Bado sioni sababu ya kuficha ficha simu kama kweli huna cha kuficha.
Ukiwa mwaminifu kweli basi hutaona shida ya kuwa muwazi kwa mwenzako.
Ukiwa mwaminifu kweli hutaona shida ya kujibu maswali ya mwenzako.
Ukiwa mwaminifu kweli hutakuwa na sababu ya kumficha mwenzako simu yako.
Ukiwa mwaminifu kweli hutapatwa na ugonjwa wa moyo mwenzako akiishika simu yako.
Kwa hiyo hakuna kilicho kigumu hapo kama kweli upo mkweli.
uko sahihi mkuu na wala sipingi hata sehemu moja.
Ila kuna case ilitokea nikaona umuhim wa kumjua mwenza wako na ujue una deal vipi na simu.
Kuna mtu wangu wa karibu sijui alikuwa anafanyiwa kusudi au ndio tabia ya yule mwanaume wake.
Mwanaume hataki namba za wanaume kwa phone book, zaidi ya ndugu alozaliwa nao tu.
Hataki picha akute za watu wengine hasa za wanaume(mambo ya whsatsap hasa kwenye groups picha zinajaa)
hataki apige simu akute call waiting, hata ukiongea na mama yako anataka ukate, umpokelee yeye.
Na mengine mengi.
Binti alikuwa muaminifu kwa jinsi alivyoonekana na alimuheshimu sana mchumbaake huyo, walikuwa kwenye process za ndoa.
Akija, anaweza kukaa siku nzima anakagua simu wakati hawajaonana hata miezi miwili.
Alivumilia yakamshinda, akawaambia kwao hataki kuolewa na huyo bwana, wasitishe process.
Kwa mtu kama huyo, asieelewa utamwambia bado anaficha ficha simu bila sababu?
Point yangu iko pale pale. UAMINIFU NI MUHIMU KATIKA MAHUSIANO.
DEAL NA SIMU YAKO KUTOKANA NA AINA YA MWENZA ULIYENAE