Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
- Thread starter
- #121
nafikiri aliongelea mtu wa kuteua tume. sijaona kwenye majadiliano haya kama si Rais ni nani mwingine anayepaswa kuteua tume kwa sheria zilizopo, wengi wanasema tume iteuliwe na wananchi wenyewe - kivipi?
Prof. Shivji alipendekeza tume iteuliwe na vyuo vikuu na vyama vya kitaaluma je itakubalika na wote?
nilisikia wengi wa wanaharakati wanasema wananchi hawajashirikishwa lakini hawasemi walihoji wangapi?
au wanasema maoni ya wananchi hayajajumuishwa je ni wangapi walioshiriki na ni wawapi?
Hili si tatizo kubwa hivyo. Ni suala la kuweka Principle tu. Kwa mfano sasa hivi Rais anateua mwenyekiti wa bodi na mawaziri wanateua wajumbe wa bodi! Kwanini RAis hateusi wote kwa mpigo? Lakini kwenye Katiba Rais anateua mwenyekiti na Katibu na wajumbe 116!! Rais ndiye anaiitisha Bunge la Katiba na kazi yote mwisho inamrudia yeye kwa maamuzi. Really?