Kwa nini mwanandoa unaficha ficha simu

Kwa nini mwanandoa unaficha ficha simu

Bado sijaona hoja ya kunishawishi kwamba ni kosa kubwa au si sawa kushika simu ya mwenzio.

Kama kweli kabisa hiyo simu haina chochote kile kilichokibaya kinachoweza kumfanya mwenzako achukie au akuhisi kwamba hauko mwaminifu, basi sidhani kabisa kama wewe mwenye simu utaona shida yeye akishika simu yako.

Mtu kama huna la kuficha wala hutapatwa na kiroho dunda kama mwenzako akishika simu yako. Na wala hutakuwa unaing'ang'ania kama ruba.

Hii ni common sense 101. Kama mtu huna la kuficha basi hutaificha simu yako!

As simple as 1,2,3 or A,B,C......not rocket science!

unachosema ni kweli ila pia inategemea na mwenza uliyenae.
Kuna wenza wengine wana-gubu. Hataki hata uwe na namba ya jinsia nyengine, utadhani wewe wajuana na wa jinsia moja tu.
Hata akute jina jipya kwa contacts, inakuwa tabu, maswali lukuki.
Inakera na kuumiza hasa pale unapojitahidi kuwa mwaminifu na kuacha yote yanaweza kumtia mashaka mwenza wako.
Nashauri, deal na simu yako kutokana na nature na mwenza uliyenae.
Ingawa hiyo isichukuliwe kama fimbo ya kufanya maovu.
 
Bado sioni sababu ya kuficha ficha simu kama kweli huna cha kuficha.

Ukiwa mwaminifu kweli basi hutaona shida ya kuwa muwazi kwa mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutaona shida ya kujibu maswali ya mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutakuwa na sababu ya kumficha mwenzako simu yako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutapatwa na ugonjwa wa moyo mwenzako akiishika simu yako.

Kwa hiyo hakuna kilicho kigumu hapo kama kweli upo mkweli.
 
My phone is my phones...
My partner is my partner...
There is no any interaction btn my phone and my partner

So kila kimoja kikae kivyakeee, vikiingiliana tabu na matatizo huanzaaa

wewe wa ajabu kweli. matatizo yanaanzaje? unajua siri za kichwa cha mtu na mienendo yake mara nyingi utazigundua kupitia simu. inaonesha wewe mienendo yako ina walakini ndo maana matatizo huanza. iweje simu kijifaa kidogo tu ukilinganishe na mtu
 
Bado sioni sababu ya kuficha ficha simu kama kweli huna cha kuficha.

Ukiwa mwaminifu kweli basi hutaona shida ya kuwa muwazi kwa mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutaona shida ya kujibu maswali ya mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutakuwa na sababu ya kumficha mwenzako simu yako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutapatwa na ugonjwa wa moyo mwenzako akiishika simu yako.

Kwa hiyo hakuna kilicho kigumu hapo kama kweli upo mkweli.

umenena sana.
 
unachosema ni kweli ila pia inategemea na mwenza uliyenae.
Kuna wenza wengine wana-gubu. Hataki hata uwe na namba ya jinsia nyengine, utadhani wewe wajuana na wa jinsia moja tu.
Hata akute jina jipya kwa contacts, inakuwa tabu, maswali lukuki.
Inakera na kuumiza hasa pale unapojitahidi kuwa mwaminifu na kuacha yote yanaweza kumtia mashaka mwenza wako.
Nashauri, deal na simu yako kutokana na nature na mwenza uliyenae.
Ingawa hiyo isichukuliwe kama fimbo ya kufanya maovu.

inategemea unainteract vipi na hiyo jinsia nyingine. yeye kukukataza bila sababu
 
Siyo hivo! Mfano Mimi nafichaficha sm staki mwenzangu aone mambo ninayofanya(siyo mabaya)na hii ni kutokana na akili take akiona kitu kidogo anapanic ka nini! Sasa kuepusha kuvuruga mahusiano pasipo sababu ya maana bora asiguse

unafiki mtupu. unamnafikia mwenzio
 
big up!!!!!!!!!!!!

nyie mna chembe chembe za uchepukaji ndio maana mnasapotiana. mngelifikiria kabla kwamba mapartner watawabana na msiwe nao ili muwe huru na simu zenu na mawasiliano yenu ya vificho.
 
Kweli kabisaaaa.. mimi nligombana na my ex kwa sababu ya hilo swala la kuchokonoa my phone, so sitaki mtu agusee simu yanguu

SITAKIII NASEMA

wewe una mambo mengi ndio maana
 
unafiki mtupu. unamnafikia mwenzio

Sio unafiki wala si mambo ya mchepuko! Kuna baadhi ya vitu mtu anapenda kufanya ambavyo havihusiani na uchepukaji au unafiki kama unavyodai! Mfano unachati na friends lakn katika kuchati kuna maneno ambayo mwenzako akiyaona tayari anasema "sio mwaminifu" anaumie bure kwa kitu kisichokuwepo!
Mi Nina study 2 ambazo zilishanikuta! Kifupi mwanamke haamini kama mume anaweza kuwa na friends Wa kike half wasiwe michepuko! Na kinyume chake
 
nyie mna chembe chembe za uchepukaji ndio maana mnasapotiana. mngelifikiria kabla kwamba mapartner watawabana na msiwe nao ili muwe huru na simu zenu na mawasiliano yenu ya vificho.

Mrs j hebu angalia mfano SMS hii waliyokuwa wana chat Mr j na lady mwingine na wala hawana mahusiano yoyote ya kingono halaf uniambie utafanyaje unaikuta kwenye simu ya mmeo Mr j.

Mr j:" bado wangu! Je wewe!?
Lady: du mi nshafika mida na tayari nimeshatoa cha mbavu kwa bosi!

Mr j: hahahahah jamaa ni noma! Hakuachi ukapumzika!?
Lady: wewe acha kabisa! Yuko fasta.kwani mama j yeye ukufika anakukodolea mimacho tu?

Mr jaaaaaa mi mpaka night Kali! Nikifika napumzika kidogo!
Lady :" mungu wangu ! Huyu mama hakufundwa eti ! Yaani anamwachia mzee mzuri kama wewe hata haonji?

Naomba jibu
Mr j hahahahah
 
Mke wangu wa ndoa, ana uhuru 100%kushika simu yangu na kufanya atakacho. Siwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba then nishindwe Kula au kunywa kisa simu, nope!

Wengi sio waamimifu katika mahusiano yao, sio rahisi wao kuruhusu mtu kushika simu ya mwenzake, ukikosa uaminifu na heshima kwa mwenzako kuna mengi utaficha, sio simu tu...
 
wewe ni tatizo. uwe single basi upate uhuru wote. sio unakuwa na mtoto wa watu then unakukuruka na apps, mara delete, mara simu extra ya kuficha. shida zote hizo za kuficha za nini na kuwa mtu kumbe huwa huridhiki na mmoja ya nini. watu waficha simu ni vicheche tu. hamna cha zaidi cha kumficha mwenza zaidi ya huo uchafu

Kwa hiyo wewe kwa akili yako unaamini mwanaume ambae hafichi simu huyo hachepuki eh..? Kalaghabaho.. simu utaachiwa wewe ukae nayo na watu wanachepuka kama kawaida. Hakuna binadamu asie na siri.. wewe mwenyewe hapo una siri zako ambazo mumeo hazijui hata kama huzifichi kwenye simu umezificha moyoni..!
 
Tell them tell them, aise umenigusa wewe Thechoji, sio siri mpaka mwili ukanisisimuka walahi!!!:wink1::clap2:
 
Kwa nini wewe mwanandoa ufiche fiche simu yako na kukataza partner wako asiwe na uhuru nayo kama hakuna uchafu tena mkubwa unaoficha na unaona ni haki yako kuuendeleza ili michepuko ione iko huru na unaijali zaidi na huyo mwenzio si chochote cha kukuzuia. Ole

Usalama wa taifa nao wawe wanaziachacha tu simu zao?
 
Bado sioni sababu ya kuficha ficha simu kama kweli huna cha kuficha.

Ukiwa mwaminifu kweli basi hutaona shida ya kuwa muwazi kwa mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutaona shida ya kujibu maswali ya mwenzako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutakuwa na sababu ya kumficha mwenzako simu yako.

Ukiwa mwaminifu kweli hutapatwa na ugonjwa wa moyo mwenzako akiishika simu yako.

Kwa hiyo hakuna kilicho kigumu hapo kama kweli upo mkweli.
Binadamu hachungwi kwa simu na kuwa muwazi katika simu it doesnt mean kuwa kila kitu kipo sawa.Watu zatumika simu za ofisini tu. ya mkononi haiguswi.
 
Mke wangu wa ndoa, ana uhuru 100%kushika simu yangu na kufanya atakacho. Siwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba then nishindwe Kula au kunywa kisa simu, nope!

Wengi sio waamimifu katika mahusiano yao, sio rahisi wao kuruhusu mtu kushika simu ya mwenzake, ukikosa uaminifu na heshima kwa mwenzako kuna mengi utaficha, sio simu tu...

Ana uhuru wa kushika simu yako kwa vile anakuwa ana mahitaji ya kuishika ikiwemo kupiga kama simu yake haina salio au una mruhusu ashike kumthibitishia kuwa upo perfect?
 
Binadamu hachungwi kwa simu na kuwa muwazi katika simu it doesnt mean kuwa kila kitu kipo sawa.Watu zatumika simu za ofisini tu. ya mkononi haiguswi.

swali ni kuwa kwa nini umzuie kushika kama huna jambo linaendelea? hata ukitumia ya ofisi kufanya yasiyofaa ni unafiki.
 
Tell them tell them, aise umenigusa wewe Thechoji, sio siri mpaka mwili ukanisisimuka walahi!!!:wink1::clap2:

hakuna partner anaempenda mwenzake akawa na siri moyoni. ukiwa na siri moyoni una walakini wewe. swala ni kwa nini ufiche simu, usianze kujihisi tu kwamba mwenzio akigusa simu yako anakuspy au unajihisi hisi bila sababu kama kweli hiyo sababu huna
 
Sio unafiki wala si mambo ya mchepuko! Kuna baadhi ya vitu mtu anapenda kufanya ambavyo havihusiani na uchepukaji au unafiki kama unavyodai! Mfano unachati na friends lakn katika kuchati kuna maneno ambayo mwenzako akiyaona tayari anasema "sio mwaminifu" anaumie bure kwa kitu kisichokuwepo!
Mi Nina study 2 ambazo zilishanikuta! Kifupi mwanamke haamini kama mume anaweza kuwa na friends Wa kike half wasiwe michepuko! Na kinyume chake

kumbe nia yako uwe na friends wa kike...yale yale. utani wa ajabu ajabu wa nini? ndio huo huo unaolead to hayo hayo matani kuwa kweli. huna nia njema wewe. na ninaamini mwenzio hakuwa mjinga kukumaindi kwenye case zote mbili
 
Back
Top Bottom