Kwa nini Mungu alimuumba binadamu?

Kwa nini Mungu alimuumba binadamu?

Dhana ya uwepo wa Muumba haikutokana na Biblia wala Quran, ilianza kama hoja ya kifalsafa na kisayansi hata kabla ya vitabu vya dini kuandikwa, ni wazi hili hukuwa ukilijua kabisa.

Mantiki yake iko hivi, imwengu una mwanzo hata sayansi kupitia Big Bang Theory inakubali hili, na chochote chenye mwanzo kimesababishwa na kitu kingine kilicho nje yake.

Hauwezi kuwa na ulimwengu tata wenye laws of physics bila kuwa na uncaused cause, biblia au Quran hazikuunda dhana ya Mungu, bali zimeelezea tu na kumpa sifa Muumba ambaye uwepo wake unathibitishwa na ulimwengu wenyewe.

Spiderman hana uhusiano na asili ya ulimwengu, yeye ni tabia tu ndani ya kitabu. Mungu ndiye aliyesababisha hata huyo mwandishi wa spiderman awepo.
Nikisema dhana ya Mungu kuumba ulimwengu imeandikwa kwenye Biblia, sina maana kuwa Biblia ndio primary source iliyoanzisha dhana hiyo.

Ndio maana post za awali nilikuambia hata hiyo Biblia imechukua hizo habari kutoka kwenye dini za kale za Kihindu.

Sasa kama kitabu kimeandika habari hiyo ni dhana rahisi tu kufikiria kuwa wazo hilo lilianzia nje ya vitabu na kuja kuwekwa katika maandishi baadaye.
 
Kama unaikubali Sayansi basi ikubali yote pamoja na misingi yake, hautakiwi kuchagua tu baadhi ya maeneo ambayo yanakuridhisha kwasababu yanaenda sawa na narrative zako.

Ili baadaye na mimi napokuoneshea mifano au hoja za kisayansi uwe unazikubali kwasababu ni za kisayansi.

So, nakuuliza.

Unaikubali Sayansi na majibu yake yanapaswa kuaminika au taarifa zake zinapaswa kuchukuliwa kama habari sahihi?

Kama jibu ni hapana, basi sioni sababu ya wewe kuja na hoja na mifano ya kisayansi ya kunishawishi wakati hata wewe kuna maeneo hukubaliani na Sayansi.
 
kwahiyo hata kama wazo lilianzia nje ya vitabu, point yako hasa ni nini? 😂

Mbona unaandika kichekesho hivi.
 
Unajichosha bure kwa kujaribu kunitengenezea miiko ya vijiweni 😂

Ngoja nikuulize swali la kitoto, ukisoma ripoti ya daktari inayosema una Group A ya damu halafu daktari huyo huyo akakwambia nadhani ukila ndizi utakuwa mrefu, lazima ukubali na hiyo hoja yake nyingine ya ndizi kisa tu aliyeongea yeye ni daktari?
 
Sasa kama haikua necessary kutuumba ila alitaka kudhihirisha tu uwezo wake si ndio show off hiyo
Hapa sasa unalazimisha kuweka tabia za kishamba za binadamu kwa Mungu! 😂

Mungu anatafuta kibali au sifa kutoka kwa nani? Kwani alikuwa anajionyesha kwa miungu wenzake au jirani zake?
 
Mungu ni mmoja tu ?
 
kwahiyo hata kama wazo lilianzia nje ya vitabu, point yako hasa ni nini? 😂

Mbona unaandika kichekesho hivi.
Hoja ni kwamba hakuna sehemu nimehusisha Biblia kama chanzo cha kwanza kuhusu dhana ya Mungu na uumbaji ulimwengu.

Vinginevyo labda kama ulikuwa hujui ulichoandika kusema

"Dhana ya uwepo wa Muumba haikutokana na Biblia wala Quran, ilianza kama hoja ya kifalsafa na kisayansi hata kabla ya vitabu vya dini kuandikwa, ni wazi hili hukuwa ukilijua kabisa."
 
Kwa wale wanaoamini mungu yupo na ndiye ameumba ulimwengu, kwa nini aliuumba ulimwengu pamoja na viumbe hai ?

Kwa nini hasa mungu alimuumba binadamu ?
Kwanini wewe unanunua kiwanja, unajenga nyumba, unafuga kuku, ng'ombe na kitimoto (ahahahahaha, kitimoto), unasomesha watoto na kuwa na hawara?
 
Eeh swali hili n gumu kweli bana 😅 Mimi naona kama Mungu alimuumba binadamu kwa ajili ya mtihani tu... maisha haya yote ni kama shule, unafanya mitihani mpaka ufaulu au usifaulu. Lakini pia kuna wale wanaosema tumeumbwa tu kwa bahati, maana yake hakuna kusudi lolote. Wewe unaamini nini mkuu? Kweli kuna kusudi au tu bahati mbaya?
 
Unajichosha bure kwa kujaribu kunitengenezea miiko ya vijiweni 😂

Ngoja nikuulize swali la kitoto, ukisoma ripoti ya daktari inayosema una Group A ya damu halafu daktari huyo huyo akakwambia nadhani ukila ndizi utakuwa mrefu, lazima ukubali na hiyo hoja yake nyingine ya ndizi kisa tu aliyeongea yeye ni daktari?
Sio mimi niliyeleta mambo ya Sayansi kwenye huu mjadala.

Ni wewe ndio umeanzisha hilo jambo.

Sasa kama hutaki ku-opt Sayansi kama chanzo sahihi kutumika kwenye mjadala, then kwanini nishawishike na zile hoja zako zenye madai ya kisayansi?

Hapo ni sawa na kusema dagaa huli ila unakula mchuzi wake.
 
Hoja ni kwamba hakuna sehemu nimehusisha Biblia kama chanzo cha kwanza kuhusu dhana ya Mungu na uumbaji ulimwengu.

Vinginevyo labda kama ulikuwa hujui ulichoandika kusema

"Dhana ya uwepo wa Muumba haikutokana na Biblia wala Quran, ilianza kama hoja ya kifalsafa na kisayansi hata kabla ya vitabu vya dini kuandikwa, ni wazi hili hukuwa ukilijua kabisa."
Hebu rudi kwenye post zako za nyuma mzee. Wewe mwenyewe ndiye uliyeleta hoja ya Spiderman ukisema kama Muumba ulimwengu ni fact kwasababu Biblia imeandika, basi Spider-Man is real because there's also a book about him.

Kitendo cha wewe kutumia Biblia kama kipimo cha kuthibitisha uwepo wa Mungu, ndicho kilichonifanya nikuonyeshe kuwa dhana ya Mungu haitegemei Biblia kama chanzo chake, ipo nje ya hapo!

Sasa kama ulikuwa unajua tangu mwanzo kuwa hiyo dhana haikutokana na Biblia, mfano wako wa Spiderman na vitabu ulikuwa unafanya nini hapa kama sio kupoteza muda wa uzi? Umeona hoja yako imefeli sasa hivi unaanza kurudi nyuma kinyamela!
 
Sio mimi niliyeleta mambo ya Sayansi kwenye huu mjadala.

Ni wewe ndio umeanzisha hilo jambo.

Sasa kama hutaki ku-opt Sayansi kama chanzo sahihi kutumika kwenye mjadala, then kwanini nishawishike na zile hoja zako zenye madai ya kisayansi?

Hapo ni sawa na kusema dagaa huli ila unakula mchuzi wake.
Mimi ndio nimeleta mfano wa kisayansi kwa sababu facts zake ni ukweli unaoonekana unaounga mkono hoja yangu ya uwepo wa Muumba. Wewe badala ya kuleta hoja mbadala kupinga hizo facts, unaleta vitisho vya kisiasa eti kwa nini nachagua baadhi ya maeneo?

Sayansi yenyewe imejengwa juu ya kuchagua na kuchuja. Kama una hoja ya kisayansi inayothibitisha ulimwengu hauna mwanzo au haufuati sheria yoyote, ilete hapa mezani tuichambue. Acha kulialia kuhusu nani kaanzisha mada ya sayansi!
 
Jibu ni rahisi tu, HATUJUI.

Hiyo mifano tata ya kisheria si lazima utata wake umaanishe Mungu, vipi kama ni ulimwengu wenyewe ndio ume create hizo pattern ila tumeangukia kwenye majibu potofu ya Mungu kwasababu tumeshindwa ku crack hiyo code kwasababu ya utata wake.

Kwanini usifikirie kuwa, hiyo dhana ya utata uliyoitaja ambayo haiko wazi kwasababu ya utata wake, inaweza kukufanya uwe karibu zaidi kuangukia kwenye majibu potofu (Mungu) ambayo wewe una confidence nayo kuwa ni sahihi?
Katika falsafa, huo ulimwengu wako ulioupa uwezo wa kujiumba na kujipangia sheria bila kuwa na chanzo cha nje, ndio unaosadifu sifa za Mungu tunayemzungumzia.

Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe unajiita hujui kwa sababu pengine unaogopa tu kumtaja Mungu Mkuu, lakini kiuhalisia umeshakubali uwepo wa hiyo nguvu kuu! Umeelewa mzee?
 
Back
Top Bottom