Umeona sasa?Hebu rudi kwenye post zako za nyuma mzee. Wewe mwenyewe ndiye uliyeleta hoja ya Spiderman ukisema kama Muumba ulimwengu ni fact kwasababu Biblia imeandika, basi Spider-Man is real because there's also a book about him.
Kitendo cha wewe kutumia Biblia kama kipimo cha kuthibitisha uwepo wa Mungu, ndicho kilichonifanya nikuonyeshe kuwa dhana ya Mungu haitegemei Biblia kama chanzo chake, ipo nje ya hapo!
Sasa kama ulikuwa unajua tangu mwanzo kuwa hiyo dhana haikutokana na Biblia, mfano wako wa Spiderman na vitabu ulikuwa unafanya nini hapa kama sio kupoteza muda wa uzi? Umeona hoja yako imefeli sasa hivi unaanza kurudi nyuma kinyamela!
Kwa mfano wewe ukiniambia kitu fulani ni scientific fact, mimi nathibitishaje kujua kama hicho kitu kweli ni fact?Mimi ndio nimeleta mfano wa kisayansi kwa sababu facts zake ni ukweli unaoonekana unaounga mkono hoja yangu ya uwepo wa Muumba. Wewe badala ya kuleta hoja mbadala kupinga hizo facts, unaleta vitisho vya kisiasa eti kwa nini nachagua baadhi ya maeneo?
Sayansi yenyewe imejengwa juu ya kuchagua na kuchuja. Kama una hoja ya kisayansi inayothibitisha ulimwengu hauna mwanzo au haufuati sheria yoyote, ilete hapa mezani tuichambue. Acha kulialia kuhusu nani kaanzisha mada ya sayansi!
Ulimwengu upi?Katika falsafa, huo ulimwengu wako ulioupa uwezo wa kujiumba na kujipangia sheria bila kuwa na chanzo cha nje, ndio unaosadifu sifa za Mungu tunayemzungumzia.
Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe unajiita hujui kwa sababu pengine unaogopa tu kumtaja Mungu Mkuu, lakini kiuhalisia umeshakubali uwepo wa hiyo nguvu kuu! Umeelewa mzee?
Soma reply yako niliyo kujibu kwa kutumia hiyo reply utaelewa.Ulimwengu upi?
Umeandika ulioupa uwezo.Soma reply yako niliyo kujibu kwa kutumia hiyo reply utaelewa.