Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo mashangilio ni "tune" au ni wazee wanashangilia? Mimi sioni watu wanashangilia kiasi ya kelele zinazosikika
Vyombo husika ni vp mkuu!kwa majibu ya Rais:
Atafikisha kwa nani?Wengi wanatumia neno kua katiba lazima iandikwe kulingana na mapendekezo ya wananchi lakin wanashindwa kutaja nani atafikisha hayo mapendekeza ya wananchi.
Ndg zangu kitu kilichopo kwa sasa ni kuwahamasisha wananchi wajue kwa nini tunahitaji katiba mpya wala si malekebisho ya katiba!!!!!!! Watu wajue hata wizi wa mchana unaofanywa na CCMna wadau wao ni udhaifu wa katiba iliyopo!!!!!!!!Haiwezekani hawa CCM na mafisadi wake wakajitia kitanzi kwa kuunda katiba makini itakayo peleka wizi woote jela, pamoja na watoto wao!!!!!!!!Lazima wananchi wafanye maamuzi magumu, mbona Kenya walikataa katiba ya kubambikizwa na wakapata katiba mpya after a long struggle ????? Tuikatae hiyo mipango ya katiba ya kubambikizwa na kulinda wezi period!!!!!!!!!!Kuburuzwa ki hivyo haikubaliki!!!!!!!!!mwanakijiji, i am sorry to say you are wrong. kama umemsikiliza vizuri jk leo amekuwa akinukuu katiba hii iliyopo ambayo ina mpa mamlaka ya kuunda Tume ya katiba.
Kwa hiyo kama aliyowahi kusema mnyika huko nyuma kilichotakiwa kufanywa bungeni ni kufanya mabadiliko ya katiba iliyopo sasa na kuigiza kipengele kitachowapa rasmi mamlaka kamili wananchi ya kuunda katiba yao wenyewe bila kuingiliwa na mamlaka yeyote kwahiyo mabadiliko ya katiba nchi hii hayawezekani kwa utaratibu uliopo inatubidi tuingie mtaani kudai haki ya kuamua namna nchi yetu itakavyotawaliwa.
We have to fight back otherwise forget about having the constitution with political and legal legitimacy.
Jamani heeeee mnakuwa kama hamuelewi kwani CCM si ni kundi la washikaji waliolifikisha taifa hili mahali lilipo sasa kwenye umasikini wa kutupwa!!!!!!!!!! Wanacho ngangania kufanya ni kuweka mfumo wa kujilinda pamoja na vizazi vyao waendelee kuibia taifa hili, sijui tumewakosea nini maskini na watoto wao wamekuwa wezi wakubwa!!!!!!!!!! Wanataka mfumo wa kuwalinda waendelee kutuburuza, watu waambiwe waelimishwe wajue hawa jamaa ni wezi wa rasilimali zetu wanafilisi nchi hawana mpango wa kusaidia chochote!!!!!!!!!!!!!Tuingoje kwenye kura za maoni tuipige chini ili tupate katiba itakayo kuwa na maadilimeme kwa taifa letu!!!!!!!!!! Hawawezi kujinyonga ni ngumu tutumie akili ya ziada!!!!Bunge la CCM bila aibu tena kwa ushabiki mkubwa kichama sheria batili ya Makinda inayojitia bingwa kupingana na katiba yetu:
1. Kwa kujiandaa kufunga Wa-Tanzania jela miaka mitatu eti kwa kupinga KATIBA YA KIKWETE na kwamba wala tusiwaze kutumia mamlaka yetu wenyewe kujadili, kupinga na kuunda katiba ya wananchi wenyewe? (The Doctrine of Ultraires)
2. Sheria inayotafuta kutugawa kimatabaka kwa maana kwamba KATIBA YA KIKWETE itapata kuundwa na hata kukosolewa tu na matajiri peke yao nchini ambao ndio wenye uwezo wa kukwepa kwenda jela Ukonga kwa kulipa faini ya milioni moja. (Malice)
3. Sheria iliotungwa sirini kwa maswahiba wachache kualikana wenyewe kwenye mijengo ya kifahari sehemu za mijini tu (Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar) KWA MWALIKO MAALUM ilhali wenye nchi kwa asilimia zetu zaidi ya 80 vijijini tukifungiwa milango nje. (Selective)
...
Tanzania tunachohitaji ni KATIBA MPYA! Katiba tuliyonayo imepitwa na wakati kwa kuwa ilitengenezwa wakati wa uhuru mwaka 1961. Katiba hiyo imekuwa ikifanyiwa mabadiliko (amendments) kuleta Jamhuri mwaka 1962, Muungano mwaka 1964, Chama kimoja mwaka 1965, Azimio la Arusha mwaka 1967 na chama kushika hatamu, vyama vingi 1992 n.k. Sasa imefika wakati katiba hii haifai tena, tunahitaji katiba mpya. Na katiba ni mali ya watanzania, si mali ya CCM, Kikwete, Kombani, Lusinde, Kilango wala Makinda. Kutunyima watanzania haki yetu ya kimsingi ya kuijadili katiba mpya iweje na hatimaye kuikubali ni kututukana. Hivi kwa kuchaguliwa kwao kuwa wabunge ndiyo kumewafanya wao kuwa wana akili kuliko watanzania zaidi ya milioni 43? Watanzania lazima tuamue, vinginevyo kuna watu wachache wanaotaka kulinda maslahi yao ambao wanateka mfumo mzima na wataendelea kufanya hivyo. Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Nakumbuka maneno ya binti mfalme Marie-Antoinette alipomuuliza mama yake, "Kwa nini watu wanaandamana, mama yake akajibu kwa kuwa hawana mkate. Binti mfalme akauliza kwa nini wasile keki?" Hapo wote waliokaa bungeni kujadili muswada wa katiba ndio kina Marie-Antoinette. Mpaka leo hawafahamu kwa nini tunaandamana!
Mkuu uko sahihi sana..hatuhitaji katiba ya KIKWETE wala ya CCM kwani katiba hiyo ndiyo iliyotufikisha hapa...nchi hii ni ya watanzania,siyo ya CHADEMA,CUF,NCCR wala CCM sasa imefika wakati watanzania waamue jinsi wanavyotaka taifa lao kuongozwa..Tume itakayoundwa na KIKWETE itakuwa ya watu wale wale na matokeo ya tume hiyo hata wananchi watoe maoni gani hatima ni ile ile...Katiba ya Kifisadi na chama kimoja,kama kweli watanzania sote tungeelewa umuhimu wa katiba katika maendeleo ya Taifa letu,tungesahau habari ya mimi CCM mimi CHADEMA na tungesimama pamoja kudai katiba ya tanzania itakayosimamia haki,usawa kwa raia wote..Chama kitakachoshinda uchaguzi kitatuongoza kwa kuifuata katiba hiyo..siyo Chama tawala kitengeneze katiba inayowawezesha wao kufanya watakalo
Katiba ya sasa inaweza kuitizama hiyo isue kama uhaini.I stand to be corrected.Nani kaamua kuwa chama chochote hakiruhusiwi kushawishi watu kuvunja muungano?
Unajua unapochaugua kuongelea masuala mazito kwa kuyatoa kama taarifa ambazo unaamini haziingii akilini kwa wepesi lazima uchague na audience itakayoweza kuvumilia huo upuuzi, na mkuu wa kaya analijua hilo kuliko vingine vyote nadhani!
Ndio maana hata kwenye kujibu madai ya walimu na mgomo waliotangaza mwaka jana nadhani, alipokataa kura za wafanyakazi, aliwaita hawa wanaotambuliwa kama 'wazee wa daresalama!'
Nina mashaka na vigezo wanavyotumia katika 'kuwachagua' kwa kuwa wamekuwa ni wepesi sana kupiga makofi kuliko hata kusikiliza, hadi unajiuliza hivi wanasikiliza kweli au wanafurahi kumuona mkuu wa kaya karibu yao!
Hiyo katiba mpya itaundwajwe bila ya Rais?? yaani utaratibu uweje labda tusaidiana hapa maana mimi nashindwa kuwaelewa wengi wenu???
Rais yupo, lakini asiwe na sehemu yoyote katika kuunda katiba mpya. Pamoja na mapungufu mengi ya katiba ya sasa, kuna suala la mamlaka makubwa sana aliyopewa Rais. Ikumbukwe ya kwamba katiba hii ni ya zamani. Kuna wakati ilikuwa ni busara kumpa Rais mamlaka makubwa. Sivyo hali ilivyo sasa, hasa kwa kuwa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi.
Mfano mmojawapo ninaweza kuutoa kwa haraka ni pale Ikulu panapofanyika vikao vya kamati kuu ya ccm. Wakayti wa Mwalimu, chama na serikali vilikuwa 'almost' kitu kimoja. Mkuu wa Mkoa alikuwa ndiye Katibu wa CCM wa mkoa. Mwenyekiti wa CCM alikuwa ndiye Rais. Hapakuwa na mwenye kuuliza swali. Kwa mantiki hiyo, Rais ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CCM, chama pekee cha Tanzania ya wakati ule, na ambacho kilikuwa kikatiba kimeshika hatamu alikuwa anazo kofia zake mbili 'intertwined'. Aliweza kuitisha kikao cha kamati kuu ya CCM Ikulu. Lakini hata hivyo Mwalimu kwa miaka yote alipokuwa ana kofia zake mbili hakufanya hivyo! Vikao vya CCM vilifanyika Makao Makuu ya CCM Dodoma ama ofisi ndogo ya CCM Lumumba. Ikulu ni mahali pa vikao vya baraza la mawaziri ambayo ni serikali. Ndivyo ilivyo kwenye nchi zinazofuata mfumo wa vyama vingi. Huwezi kuona kikao cha Democratic Party Marekani kinafanyika White House!
Katiba imefanyiwa mabadiliko 'amendments' na kusema nchi yetu ni nchi ya vyama vingi. Sasa kwa nini bado jk na serikali yake wanaendelea kufanya kazi katika dhana ya enzi za chama kimoja? Ndani ya mfumo wa sasa ni kosa kwa Rais kufanya vikao vya kichama kwenye ofisi ya serikali. Hapo kunakuja kitu kinachoitwa kwa kiingereza 'conflict of interests' samahani sijui nitumie neno gani kwa kiswahili kuelezea dhana hiyo.
Sasa huo ni mfano mmoja tu, lakini jk kutokana na mapungufu ya katiba ya sasa amekuwa akifanya mambo mengi ambayo ni dhahiri hatakiwi kufanya, ila analindwa na katiba ambayo imepitwa na wakati. Tunapotaka kufanya mabadiliko ambayo yatapunguza mamlaka yake, yeye hapaswi kuwa sehemu ya mchakato huo. Hii ni pamoja na kuteua tume ya watakaokaa na kutunga muswada kamili. Kumwacha jk awemo kwenye mchakato huo ni kujidanganya ya kuwa atachagua watu ambao watakuwa na mtazamo tofauti na wake. Wewe umeona wapi hakimu anashitakiwa mahakamani kwa kosa la jinai halafu yeye ndiye anayepewa mamlaka ya kuchagua mwendesha mashitaka, hakimu na wazee wa mahakama?
Sasa huu ndiyo mfano gani?Rais yupo, lakini asiwe na sehemu yoyote katika kuunda katiba mpya. Pamoja na mapungufu mengi ya katiba ya sasa, kuna suala la mamlaka makubwa sana aliyopewa Rais. Ikumbukwe ya kwamba katiba hii ni ya zamani. Kuna wakati ilikuwa ni busara kumpa Rais mamlaka makubwa. Sivyo hali ilivyo sasa, hasa kwa kuwa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi.
Mfano mmojawapo ninaweza kuutoa kwa haraka ni pale Ikulu panapofanyika vikao vya kamati kuu ya ccm. Wakayti wa Mwalimu, chama na serikali vilikuwa 'almost' kitu kimoja. Mkuu wa Mkoa alikuwa ndiye Katibu wa CCM wa mkoa. Mwenyekiti wa CCM alikuwa ndiye Rais. Hapakuwa na mwenye kuuliza swali. Kwa mantiki hiyo, Rais ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CCM, chama pekee cha Tanzania ya wakati ule, na ambacho kilikuwa kikatiba kimeshika hatamu alikuwa anazo kofia zake mbili 'intertwined'. Aliweza kuitisha kikao cha kamati kuu ya CCM Ikulu. Lakini hata hivyo Mwalimu kwa miaka yote alipokuwa ana kofia zake mbili hakufanya hivyo! Vikao vya CCM vilifanyika Makao Makuu ya CCM Dodoma ama ofisi ndogo ya CCM Lumumba. Ikulu ni mahali pa vikao vya baraza la mawaziri ambayo ni serikali. Ndivyo ilivyo kwenye nchi zinazofuata mfumo wa vyama vingi. Huwezi kuona kikao cha Democratic Party Marekani kinafanyika White House!
Katiba imefanyiwa mabadiliko 'amendments' na kusema nchi yetu ni nchi ya vyama vingi. Sasa kwa nini bado jk na serikali yake wanaendelea kufanya kazi katika dhana ya enzi za chama kimoja? Ndani ya mfumo wa sasa ni kosa kwa Rais kufanya vikao vya kichama kwenye ofisi ya serikali. Hapo kunakuja kitu kinachoitwa kwa kiingereza 'conflict of interests' samahani sijui nitumie neno gani kwa kiswahili kuelezea dhana hiyo.
Sasa huo ni mfano mmoja tu, lakini jk kutokana na mapungufu ya katiba ya sasa amekuwa akifanya mambo mengi ambayo ni dhahiri hatakiwi kufanya, ila analindwa na katiba ambayo imepitwa na wakati. Tunapotaka kufanya mabadiliko ambayo yatapunguza mamlaka yake, yeye hapaswi kuwa sehemu ya mchakato huo. Hii ni pamoja na kuteua tume ya watakaokaa na kutunga muswada kamili. Kumwacha jk awemo kwenye mchakato huo ni kujidanganya ya kuwa atachagua watu ambao watakuwa na mtazamo tofauti na wake. Wewe umeona wapi hakimu anashitakiwa mahakamani kwa kosa la jinai halafu yeye ndiye anayepewa mamlaka ya kuchagua mwendesha mashitaka, hakimu na wazee wa mahakama?
Kwenye mvutano huu,sijui ni kwa vipi katiba ya wananchi itapatikana...Given how serous the issue is to both sides.Pipijojo, kama hujui sheria kama mie hapa, kukaa chini na kuwasikia wataalam siyo dhambi.
Ona sasa unavyojidhihirisha ulivyo mweupe.SOBY, MM Mwanakijiji, JMushi1 na wengine, nimeupenda mjadala wenu zaidi ya hotuba.
Endeleeni kutufungua macho wengine. Naona ngoma bado mbichi sana.
Nimelipenda swali la "Maadamu Kikwete na CCM wana kila kitu, kwa nini hawajaandika wao peke yao katiba......?"
Kinachoitwa mamlaka ya Kikatiba hakitolewi kwenye sheria kinatolewa kwenye Katiba. Sheria hii iliyopitishwa ilitakiwa kwanza kufanyia marekebisho Katiba iliyopo sasa (na iridhiwe na BLW Zanzibar) halafu ndio kutoka hapo tunaweza kuzungumza mengine. Sheria hii imetoa madaraka kwa rais ambayo hana Kikatiba. Rais hana madaraka ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya nchi. Period. Wengi wamekuwa wakijenga hoja ati kwa vile yeye ni Rais basi hayo madaraka yako inherent ndani ya ofisi yake. Hii si kweli. Je Rais ana madaraka ya kuanzisha cheo cha Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano? Wengine wanaweza kusema "ndiyo anayo" kwa sababu yeye ni Rais ukweli ni kuwa hana kwa sababu RAIS ANAYO MADARAKA YALE TU AMBAYO AMEPEWA KWENYE KATIBA.
Labda watu wamesahau tu; Disemba 31 mwaka jana Rais Kikwete alisema hivi akitoa ahadi ya Tume (msisitizo mweusi na mistari wangu):
a. Hivi nani alikuwa na Kikwete walipoamua kuanzisha mchakato huu (hakukuwa na kamati kuu ya CCM, NEC au Mkutano Mkuu wa CCM!)
b. Anayo haki ya kuanzisha tume ya maoni lakini Tume ya kusimamia kuandikwa kwa Katiba Mpya haipo - kwa sababu atakuwa amevunja ahadi yake ya "naapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuru ya Muungano". Mgogoro huu nilikuwa nao pia na wabunge wa Zanzibar waliokuwa wanataka "muungano uvunjwe" wakiwa wameapa kuulinda!
c. Tunavyoona ni kuwa sheria hii imefanya yale ambayo Kikwete aliyataka yafanyika - yeye atakuwa muundani wa tume, yeye ataipa hadidu rejea na tume itaripoti kwake. Mjadala wote wa tangu Machi ulikuwa ni kiini macho tu kwani tayari Kikwete alishaamua nini kifanyike na kimefanyika na siwezi kushangaa kuwa hata Katiba yenyewe itakuwa vile ambavyo yeye anataka.
Mkitaka tuwavuruge kweli!
Watu wadai tuwe na nchi moja! (kanuni ya kulinda Muungano inatumika lakini Zanzibar hawatokubali).
Nani kaamua kuwa chama chochote hakiruhusiwi kushawishi watu kuvunja muungano?