Kwa nini Rais analazimisha kitu ambacho hana madaraka nacho ya Kikatiba? (Video) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Rais analazimisha kitu ambacho hana madaraka nacho ya Kikatiba? (Video)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280


  Kwa haraka inawezekana kudhaniwa kuwa Rais Kikwete ameweza kutetea kwanini yeye ndiye aanzishe na kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Kwamba alitumia madaraka yale yale ambayo yalitumiwa na viongozi wengine wa nyuma- japo mara zote hizo haikuwa kuhusu Katiba Mpya bali kubadilisha katiba iliyokuwepo na kuiboresha na pale ambapo kulikuwa na kwenda kwenye Katiba ya kudumu kulifanyika katika mazingira ya chama kimoja na hivyo kuondoa hoja ya ushiriki wa vyama vingine na hata kuhoji. Rais ndiye alikuwa mkuu wa chama hicho kimoja na ndiye mkuu wa serikali na hivyo inaeleweka kwanini ilikuwa hivyo. Hili halihalalishi hali iyo kurudiwa sasa katika uelewa wetu wa demokrasia ya vyama vingi na ukuu wa wananchi (siyo chama kama ilivyokuwa zamani).

  Hatujawahi kuwepo hapa tulipo sasa. Njia hizo za zamani zilizotumika ndizo zilipotufikisha hapa na tunahitaji ubunifu wa hali ya juu. Kurudia mambo yale yale kwa namna ile ile kuna jina lake lakini kwa vile tunaishi katika zama mpya tungetarajia ubunifu zaidi.

  Katiba ya sasa haimpi Rais kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ana uwezo akitaka wa kusimamia kwa kupitia chama chake mchakato wa kufanya mabadiliko ya katiba ya sasa. Lakini kwa vile anachotaka ni katiba Mpya napendekeza kuwa Katiba ya sasa haina madaraka hayo kwa Rais au kwa mtu mwingine yeyote na kiukali kabisa tunaweza kugeuza na kudai zoezi zima haliwezi kufanya na wale walioapa kulinda Katiba ya sasa! Hakuna kipengele chochote kinachohusiana na kuandika katiba mpya katika Katiba yetu ya sasa. Sasa kama hakuna imekuwaje Rais aamini kuwa ana madaraka ya kuanzisha hata kuitisha Bunge la Katiba?

  Kujibu swali lake la mwisho ni kuwa:

  a. Kabla ya kuundwa kwa tume hiyo ya kukusanya maoni ilitakiwa kwanza yafanyike mabadiliko katika Katiba ya sasa ambayo yangeweza utaratibu wa kuandika Upya Katiba ya nchi. Katiba ya sasa inaruhusu kufanyiwa mabadiliko tu (ammendments) lakini hairuhusu kuwepo kwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya.

  b. Mabadiliko hayo ya Katiba ya kuweka mchakato ndio yangejadili nani na kwa vipi teuzi za tume ya kuandika Katiba unatakiwa kufanyika. Haiwezekani Rais aliyeko madarakani anajiamulia tu kuandika Katiba Upya yeye mwenyewe halafu wengine wafuate; Tukumbuke tamko la kuandika Katiba Mpya lilitolewa kwenye salamu za mwaka mpya! Halikutolewa Bungeni na wala hakukuwa na utaratibu wa kuonesha kuwa umejali wananchi. Ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Kikwete. Tukumbuke kuwa kwenye hotuba ile hakusema "amedhamiria" la hasha alisema "ameamua".

  c. Ni kutoka hapo sasa ndio sheria ya kusimamia mchakato wa kuelekea Katiba Mpya ungeweka. Ina maana ya kwamba suala la Kuandika Katiba Mpya lingewekwa ndani ya Katiba ya sasa na kuangaliwa kama tunavyoangalia yale mambo 8 ambayo yanahitaji ridhaa ya pande mbili za Muungano (theluthi mbili ya wajumbe). Lakini kwa hivi ilivyo Kikwete na Shein wataamua wao wenyewe. Sasa hiyo sheria ndio ingezingatia maoni ya watu wengine.

  Utaona basi kuwa kosa la kwanza limefanyika kwa kutozingatia Katiba ya sasa kwanza - haina mchakato wa kuandika Katiba Mpya - na hivyo kufanya hoja ya Katiba Mpya haiwezi kutolewa na wale walioapa kuilinda ya sasa na kama inatolewa walitakiwa kwanza kufanyia mabadiliko hii Katiba ili wajipe uwezo wa kuzungumzia "katiba mpya".

  Kwa vile suala la Katiba Mpya basi ni la nje ya watawala wetu wa sasa ni wazi kuwa toka mwanzo ushiriki wao ulitakiwa uwepo na siyo mtindo huu wa kuburuzana na kuwapa wananchi taarifa zisizo za kweli kwa ajili ya faida za kisiasa (political expediency). Badala ya kusahihisha makosa wameamua kuendelea katika kukosea. Wananchi wafanye nini?

  a. Watahamasishana wasishiriki kwenye hiyo tume na kuwaachia wana CCM wakaambizane wanayotaka kuyasikia. Yaani A total boycott of the exercise. Hakuna namna ya kuwalazimisha wananchi washiriki. Na kama tulivyoona leo hata wana CCM wenyewe hawako katika hali ya kuruka ruka sana na kufurahia mchakato wenyewe.

  b. Watasubiri ije siku ya kupiga kura ya maoni watahamasishana kwenda kuungusha kwenye sanduku la kura kuwaonesha watawala kuwa wananchi ndio wako supreme zaidi ya Rais na Bunge. Kwa vile wamekubali kuweka kiwango cha chini ya asilimia 50 kupitisha ni kiwango kidogo sana kukifikia! kwani upinzani unahitaji kuhamasisha asilimia 51 tu!

  Sioni dalili yoyote ya watawala kukaa pamoja na kama tuliyoyashuhudia wiki hii ni mfano basi Kikwete hayuko tayari hata kukubali hoja za upande wa pili - ila upande wake ndio anataka ukubaliwe bila kuhojiwa au kupingwa. Na uamuzi wa kuweka adhabu kwa watu watakopinga mchakato huu umethibitisha pasipo shaka kuwa kwa njia ya kawaida haiwezekni kushinda isipokuwa kwa shurti, vitisho na vifungo.


  Utabiri wangu: Mswada huu utarudishwa mapema tena Bungeni ili ufanyiwe marekebisho kama walivyofanya kwenye msaada ya gharama za uchaguzi ambao wengine tuliupinga na kuonesha makosa mapema wakang'ang'ania na kusaini kwa mbwembwe lakini miezi mitatu tu baadaye wakaurudisha na bado wanahitaji kuufanyia marekebisho. Mswada huu ukiwa sheria hautekelezeki, haukubaliki, na watawalazimisha watu kuupuza. Tunaposema katiba ni 'mama' hatusemi tu hivi hivi. Sasa mama habambikiziwi! Vingenevyo wapo Watanzania ambao wataiona katiba ijayo kuwa ni 'katiba ya kambo'! Hawataipenda, hawataizingatia na watajaribu kweli kweli kuibadilisha. Kama Rais wa sasa ameweza kufanya hivi bila kuulizwa na mtu guess what akija Rais mwingine?

  Hadi wakubali kusikiliza upande wa pili na kufuata ile kanuni ya kwanza - KATIBA LAZIMA ITOKE KWA WANANCHI WENYEWE. Kuanzia mfumo wa kuwashirikisha wananchi, nani anasimamia na inafikiwa vipi ni lazima iwe inasimama kwenye madaraka ya wananchi kutawala.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mwanakijiji, i am sorry to say you are wrong. kama umemsikiliza vizuri jk leo amekuwa akinukuu katiba hii iliyopo ambayo ina mpa mamlaka ya kuunda Tume ya katiba.

  Kwa hiyo kama aliyowahi kusema mnyika huko nyuma kilichotakiwa kufanywa bungeni ni kufanya mabadiliko ya katiba iliyopo sasa na kuigiza kipengele kitachowapa rasmi mamlaka kamili wananchi ya kuunda katiba yao wenyewe bila kuingiliwa na mamlaka yeyote kwahiyo mabadiliko ya katiba nchi hii hayawezekani kwa utaratibu uliopo inatubidi tuingie mtaani kudai haki ya kuamua namna nchi yetu itakavyotawaliwa.

  We have to fight back otherwise forget about having the constitution with political and legal legitimacy.
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi sijawahi kuona mwanasiasa anae zungumza na watu kwenye mkutano huku amekaa, nadhani huyu siyo raisi hata mtitiriko wa sauti yake haina hadhi ya uraisi
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kwa nini wameweka vitisho vya hukumu na vifungo mtu akihoji? kama huo si udikteta ni nini waache kabisa mchezo tutamalizana kwa ajili ya katiba, wachezee katiba ya CCM si hii.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Alinukuu kipengele gani?
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nyie ni miongoni mwa wanaofikiri kuwa Rais hapotoki.
  Bw. KIKWETE kaishia kurusha vijembe na kwakua alikua anasikilizwa na wababu waliochoka akili ndio maana wakampigia makofi.
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nimemnukuu tu yeye kuwa anadai kuwa anayo mamlaka hayo na katiba na pia ametoa mfano wa tume mbalimbali huko nyuma za kushugulikia maswala ya katiba mwaka 1963 na mwaka 1983 ambazo ni Rais ndio aliziunda utaratibu ambao binafasi sikubaliani nao kwani kwa kuwa ulitumika mwaka 1983 na 1963 basi unafaa kwa watu wa 2011 that is wrong. kwahiyo kama hakuna kipengele chochote basi ndio itatupa hoja nzuri ya kuingia barabarani hiyo jumapili.
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Sote tumemsikiliza hakunukuu kipengele chochote cha katiba alichokuwa anafanya ni kutoa historia ya matukio ya mabadiliko ya katiba tangu uhuru. Kosa analofanya ambalo linaweza kumuingiza matatani huko mbele ni kuvunja katiba kwa kujipa mamlaka asiyokuwa nayo, atuambie ni kifungu gani kinasema yeye na rais wa Zanzibar watashauriana kuunda tume, mimi nilimstukia toka mwanzo wa hotuba amerudirudia sana kuwa yeye na serikali hawajavunja katiba alijua, angalizo aangalie asije kushtakiwa kwenye mahakama za kimataifa.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,584
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  Hajanukuu kipengele chochote,na si kwa bahati mbaya,ni kwamba hakuna,amebakia tu kusema hakuna sheria iliyovunjwa na kutumia mifano irrelevant ya "maboresho" yaliyowahi kufanywa kipindi cha nyuma mengi wakati wa utawala wa chama kimoja. Hatujawahi kuwa na katiba mpya kama anavyotuaminisha.

  Pia vile vile katiba iliyopo ameapa kuilinda na tutegemee atafanya hivyo kwa kutumia every "weapon" at his disposal.

  Kama ni kweli tunataka katiba mpya ya wananchi,basi ni lazima umakini wa hali ya juu uwepo in every single step of the process.
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  binafsi nakubaliana nanyi kuwa hakuna kipengele kama hicho swali langu kwenu je rasimu hii iliyopita haimpi mamlaka Rais ya kuunda Tume ya katiba ingawaje yeye anadai kuwa katiba iliyopo sasa ndio imempa mamlaka je rasimu hii iliyopitishwa na Bunge haimpi mamlaka haya ambayo katiba ya hivi sasa haimpi naombeni ufafanuzi ???
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAMBO TISA YA MSINGI MNO AMBAYO RAIS KIKWETE NA WASHAURI WAKE WALIJISAHAULISHA JUU YA 'MUSWADA WA MKINDA' NA NAFASI YA KUFANIKIWA NAYO AU MDORORO HADI MWISHO

  1. Pamoja na kuwa na dola, ili sheria yoyote ifanikiwe ni sharti ipate ridhaa ya wananchi na uhiari wa kuinga mkono katika hatua zote.

  Hadi hapa ni mtu mwenye mtindio tu wa akili anaweza kuunga mkono
  mchezo ambao kanuni zake ni sharti zinyeshe kama mvua ya mawe toka angani na kwamba ushiriki wao kwenye kuunda kanuni hizo ni batili kwa namna yoyote ile.

  Wananchi wala hatuna mkono na hata kujihisi kule kuwa sehemu ya waundaji wa hizo kanuni za kuongoza upatikanaji wa katiba mpya. Ni kwa sababu hii ndio maana tunamuachia Rais Kikwete kutumia nguvu nyingi sana za Said Mwema kulazimisha upatikanaji wa katiba mpya kwa mkondo wao huo huku sisi tujitafutia mkondo wetu wenyewe utakaotuweka kwenye KITI CHA MADEREVA wa mchakato wa upatikanaji katiba mpya badala ya kulazimishwa na mtu yeyote kugeuzwa ABIRIA kwenye gari letu sisi wenyewe. Dr Bana elimu yako isitumike kuchumia tumbo kiasi hicho; tu nasema hatukubaliani kuburuzwa.

  2. Licha ya Katiba yetu kuandikwa safari TANO tofauti, ni safari hii tu katika historia ambapo Watanzania tumewiwa kujitungia katiba wenyewe bila kutungiwa na baadhi ya watawale kama ambavyo ilivyokua ada huko nyuma. Hii ndio maana tunakataa udalali ama wa ikulu au CCM katika hili.

  3. Kwamba uundwaji wa katiba wala si shughuli ya kiserikari hivyo kufanya mtu yeyote kujitwisha jukumu la kuliongoza na kuteua watu wake kwa kuegemea cheo chake cha kiserikali.

  4. Marais waliopita walichokifanyia katiba yetu huko nyuma ilikua ni marekebisho madogo madogo ya hapa na pale amb ayo kimsingi ni shughuli ya kibunge kushughulika na uundwaji wa sheria kama hizo. Ila kwa safari hii tunachokusudia kufanya si kutia viraka zaidi bali ni kuliunda upya katiba yetu ya nchi hivyo urais wa mtu ndipo unopokosa nafasi kwenye shughuli hii pevu.

  5. Mabadiliko ya huko nyuma yalikua ni yale ya chini ya mfumo wa chama kimoja na hata wakati mwingine ilionekana ni vema CCM kujikamilishia tu yenyewe kupitia kwa kutumia tu mitandao yake tu ya ndani kichama. Tofauti kabisa na misingi hiyo, wito wa wananchi kutaka kujiundia upya na wenyewe katiba mpya hivi sasa ni zoezi chini ya mfumo ya vyama vingi hivyo usimamiaji wa shughuli nzima, uteuzi wa tume, kupeana hadidu za rejea ya kazi ni sharti utokane na sura hizo za sasa na kwa uwiano wa aina hiyo hiyo vile vile. Tofauti na hapo, hakuna kitu hapa!!

  6. Pamoja na yote, hivi sasa serikali yetu imelalamikiwa sana tu kughubikwa na vitendo vya ki-fisadi dhidi ya umma wanaotuongoza na kwamba lengo kuu la katiba ni kutafuta kuziba mianya wanazozitumia hivi sasa kutukwapulia kodi na kuturudisha nyuma ki-maendeleo hivyo kuoneka kuwa ni genge kuuuubwa lenye watu waliokosa uadilifu ki-uongozi.

  Kwa kigezo hicho hicho cha uongozi mzima wa serikali kuonekana dhahiri kutiliwa shaka katika mambo mengi sana tu na hasa kule kudaiwa kutuchakachulia uchaguzi wetu mkuu hapo mwaka jana, ni dhahiri kwamba haku mwananchi yeyote mwenye akili timamu atakayekubaali kuunda katiba mpya chini ya watu ambao kwao ni zaidi ya mafisi watu.

  7. Muswada wa CCM kujiundia Katiba ya kiserikali ni mswada na hatimaye kuelekea kuzaa SHERIA BATILI inayopingana na misingi ya katiba yetu ya sasa hivyo kujiweka katika hatari kubwa mno ya KUPINGWA KISHERIA katika mahakama ya kikatiba au nyinginezo wakati wowote tangu hivi sasa hivyo wenye kujisherehesha katika ubatili wake wote huo, hebu kwanza kaficheni shahada zenu za maua maana hata Rais Kikwete akiidhinisha ki-ushabiki na kiitikadi za kisiasa zaidi kama ambavyo hali inavyoonyesha tangu awali, WALA KITENDO HICHO TU KAMWE HAKIWEZI KUIFANYA KATIBA YETU YA SASA KUWA MTUMISHI WA MSWADA WA CCM ila ukweli ni kwamba kinyume cha hapo ni WAJIMBU NA NI LAZIMA!!

  8. Kwa mtaji wa hotuba ya Rais Kikwete kwa kundi la wazee wa chama chake cha CCM mkoani Dar es salaam, ni wazi kwamba rais hajaelewa kwamba kwenye utunzi sheria na utekelezaji wake wananchi huwa tunahiari KUKASIMU MADARAKA yetu kwao kupitia mkataba maalum uitwao katiba ila kwa uundwaji wa katiba yenyewe hata mshauri wake Dr Bana anajua kwamba HATUWEZI HATA KIDOGO KUWAKASIMIA vile vile madaraka wakatuketelezee haya yalio haki yetu ya msingi kabisa!!!!!!!!!!

  9. Kwa kuwa Rais Kikwete mpaka hivi sasa ndiye Nahodha wa timu ya mpira wa kisiasa iitwayo CCM, hivyo kuwa ni mdau na uzao wa katiba, inayoshindana na timu nyinginezo za mpira wa kisiasa kama vile CHADEMA FC, TLP, NCCR-Mageuzi na hizo timu nyinginezo, Misingi ya utawala bora ambayo yeye mwenyewe amekua akiimba mdomoni bila kuchoka lakini kwa matendo kinyume chake zaidi ya hata Mzee Wasira anavyojulikana kufanya kila uchao, kamwe haimruhusu yeye kujitangaza na au kutangazwa na bunge la CCM kujitwisha na kofia la pili la KUWA REFAREE kwa wakati huo huo katika mashindano ambayo yeye ndiye jemadari wa upande wake wanapopanga mashambulizi kwa timu pinzani.

  NB: Kwa haya machache ni kwamba Rais Kikwete ajisikie huru kuongoza kundi moja la kuunda KATIBA LA KISERIKALI NA KICHAMA tangu mwanzo wa zoezi lao zima huku na sisi wananchi kukijikusanya kwa makundi yetu tukijipanga ndani ya Baraza la Katiba Taifa kujiundia katiba mpya bila mizengwe na mwisho wa siku tukazikutanishe rasimu zetu kushindanishwa kwenye kura ya maoni hapo mwisho wa siku. Shughuli sasa ianze mara moja bila vurugu wala kupoteza wakati.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Kinachoitwa mamlaka ya Kikatiba hakitolewi kwenye sheria kinatolewa kwenye Katiba. Sheria hii iliyopitishwa ilitakiwa kwanza kufanyia marekebisho Katiba iliyopo sasa (na iridhiwe na BLW Zanzibar) halafu ndio kutoka hapo tunaweza kuzungumza mengine. Sheria hii imetoa madaraka kwa rais ambayo hana Kikatiba. Rais hana madaraka ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya nchi. Period. Wengi wamekuwa wakijenga hoja ati kwa vile yeye ni Rais basi hayo madaraka yako inherent ndani ya ofisi yake. Hii si kweli. Je Rais ana madaraka ya kuanzisha cheo cha Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano? Wengine wanaweza kusema "ndiyo anayo" kwa sababu yeye ni Rais ukweli ni kuwa hana kwa sababu RAIS ANAYO MADARAKA YALE TU AMBAYO AMEPEWA KWENYE KATIBA.

  Labda watu wamesahau tu; Disemba 31 mwaka jana Rais Kikwete alisema hivi akitoa ahadi ya Tume (msisitizo mweusi na mistari wangu):
  a. Hivi nani alikuwa na Kikwete walipoamua kuanzisha mchakato huu (hakukuwa na kamati kuu ya CCM, NEC au Mkutano Mkuu wa CCM!)
  b. Anayo haki ya kuanzisha tume ya maoni lakini Tume ya kusimamia kuandikwa kwa Katiba Mpya haipo - kwa sababu atakuwa amevunja ahadi yake ya "naapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuru ya Muungano". Mgogoro huu nilikuwa nao pia na wabunge wa Zanzibar waliokuwa wanataka "muungano uvunjwe" wakiwa wameapa kuulinda!
  c. Tunavyoona ni kuwa sheria hii imefanya yale ambayo Kikwete aliyataka yafanyika - yeye atakuwa muundani wa tume, yeye ataipa hadidu rejea na tume itaripoti kwake. Mjadala wote wa tangu Machi ulikuwa ni kiini macho tu kwani tayari Kikwete alishaamua nini kifanyike na kimefanyika na siwezi kushangaa kuwa hata Katiba yenyewe itakuwa vile ambavyo yeye anataka.

  Mkitaka tuwavuruge kweli!

  Watu wadai tuwe na nchi moja! (kanuni ya kulinda Muungano inatumika lakini Zanzibar hawatokubali).
   
 13. T

  Taso JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Msaada kwenye tuta. Hivi hiyo "tume ya kukusanya maoni" ikishakusanya maoni itayapeleka wapi, au itayafanya nini?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa majibu ya Rais:
   
 15. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Act No.15 0f 1984. Section 12
  Labda uanze na Article 62 (1) and (3).
  Oanisha na article 64(1).
  Halafu jaribu kuoanisha na article 63(1) na (3)(d).
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  What a cheap shot.
  Kwanini usitumie act iliyopitishwa jana, badala yake unatumia hotuba?
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Anhaa, kumbe kuna la zaidi ya "kukusanya maoni." Hayo "mapendekezo" ndio draft ya Katiba au?
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,584
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  Fafanua zaidi mkuu,zinasemaje?
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Nov 19, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [h=3]KIKWETE HAS A POINT BUT HERE IS A COUNTERPOINT[/h]
  [​IMG]
  "We don't need JK's Commission! It will disturb the process by being malicious to the process in favour of the ruling party....we need first of all to amend the current Constitution especially article 98. The amendment that shall allow formation of an independent commitee not emanating from JK or any president thereto. This commission shoul include representatives from all walks of life ranging from ordinary citizens, religious leaders, CSOs, politicians and political parties, legal experts etc in our country that will collect the views of the people...it is not possible to suspend a constitution in any society if there is no revolution by mass or military coup de tat. In peaceful mood as in Tanzania we cannot suspend the current constitution...mind you to suspend a current constitution in absence of military coup de tat or mass revolution like the ones in Egypt, Tunisia or elsewhere amount to treason which is one of the capital offences in our law. Even JK HAS NO POWER legally to suspend a constitution because he was sworn in to defend it no matter how bad it is...." - A Young Tanzanian Lawyer in a Constitutional Debate, March 2011
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huwezi kutaja ACT itokanayo na sheria inayotafuta KULITUMIKISHA KATIBA YETU YA SASA iendane nayo badala ya bunge kukidhi msingi mama wa kufanya sheria zote za nchi KUITUMIKIA sheria mama ambayo ni katiba ya nchi.

  Indeed, yours is a miserably confused shot here!!

   
Loading...