Kwa nini mwanandoa unaficha ficha simu

Kwa nini mwanandoa unaficha ficha simu

Mtu akificha sim yake n waz ana jambo baya hatak mwenzie ajue

hakuna sababu ya kuficha simu. Kufanya hivyo ni dhahiri kuna jambo unaficha. na hakuna sababu ya kupekua simu ya mwenzako kama na wewe unayo yako. Kufanya hivyo ni dhahiri kuna jambo unatafuta. Yote hayo mawili ni mabaya kwa mahusiano.
 
nakubali uaminifu ni suala muhimun na huambatana na uwazi maana kama kukiwa na mazingira ya kuficha vitu, hisia za usaliti huanza kujitokeza. Lakini vile vile kumtilia mashaka mwenzi wako hutengeneza hisia kuwa humuamini na yeye anaweza kuanza kujenga hisia za kutokukuamini vile vile. Amini usiamini, suala la kupekua simu ya mwenzio kusoma message alizotuma ama kutumiwa halina afya ndani yake hata kidogo. kama kuna jambo anapenda kukushirikisha atakwambia na kwa kuwa unaamini kuwa hatakuficha lile ambalo angependa ujue. Tutabishana sana lakini mimi sioni sababu ya kuanza kupekenyua simu ya mke wangu kabisa. Kama nina nia ya dhati kuitumia simu kuandika message au kupiga, jitafanya hivyo lakini si kuanza ku-scroll message zote hadi pale nilipoishia jana...

Bado sijaona hoja ya kunishawishi kwamba ni kosa kubwa au si sawa kushika simu ya mwenzio.

Kama kweli kabisa hiyo simu haina chochote kile kilichokibaya kinachoweza kumfanya mwenzako achukie au akuhisi kwamba hauko mwaminifu, basi sidhani kabisa kama wewe mwenye simu utaona shida yeye akishika simu yako.

Mtu kama huna la kuficha wala hutapatwa na kiroho dunda kama mwenzako akishika simu yako. Na wala hutakuwa unaing'ang'ania kama ruba.

Hii ni common sense 101. Kama mtu huna la kuficha basi hutaificha simu yako!

As simple as 1,2,3 or A,B,C......not rocket science!
 
Na aipekuaye simu ya mwenzake je...? anatafuta nini?

Anachokitafuta anakijua yeye mpekenyuaji.

Lakini, kama hamna kitu kibaya humo kwenye simu, hata apekenyue mara bilioni elfu tano, hatakuta kitu.

Na kama kweli hakuna kitu kibaya humo kwenye simu, mimi binafsi wala sitakuwa na shida kama akiamua kupekenyua mara bilioni elfu kumi maana hatakuta chochote kibaya.

Kwangu mimi kuficha kunaashiria ubaya zaidi kuliko kupekenyua.
 
Sawa, lakini unajua huyo anayepekenyua akishakuwa na nia ovu anachofanya? Atahakikisha ili kujenga uhalali huo anaiacha yake free ili 'na wewe' uipekenyue kama atakavyopekenyua yako. lakini kabla ya hapo inafanyiwa cleaning kiasi cha kutosha ili iwe safe for your eyes!

All in all, inabidi watu wawe waaminifu kwenye mahusiano ili woga wa kupekenyuliwa simu usiwepo, na wala kiherehere cha kupekenyua simu ya mwenzako kisiwepo. Bitter pill to swallow ni kwamba: Faithfulness 101 course wengi ni failures! Hawafai hata ku-carry! matokeo yake ndio inaanza michezo ya call barring na simu 'zinazoishi' kwenye gari tu, haziingii ndani ya nyumba.

Complete failure in relationships.
 
Na ieleweke kuwa kila mtu anasimu yake hivyo basi kila mtu ashike simu yake
 
nakubali uaminifu ni suala muhimun na huambatana na uwazi maana kama kukiwa na mazingira ya kuficha vitu, hisia za usaliti huanza kujitokeza. Lakini vile vile kumtilia mashaka mwenzi wako hutengeneza hisia kuwa humuamini na yeye anaweza kuanza kujenga hisia za kutokukuamini vile vile. Amini usiamini, suala la kupekua simu ya mwenzio kusoma message alizotuma ama kutumiwa halina afya ndani yake hata kidogo. kama kuna jambo anapenda kukushirikisha atakwambia na kwa kuwa unaamini kuwa hatakuficha lile ambalo angependa ujue. Tutabishana sana lakini mimi sioni sababu ya kuanza kupekenyua simu ya mke wangu kabisa. Kama nina nia ya dhati kuitumia simu kuandika message au kupiga, jitafanya hivyo lakini si kuanza ku-scroll message zote hadi pale nilipoishia jana...

Watu wabaya mkuu wanasoma conversation zooote ni shida mtu unakuwa huna uhuru na simu yako hata kama hufanyi maovu
 
Sawa, lakini unajua huyo anayepekenyua akishakuwa na nia ovu anachofanya? Atahakikisha ili kujenga uhalali huo anaiacha yake free ili 'na wewe' uipekenyue kama atakavyopekenyua yako. lakini kabla ya hapo inafanyiwa cleaning kiasi cha kutosha ili iwe safe for your eyes!

Sasa unachofanya wewe hapa ni ku-speculate tu. Lakini kwa lengo la majadiliano hakuna ubaya.

Yeye akifanya hivyo basi hilo litakuwa tatizo lake na si lako na hata nafsi yake kuna uwezekano mkubwa tu kuwa itamsuta kwa sababu ya huo unafiki wake na ipo siku huo unafiki utabumburuka tu.

Kiini cha hoja yangu hakipo kwa upande wa pili. Kipo kwa upande wako (wewe mwenye simu). Kama wewe kweli kabisa huna cha kuficha ndani ya hiyo simu wala hutakuwa na wasiwasi wowote ule endapo mwenzako ataishika simu yako.

Kama kweli hufanyi lolote lile lililo baya basi hata akikuomba mbadilishane simu kwa siku au wiki nzima, hutakuwa na shida wala wasiwasi wowote kutekeleza hilo ombi lake.

That's just basic common sense!

All in all, inabidi watu wawe waaminifu kwenye mahusiano ili woga wa kupekenyuliwa simu usiwepo, na wala kiherehere cha kupekenyua simu ya mwenzako kisiwepo.

Hapana. Kwa mtazamo wangu naona ni vyema mtu kuwa mwaminifu kwa mwenzako katika hali yoyote ile na si kwa hofu au woga wa kupekenyuliwa simu.

Simu isiwe ndo sababu ya mtu kuwa mwaminifu kwa mwenza wake.

Bitter pill to swallow ni kwamba: Faithfulness 101 course wengi ni failures! Hawafai hata ku-carry! matokeo yake ndio inaanza michezo ya call barring na simu 'zinazoishi' kwenye gari tu, haziingii ndani ya nyumba.

Complete failure in relationships.

Hapo nakubaliana na wewe.
 
Watu wabaya mkuu wanasoma conversation zooote ni shida mtu unakuwa huna uhuru na simu yako hata kama hufanyi maovu

Kama hufanyi maovu mi nadhani ndo unakuwa huru zaidi na hiyo simu yako.

Maana hata ukiisahau mezani ukiwa umeenda sokoni hutopatwa na kiwewe.
 
Kama hufanyi maovu mi nadhani ndo unakuwa huru zaidi na hiyo simu yako.

Maana hata ukiisahau mezani ukiwa umeenda sokoni hutopatwa na kiwewe.

Aaaghhhh!!!!! Inaboa sana kwaio asome kila kinachojili ktk maisha yangu ya kila siku?????? Kuna mambo ya kifamilia sio lazima ajue..... Mastory na mashosti zangu aaghhh mtupishe na nyie na ufukunyuku wenu
 
Hoja siyo suala la kusoma kila kinachojiri.

Hoja ni kwa nini mtu upatwe na kiroho dunda kisa simu tu?

Ni mambo gani ya kifamilia ambayo hutaki mumeo ayajue?

Kwa nini mtu utake kumficha mumeo (ambaye ni sehemu ya familia) mambo ya kifamilia?

Ni ujinga mtupu na ndo maana kuna watu wanaona hayo mambo ya ndoa ni unafiki.
 
Simu kama moyo wa mtu. Hivyo mwenye kuficha na afiche na aliye tayari kuweka wazi aanike..otherwise "Usiusemee moyo"
 
Nilishamtahadharisha mkewangu, akitaka kuharibu siku yake, achokonoe sime yangu, hasikii, tangu juzi analia baada ya kukuta sms za utani wa maofisini. MSIBA MZITO:der:
 
Watu wabaya mkuu wanasoma conversation zooote ni shida mtu unakuwa huna uhuru na simu yako hata kama hufanyi maovu[/QUOT

then wewe una matatizo na huo uhusiano wako au hujamridhia huyo ulie nae meaning that kuna mipango ya kando nje unayoiona zaidi. wewe unakua unaficha conversation gani labda haswa huyo partner asione? ah huo unaitwa wizi mtupu bana. hakuna kitu kama private kwa mahusiano. mficha simu anaficha uozo
 
Aaaghhhh!!!!! Inaboa sana kwaio asome kila kinachojili ktk maisha yangu ya kila siku?????? Kuna mambo ya kifamilia sio lazima ajue..... Mastory na mashosti zangu aaghhh mtupishe na nyie na ufukunyuku wenu

huo ni ubinafsi kati yenu. hizo stori zote ulizotaja na mashosti,na familia si za kuficha. labda kama napo hapo huwa mnamteta mkichat. huo unakua kama uhusiano wa paka na panya
 
Nilishamtahadharisha mkewangu, akitaka kuharibu siku yake, achokonoe sime yangu, hasikii, tangu juzi analia baada ya kukuta sms za utani wa maofisini. MSIBA MZITO:der:

yeye ni mtu mzima. ninaamini anajua tofauti ya utani wa kiofisi na vinginevyo vibaya vinavyoweza kujiri. ukweli unao mwenyewe. sio vizuri lakini, kwa nini uwe na utani wa ajabu ajabu tena kwa chats namna hiyo kama kweli ni utani? je angekuwa ni yeye umekuta hivo?
 
ukweli hizi simu inaweza sababisha ndoa kuwa hatarini bora tu kila mtu ashike simu yake, kuna siku imeingia msg. kwenye simu yangu inasema" Baba asante sana kwa ulichonifanyia jana, ukweli baba tangu niolewe sijwahi kuwa na mpenzi nje ya ndoa yangu ni wewe tu baba, na penzi unalonipa hata mume wangu hanipi hivyo, wala hajawahi kunipa penzi kinyume cha maumbile kama wewe asante baba". Hii ni msg ya kweli kabisa wala sijatunga, imagine iliingia usiku na uzuri mimi ni mwanamke sasa pata picha ningekuwa wa kiume ingekuwaje? Kesho yake nilimpigia simu huyo mwanamke nilimchamba balaa kuanzia siku hiyo cm yake haipatikani sijui kabadili line? Anajidai anaadabu eti baba, baba kila sentesi, hizi CM ni janga.
 
Duuu kumbe huko kwenye ndoa kuna furugu mechi (vurugu) na simu mwee..........si muwafunge GPS basi
 
unapozungumzia neno ''kuichunguza'' wamaanisha nini??

Mimi binafsi sikamati cm ya mpenzi wangu for no reason,,

labda kama imeita na hayupo(i receive on behalf)
au kuna app. Ipo kwake mie sina,then natumia sim yake.

Ni upuuzi kushika cm ya mpenzio kwa kuhisi tu.,, michepuko. Upuuzi.

you receive it on behalf, siku moja utakuja tukanwa bureee!
 
Back
Top Bottom