Kwa nini unamchoka mkeo? Dawa hii hapa

Kwa nini unamchoka mkeo? Dawa hii hapa

Benjonathantz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2014
Posts
237
Reaction score
52
Habari za saa hizi!

Wanajamvi, Leo nimeona vyema nizungumzie swala la mapenzi ya Ndoa kwa undani kiasi.

Waswahili wanasema ndoa nyingi ni Tamu sana mwanzoni lakini zinapoendelea hufikia Uchungu uliopitiliza. Katika uchunguzi wangu nimebaini sababu kadhaa zinazo sababisha mapenzi ya ndoa kupoteza ladha.
Sababu hizo ni:

1.Unadhifu/Urembo wa awali kipindi cha uchumba hupotea.

2.Majina ya kuonyesha upendo kama vile Mpenzi, Sweetheart , Dear na kadhalika huwa adimu na wakati mwingine hupotea kabisa.

3.Kujali na kuthamini kimapenzi kunafifia: Kwa mfano enzi za uchumba mwanaume alikuwa tayari kumfungulia mkewe Mlango wa Gari lakini siku zinavyozidi kwenda haoni tena tabia kama hizo. Inafifiza mapenzi ya ndoa na kupelekea kuchokana..

4.Kumtoa out mkeo/Mmeo mara kwa mara kipindi cha uchumba havionekani mkiwa ndani ya nyumba.

Hizo ni baadhi ya visababishi ya upotevu wa ladha ya ndoa....

Siku moja mzee mmoja alinimbia Huwezi kula mahindi kila siku. Hii kauli haifai katika maisha ya Ndoa. Ulisha apa kuwa utamlinda, utamheshimu, utakuwa nae hadi kifo kiwatenganishe. Mahidi yanaweza kutumika kama Makande, Ugali au Uji.

Yanayokupasa kutenda ilikudumisha ndoa yenye furaha na Amani ni haya yafuatayo:
1.Kuwa nadhifu/Mrembo zaidi.

2.Mwite majina ya upendo kwa mfano: My lovely wife nk

3.Endelea kumjali na Kumthamini zaidi ya mtu/watu wengine wa kawaida. Na aone jinsi unavyo mthamini

4.Mtoe out mara kwa mara kwenda mbuga za wanyama, Baharini, kwenye Hotel za kifahari na kadhalika.

5. Onyesha furaha unapokuwa nae katika mazungumzo yafamilia na kawaida. Mkiwa njiani onyesha tabasamu kubwa kuonyesha kufurahishwa kutembea na mkeo/mmeo.

6. Leta mada zenye utani usio na mauzi ili kuleta vicheko muda wote ndani ya nyumba.

7. Kuwa mwepesi kusamehe na kusahau makosa ya mpenzi wako..

Kumbuka:
Mkeo/Mmeo ni Bora hivyo Mpende na Umjali kwa dhati.

UKIYAFUATILIA HAYA, FURAHA KATIKA NDOA YAKO ITADUMU DAIMA HADI KIFO.
 
Tatizo wengi huanza na maisha ya bongo movie baadaye yanawashinda rangi zao hali zinaanza kuonekana.
suluhisho ni kuishi kama ulivyo kama hutaweza kumuita honey mwezio siku zote bora usimuite toka mwanzo ukija kuacha kumuita atajua umeacha kumpenda...."......kila mtu atende kama alivyokusudia moyoni"
 
Nimekubali mawazo yako heshima ndugu...
 
kikubwa watu ni kuigiza kama ni mtu mzuri sn kumbe boonge la mwizi.

bora ukutane na mwizi wa nguo kuliko mwizi wa mapenzi
 
kikubwa watu ni kuigiza kama ni mtu mzuri sn kumbe boonge la mwizi.

bora ukutane na mwizi wa nguo kuliko mwizi wa mapenzi

Upo right kabisa. Tatizo wapenzi wengi ni wanafiki. Mapenzi ya kinafki.
 
Sijaoa bado lakini naona upo right sna hi digital life imetuharibu ndoa zetu si vijana wa baaadae zitakuwa ngumu mtu mzima karibia anafunga ndoa lakini kwenye social networks anapost picha eti jayz na Beyonce Kim na kanye anafananisha na yeye na mtu wake wanacopy hadi maisha
 
Kiukweli mapenzi magumu sana watu twaumia eti mtu anasema anakupenda ila simu hakupigii wala hapokei simu zako, hakutumii meseji hadi utume.
Ma
 
natamani niwafunde wale wote wenye matatizo kwenye mahusiano yao na wale wanaojiandaa kuingia kwenye mahusiano natamani mno coz mi naifurahia mno ndoa yangu na tunaishi kwa furaha na amani
 
natamani niwafunde wale wote wenye matatizo kwenye mahusiano yao na wale wanaojiandaa kuingia kwenye mahusiano natamani mno coz mi naifurahia mno ndoa yangu na tunaishi kwa furaha na amani

anza na mimi
 
wakati mwingine mke anachoka mazingira
we kila siku teremka tukaze,chumba kimebanana
out hamuwatoi japo wakaona new fassion
afu mnataka wawavutie eboooo,wanaume wajibikeni som tym!!
 
wakati mwingine mke anachoka mazingira
we kila siku teremka tukaze,chumba kimebanana
out hamuwatoi japo wakaona new fassion
afu mnataka wawavutie eboooo,wanaume wajibikeni som tym!!

ndege wanaofanana huruka pamoko, njoo nikutoe mama!
 
Sijaoa bado lakini naona upo right sna hi digital life imetuharibu ndoa zetu si vijana wa baaadae zitakuwa ngumu mtu mzima karibia anafunga ndoa lakini kwenye social networks anapost picha eti jayz na Beyonce Kim na kanye anafananisha na yeye na mtu wake wanacopy hadi maisha

Mungu atusaidie...
 
[QUOTE
4.Mtoe out mara kwa mara kwenda mbuga za wanyama, Baharini, kwenye Hotel za kifahari na kadhalika
.[/QUOTE]

Kama uchumi unaruhusu
 
Back
Top Bottom