitu cha maana zaidi ya kukuambia kala mademu wangapi wa ustawi wa jamii krisimasi na mwaka mpya...wengi vision zao ni kama zilivyoziandika hapo juu....
mkubwa leo umeua sana punguza ukali wa maneno kwa sisi wadogo zako!
poa tutayafanyia kazi maneno yako!maana umegonga mlele mkuu
 
About creativity uko right mkuu,wengi wetu wanawaza vitu vya kijinga jinga,kama tumelogwa vile
mtu akipata kikazi anaona amemaliza kila kitu,hafikirii tene,Poor sie vijana!
 
hongera yoyo kwa kufunguka. kuna baadhi pia ya watu wazima wako hivyo hivyo, acha tu, tena ni ni wazee halafu wajiita vijana, hadi 60 yrs bado wanajiona wadogo, na ndio wanaowapotosha kabisa vijana wanaochipukia. maana kijana akiona mzee hakamatiki, anafikiri ndio style ya maisha
 
TATIZO NI HALI YA UKOLONI NDO ILITUMALIZA.... TULINYANYASWA SANA NA KUWA WATUMWA NA MASIKINI TUSIO KUWA NA MALI, sasa tunachojaribu kufanya ni kujikwamua kimaisha ili na sisi tuishi maisha ya raha kama walivyokuwa wakoloni.....

KAZI KWA MWAFRIKA AU MTANZANIA NI KAMA UTUMWA KWAKE...yaani ni kama unataka umtawale pale unapomwambia afanye kazi, tumeadhiliwa na ukoloni... Na hii imeridhiwa mpaka sasa.
 
Kuna mpuuzi mmoja humu leo eti kaniambia Sharo Millionea ndio role model wake, sasa usitalajie kitu cha maana kutoka kwa hawa Watoto.
 
The hypothetical person lacking a sense of humour would likely find the behaviour induced by humour to be inexplicable, strange, or even irrational. Though ultimately decided by personal taste, the extent to which a person will find something humorous depends upon a host of variables, including geographical location, culture, maturity, level of education, intelligence and context.
 
Yo Yo umethibitisha wewe ni kiboko na mwanapinduzi wa kifikra tena asikudanganye mtu eti kuna baadhi wako poa sio kweli ni vijana wote na pia asilimia sabini ya vijana wenzangu wa zamani. Hayo ndio maisha yao na wanajiona wamefika ukiweka mada nzito kwenye mtandao wowote wanatema vijipumba pumba hata havieleweki. Lakini je Yo Yo una habari equations of life zimegunduliwa na mtanzania mwenzetu na zinaweza kuelezea tabia zote hizo, chanzo chake na jinsi ya kurekebisha? hebu tembelea Home na ukishindwa kuziona nijulishe nizimwage juu ya jamvi.
 
uko sahihi na mengi yamesemwa ni sahihi kabisa,cha muhimu vijana tubadilike tuwe na ndoto sahihi za kufikia kufanikiwa
 
ndio maana vijana wa kike na wakiume machuoni baada ya kushindana akili wanashindana kuvaa na kununua simu kali. ubishoo na ustistaduu umewajaa. kazi kwenda klabu na kuchat facebook.kwao ndio mpango mzima
 
hawa ndio wakifika maofisini wakakuta mambo sivyo walivyopanga au kufikiri kabla wanaanza kuiba ili kupata mafanikio ya haraka haraka.
kazi zenyewe hawataki kufanya dili za kuiba pesa ndio wanachowaza saa zote.
 
Back
Top Bottom