Kwa nini maandamano October 29 yalifeli?

KWA NINI MAANDAMANO OCTOBER 29 YALIFELI?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kwanza nitoe pole kwa yote yaliyotokea. Waliathiriwa na kuathirika kwa kuuawa, kujeruhiwa na kuharibiwa biashara zao.

2. Niliandika uzi kueleza namna gani maandamano ya October 29 yatakavyofeli. Sikuandika kwamba hayatofanyika. Hivyo wale mnaoninukuu basi wekeni kumbukumbu zenu sahihi.

3. Kimsingi nilijua maandamano ya October 29 yasingezidi masaa sita. Na ndivyo ilivyokuwa. Kama mtakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa maandamano yatafeli(kumaanisha yatakuwepo ila hayatafanikiwa) na yakijitahid basi hayazidi masaa sita.

4. Hapa nitaandika kama mchambuzi. So wasomaji kazi yenu ni kusoma. Sitawaamulia namna ya kufikiri, kuelewa, kupokea na kutoa maoni yenu.

5. Nitaeleza kwa nini maandamano ya October 29 yalifeli sio kwa sababu ya kusikia au kuhadithiwa au kuota bali nikiwa shahidi na shuhuda kwa kilichotokea.

6. Sitampendelea mtu wala sitamuonea Mtu. Nitaeleza kichambuzi. Sehemu ya makosa ya waandamanaji nitasema, sehemu ya makosa ya Askari pia nitasema.

7. Hoja za kufeli maandamano nilishazitoa kabla ya maandamano. Lakini hoja chache ndizo zilizojitokeza na kuyafanya yasifanikiwe kwa ground.

8. Hoja ni kama ifuatavyo;
a) Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwa Waandamanaji.
Hii hoja niliitaja kabla ya maandamano na nilisema itakuwa moja ya hoja zitakazofelisha maandamano.

Siku ya maandamano waandamanaji walikuwa na maslahi na malengo yaliyopishana na kukinzana.
I) Wapo waliokuwa wanataka reforms na mabadiliko ya kweli ya nchi. Hawa walikuwepo. Na niliwasikia.

ii) Wapo waliokuwa wanahitaji Kumtoa Rais Samia suluhu Ikulu. Hawa mpango wao ulikuwa kufika Ikulu na kumng'oa Rais. Walikuwa wakiimba hivyo na kusema na walikuwa wanahakika mpaka usiku wangekuwa wamefika Ikulu.

iii) Wapo ambao walikuwa wanahitaji Watu waliotekwa na kupotezwa.

iv) Wapo ambao walikuwa wanaandamana kama mchezo fulani hivi wa maonyesho. Unaweza kushangaa lakini watu hao walikuwepo. Na niliwaona.

v) Wapo ambao walikuwa na matatizo mengi ambayo hayaelezeki. Hawa walikuwa wakilia tuu. Waliiona huenda siku hiyo ingekuwa siku ya mabadiliko ya matatizo yao.

vi) Wapo ambao kwao hiyo ilikuwa fursa ya kufanya Uhalifu kwa kuvunja na kuiba mali za watu. Watu hao walikuwepo.

Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwenye maandamano kuliyafanya yadhibitiwe.

Nilieleza hapa kwenye uzi wangu wa MY SIDE: matukio ya uhalifu yalifanya waandamanaji kugawanyika na kupungua wengine wakarudi nyumbani. Siongei kukisia au kutunga kama zile riwaya zangu. Hapa nazungumzia kilichotokea.

b) Ukosefu wa Uongozi wakati wa maandamano.
Watu wengi wenye malengo hasa ya kiharakati na kutaka mabadiliko bila kiongozi ni ngumu sana kufanikiwa.

I) Yalifeli kwa sababu hakukuwa na chain of command. Hapakuwa na kiongozi wa kutoa maelekezo na kufuatwa.
Hapakuwa na good organization wakati wa maandamano.
Kila mtu alijifanyia anavyojua. Wengine waliimba, wengine walirekodi, wengine walirusha mawe, wengine walichoma moto, wengine walikuwa wanavamia.

ii) mara kadhaa kulikuwa na mabishano baina ya waandamanaji. Wengine wakisema tufanye hivi wengine hapana jamani tusifanye. Wengine wakikataza uharibifu wengine wakishadadia uhalifu na wengine wakifanya.

iii) Kila barabara ya waandamanaji ingepata viongozi huenda mambo yangeenda vizuri. Na viongozi wapatikane siku ya tukio.

iv) ukosefu wa viongozi tafsiri yake ni kushindwa kufanikisha malengo ya maandamano bila kujali kama yalikuwa na nia njema au mbaya.

c) Kundi la Wahalifu liliharibu muelekeo wa maandamano na kuyafanya yafeli kwa haraka.

i) Niliandika maandamano yalianza kidogo kidogo saa tatu kuelekea saa nne.
ii) Mpaka saa nne na nusu maandamano yalikuwa hayana uhalifu na fujo zile za kutisha. Hata Jeshi la Wananchi JW lilikuwa linalinda raia.
Kwa ambao hamkuwepo hata nyie mliona kwenye video ambazo zimepostiwa mitandaoni.

iii) Wahalifu hasa Wezi na wachoma vituo vya mwendokasi, vituo vya mafuta, vituo vya kuhesabia kura n.k. hawa ndio walibadilisha upepo wa tukio zima.
Hayo yalianza saa tano kuelekea saa sita ambapo yalidumu kwa takribani masaa matatu. Kwa kukata kata. Yaani sio ile non stop.

iv) Hivyo kulikuwa na wahalifu wa maslahi yao binafsi yaani kuiba vitu. Lakini kulikuwa na wahalifu wa kutaka kukomoa serikali na watu fulani hawa ndio walichoma vituo vya mwendo kasi na wengine nyumba za ccm, na watu kadhaa mashuhuri.

9. Askari na Polisi nao hawawezi kukwepa Lawama katika tukio hili.

10. Wao ndio wamesomea kazi hiyo na wanaowajibu wa kulinda watu na mali zao.

11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu.

13. Kama walivyofanya JW wakati wa asubuhi kusaidia waandamanaji waandamane ila kwa usalama bila kuumizana, kuharibu mali na kuleta vurugu hata polisi nao wangeweza kufanya hivyo.

14. Hapakuwa na sababu ya kuuana kwa kiwango kile kama hatua sahihi tangu dakika za awali zingefanyika.

15. Polisi wamekosea pakubwa kutumia nguvu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi.

16. Viongozi wa serikali, vyombo vya dola vinapaswa kujua kuwa saikolojia ya Wananchi ni tofauti na saikolojia ya Polisi au Maaskari.

17. Niligundua pia moja ya madhara Makubwa yamesababishwa na tatizo la tofauti za kisaikolojia baina ya Askari na wananchi.

18. Askari na vyombo vya dola wao saikolojia yao inaongozwa kwa kufuata Amri ya mkubwa bila kujali uhalali wake.
Ila saikolojia ya wananchi au raia hawaongozwi na kwa kufuata amri bila maelezo. Utawala wa kiraia unajenga saikolojia ya kuhoji, kutoa maoni na ikiwezekana kupinga ikiwa amri sio halali.
Hao ni wananchi.

19. Hivyo Polisi anavyomchukulia Rais Samia ni tofauti na raia wa kawaida anavyomchukulia Rais Aamua.
Polisi humchukulia Rais kama Boss wake, mkuu wa kazi na Amir jeshi Mkuu.
Wakati mwananchi humchukulia Rais kama kiongozi aliyemchagua ambaye anamlipa pesa kupitia kodi asimamie rasilimali za nchi ikiwemo watu(yeye)

20. Raia haoni shida kumkosoa Rais au kiongozi yeyote wa nchi kwa sababu kisaikolojia mwananchi anajua yeye ndiye amemuweka pale.
Wakati Polisi Rais akikohoa tuu kidogo atafanya tuu bila kuuliza bila kusita.

21. Polisi, vyombo vya dola ni muhimu kuelewa kuwa mazingira yenu ya kazi hayahusiani na mazingira ya wananchi wengine ambao sio Polisi.
Utawala wa kiraia hasa kwa nchi yenye demokrasia kama yetu ni tofauti na utawala wa kijeshi wa kupokea amri tuu.

22. Lazima tuelewe kuwa Kama Polisi na vyombo vya dola vitaleta mambo yao ya kijeshi kwa raia wananchi wengi watazidi kuumia sana kwani jeshini ndio hakuna ukosoaji, hasa kumkosoa na kumpinga kiongozi aliye juu yako.

23. Rais Samia kama kiongozi wa nchi pia ni muhimu kuelewa kuwa yeye ni Amir jeshi lakini hatakiwi kutumia kanuni za jeshi kwa wananchi wa kawaida.

24. Ili kuondoa mgongano kati ya utawala wa kijeshi na utawala wa kiraia ni vizuri utulivu, hekima, utu na uzalendo vitangulizwe mbele.

25. Kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unaposema watu wasiandamane kwa kutumia koti la kijeshi ni kuleta maumivu, mauaji na majeraha kwani lazima wapo wananchi ambao wao hawakusikilizi kama Amri jeshi mkuu bali wanakusikiliza kama raia mwenye cheo cha urais.

26. Sasa Amir jeshi umesema watu wasiandamane. Watu wakafanya hivyo. Automatically utaona wanakudharau jambo ambalo sio lazima liwe kweli.
Sio kwamba wanakudharau nope! Wao wanaona ni haki yao kuandamana na kudai wanachodai. Na wao saikolojia yao wanaamini nchi yao ni ya kidemokrasia

27. Hasira za polisi au vyombo vya dola kufikiri vimedharauliwa na hasira zisizo halali kabisa kwani hakuna wananchi wanaodharau askari wao, jeshi lao, au vyombo vya dola;

28. Isipokuwa Polisi na vyombo vya dola wanataka kutumia kanuni za kijeshi kwa wananchi wanaoamini utawala wa kidemokrasia.
Kutokuelewana huko ndio kunatokeaga mvurugano.

29. Sio tuu katika sakata hilo lililopita. Hata katika masakata mengine.
Zipo hadithi Unakuta baadhi ya wanajeshi wanataka kuishi mtaani kama wanajeshi kwa kutumia falsafa za kijeshi mtaani jambo ambalo wakati mwingine inaripotiwa ikileta shida. Kwamba Mjeshi au Askari anataka ukiongea naye uwe kama unaongea sijui na nani jambo ambalo sio sahihi kabisa.

30. Nikielekea kumaliza, Vyombo vya dola, askari polisi na wengine tukio kama hili lisijirudie. Tunapofanya kazi tusifanye kuonyeshana umwamba, kukomoana, hayo sio maadili ya kazi. Hivyo kilichofanyika hata kama ni kudhibiti uhalifu ulikuwa na ukatili na unyama uliopitiliza.

31. Hii inaweza kuleta matokeo mabaya na kuleta chuki na dhana potofu kuhusu kazi ya uaskari ambayo mimi kama Mtibeli naamini na kujua ni moja ya kazi njema na nzuri katika maisha ya viumbe. Kumbuka hata malaika wa mbinguni ni Askari na wanajeshi.
So ni muhimu kila askari kutafakari na kufanya wajibu wake. Ili kuifanya kazi ya uaskari iheshimiwe na mtu akipita asione aibu kujitambulisha kwa watu kubwa yeye ni Askari Polisi.

32. Mwisho, hakuna namna sahihi ya watu kudai haki zao zaidi ya maandamano. Kuzuia maandamano ni kutengeneza ufa mkubwa wa watu kutafuta njia nyingine ngumu zaidi ambazo sio salama kwa taifa.

33. Ni muhimu maandamano yapewe ulinzi na askari ili kupunguza madhara.
Lazima ijulikane kuna watu wanamadai yao. Ni muhimu kuyasikiliza ili tuende pamoja. Tusiende mbali tukawaacha wengine nyuma wakinung'unika.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster.
Kwa sasa Dar es salaa

Walikuwa wakiimba jeshi 😁😁😁propaganda za Mengi zakijinga Sana ile wanadandia gari la jeshi ahaaa .

😁😁

RIP my buddies wote
 
Uzi wowote ambao nikiona tu mwandishi anaanza kwa maneno ya self defense (kutengeneza backup ya kumlinda) najua hapo hamna kitu zaidi ya bias na uzugaji.

Unaposema maandamano hayakuzidi masaa 6, ulitakiwa utuambie hii umeitoa kwa mujibu wa tafiti gani?

Au lah utuambie fact yako imezingatia muktadha wa eneo dogo ambalo wewe ulikuwepo kwenye hiyo siku.

Lakini ku generalize kusema maandamano hayakuzidi masaa 6, huo ni uongo pure.
Na mimi ndio nimeishia hapo sijaendelea uzi mzima umekua null and void ab initio
 
Maandamano hayakuzidi masaa sita.
Yalikuwa yanatokea na kupotea na yakitokea hayamalizi haya dakika 10 -20 wanatawanyika kunakuwa peupe.

Nakuhakikishia ukijumlisha Masaa ya nchi nzima hayawezi kuzidi masaa sita.

Ila doria ndio ilikuwa ya siku sita mpaka saba.

Niambie eneo gani Dar maandamano yalidumu walau lisaa limoja non stop?

Sio kwamba nadogodesha kilichofanywa na waandamanaji bali nazungumzia kilichotokea.

Wanaandamana labda kutoka Ubungo kuelekea shekilango. Kabla hawajafika ndani ya dakika 10 wanatawanywa kuna kunatulia. Wanafanya hivyo labda mara nne kisha panakuwa kimya moja kwa moja.

Barabara zilikuwa hazina vizuizi magari ya polisi yakitoka huko yanakotoka ndani ya dakika mbili njia zote zinakuwa nyeupe watu wamekimbia.

Pengine vingekuwepo vizuizi barabarani yangedumu kwa masaa mengi zaidi kama sio siku nzima
Hizo data naona unazitoa straight out of your makalio deep inside 🤮💩
 
Shots za maneno yako mwenyewe, sijui mnaandika vitu ili mfaidike nini, hasa vitu vinavyogusa maisha ya watu.
View attachment 3500385View attachment 3500386
Mnatakiwa kuwa makini, hasa nyie mnaopenda kuandika makala, you're provoking people, mkitukanwa mnaona kuonewa!! Kumbukeni damu zimemwagika.
Ni muongo. Anataka kusema hakusema maandamano hayatafanyika. He said it.
 
Robert amenisikitisha sana, kusema maandamano hayajafanyika au hayajafanikiwa ni kusema hana habari na damu za ndugu zake waliokufa kwa risasi za moto toka kwa madhalimu.

Yawe organised, yawe disorganised lakini yalifanyika, matokeo wote tumeyaona, watawala wameyaona, mafisadi na hata chawa wameyaona. Kila mtu ana la kujifunza.
 
KWA NINI MAANDAMANO OCTOBER 29 YALIFELI?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kwanza nitoe pole kwa yote yaliyotokea. Waliathiriwa na kuathirika kwa kuuawa, kujeruhiwa na kuharibiwa biashara zao.

2. Niliandika uzi kueleza namna gani maandamano ya October 29 yatakavyofeli. Sikuandika kwamba hayatofanyika. Hivyo wale mnaoninukuu basi wekeni kumbukumbu zenu sahihi.

3. Kimsingi nilijua maandamano ya October 29 yasingezidi masaa sita. Na ndivyo ilivyokuwa. Kama mtakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa maandamano yatafeli(kumaanisha yatakuwepo ila hayatafanikiwa) na yakijitahid basi hayazidi masaa sita.

4. Hapa nitaandika kama mchambuzi. So wasomaji kazi yenu ni kusoma. Sitawaamulia namna ya kufikiri, kuelewa, kupokea na kutoa maoni yenu.

5. Nitaeleza kwa nini maandamano ya October 29 yalifeli sio kwa sababu ya kusikia au kuhadithiwa au kuota bali nikiwa shahidi na shuhuda kwa kilichotokea.

6. Sitampendelea mtu wala sitamuonea Mtu. Nitaeleza kichambuzi. Sehemu ya makosa ya waandamanaji nitasema, sehemu ya makosa ya Askari pia nitasema.

7. Hoja za kufeli maandamano nilishazitoa kabla ya maandamano. Lakini hoja chache ndizo zilizojitokeza na kuyafanya yasifanikiwe kwa ground.

8. Hoja ni kama ifuatavyo;
a) Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwa Waandamanaji.
Hii hoja niliitaja kabla ya maandamano na nilisema itakuwa moja ya hoja zitakazofelisha maandamano.

Siku ya maandamano waandamanaji walikuwa na maslahi na malengo yaliyopishana na kukinzana.
I) Wapo waliokuwa wanataka reforms na mabadiliko ya kweli ya nchi. Hawa walikuwepo. Na niliwasikia.

ii) Wapo waliokuwa wanahitaji Kumtoa Rais Samia suluhu Ikulu. Hawa mpango wao ulikuwa kufika Ikulu na kumng'oa Rais. Walikuwa wakiimba hivyo na kusema na walikuwa wanahakika mpaka usiku wangekuwa wamefika Ikulu.

iii) Wapo ambao walikuwa wanahitaji Watu waliotekwa na kupotezwa.

iv) Wapo ambao walikuwa wanaandamana kama mchezo fulani hivi wa maonyesho. Unaweza kushangaa lakini watu hao walikuwepo. Na niliwaona.

v) Wapo ambao walikuwa na matatizo mengi ambayo hayaelezeki. Hawa walikuwa wakilia tuu. Waliiona huenda siku hiyo ingekuwa siku ya mabadiliko ya matatizo yao.

vi) Wapo ambao kwao hiyo ilikuwa fursa ya kufanya Uhalifu kwa kuvunja na kuiba mali za watu. Watu hao walikuwepo.

Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwenye maandamano kuliyafanya yadhibitiwe.

Nilieleza hapa kwenye uzi wangu wa MY SIDE: matukio ya uhalifu yalifanya waandamanaji kugawanyika na kupungua wengine wakarudi nyumbani. Siongei kukisia au kutunga kama zile riwaya zangu. Hapa nazungumzia kilichotokea.

b) Ukosefu wa Uongozi wakati wa maandamano.
Watu wengi wenye malengo hasa ya kiharakati na kutaka mabadiliko bila kiongozi ni ngumu sana kufanikiwa.

I) Yalifeli kwa sababu hakukuwa na chain of command. Hapakuwa na kiongozi wa kutoa maelekezo na kufuatwa.
Hapakuwa na good organization wakati wa maandamano.
Kila mtu alijifanyia anavyojua. Wengine waliimba, wengine walirekodi, wengine walirusha mawe, wengine walichoma moto, wengine walikuwa wanavamia.

ii) mara kadhaa kulikuwa na mabishano baina ya waandamanaji. Wengine wakisema tufanye hivi wengine hapana jamani tusifanye. Wengine wakikataza uharibifu wengine wakishadadia uhalifu na wengine wakifanya.

iii) Kila barabara ya waandamanaji ingepata viongozi huenda mambo yangeenda vizuri. Na viongozi wapatikane siku ya tukio.

iv) ukosefu wa viongozi tafsiri yake ni kushindwa kufanikisha malengo ya maandamano bila kujali kama yalikuwa na nia njema au mbaya.

c) Kundi la Wahalifu liliharibu muelekeo wa maandamano na kuyafanya yafeli kwa haraka.

i) Niliandika maandamano yalianza kidogo kidogo saa tatu kuelekea saa nne.
ii) Mpaka saa nne na nusu maandamano yalikuwa hayana uhalifu na fujo zile za kutisha. Hata Jeshi la Wananchi JW lilikuwa linalinda raia.
Kwa ambao hamkuwepo hata nyie mliona kwenye video ambazo zimepostiwa mitandaoni.

iii) Wahalifu hasa Wezi na wachoma vituo vya mwendokasi, vituo vya mafuta, vituo vya kuhesabia kura n.k. hawa ndio walibadilisha upepo wa tukio zima.
Hayo yalianza saa tano kuelekea saa sita ambapo yalidumu kwa takribani masaa matatu. Kwa kukata kata. Yaani sio ile non stop.

iv) Hivyo kulikuwa na wahalifu wa maslahi yao binafsi yaani kuiba vitu. Lakini kulikuwa na wahalifu wa kutaka kukomoa serikali na watu fulani hawa ndio walichoma vituo vya mwendo kasi na wengine nyumba za ccm, na watu kadhaa mashuhuri.

9. Askari na Polisi nao hawawezi kukwepa Lawama katika tukio hili.

10. Wao ndio wamesomea kazi hiyo na wanaowajibu wa kulinda watu na mali zao.

11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu.

13. Kama walivyofanya JW wakati wa asubuhi kusaidia waandamanaji waandamane ila kwa usalama bila kuumizana, kuharibu mali na kuleta vurugu hata polisi nao wangeweza kufanya hivyo.

14. Hapakuwa na sababu ya kuuana kwa kiwango kile kama hatua sahihi tangu dakika za awali zingefanyika.

15. Polisi wamekosea pakubwa kutumia nguvu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi.

16. Viongozi wa serikali, vyombo vya dola vinapaswa kujua kuwa saikolojia ya Wananchi ni tofauti na saikolojia ya Polisi au Maaskari.

17. Niligundua pia moja ya madhara Makubwa yamesababishwa na tatizo la tofauti za kisaikolojia baina ya Askari na wananchi.

18. Askari na vyombo vya dola wao saikolojia yao inaongozwa kwa kufuata Amri ya mkubwa bila kujali uhalali wake.
Ila saikolojia ya wananchi au raia hawaongozwi na kwa kufuata amri bila maelezo. Utawala wa kiraia unajenga saikolojia ya kuhoji, kutoa maoni na ikiwezekana kupinga ikiwa amri sio halali.
Hao ni wananchi.

19. Hivyo Polisi anavyomchukulia Rais Samia ni tofauti na raia wa kawaida anavyomchukulia Rais Aamua.
Polisi humchukulia Rais kama Boss wake, mkuu wa kazi na Amir jeshi Mkuu.
Wakati mwananchi humchukulia Rais kama kiongozi aliyemchagua ambaye anamlipa pesa kupitia kodi asimamie rasilimali za nchi ikiwemo watu(yeye)

20. Raia haoni shida kumkosoa Rais au kiongozi yeyote wa nchi kwa sababu kisaikolojia mwananchi anajua yeye ndiye amemuweka pale.
Wakati Polisi Rais akikohoa tuu kidogo atafanya tuu bila kuuliza bila kusita.

21. Polisi, vyombo vya dola ni muhimu kuelewa kuwa mazingira yenu ya kazi hayahusiani na mazingira ya wananchi wengine ambao sio Polisi.
Utawala wa kiraia hasa kwa nchi yenye demokrasia kama yetu ni tofauti na utawala wa kijeshi wa kupokea amri tuu.

22. Lazima tuelewe kuwa Kama Polisi na vyombo vya dola vitaleta mambo yao ya kijeshi kwa raia wananchi wengi watazidi kuumia sana kwani jeshini ndio hakuna ukosoaji, hasa kumkosoa na kumpinga kiongozi aliye juu yako.

23. Rais Samia kama kiongozi wa nchi pia ni muhimu kuelewa kuwa yeye ni Amir jeshi lakini hatakiwi kutumia kanuni za jeshi kwa wananchi wa kawaida.

24. Ili kuondoa mgongano kati ya utawala wa kijeshi na utawala wa kiraia ni vizuri utulivu, hekima, utu na uzalendo vitangulizwe mbele.

25. Kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unaposema watu wasiandamane kwa kutumia koti la kijeshi ni kuleta maumivu, mauaji na majeraha kwani lazima wapo wananchi ambao wao hawakusikilizi kama Amri jeshi mkuu bali wanakusikiliza kama raia mwenye cheo cha urais.

26. Sasa Amir jeshi umesema watu wasiandamane. Watu wakafanya hivyo. Automatically utaona wanakudharau jambo ambalo sio lazima liwe kweli.
Sio kwamba wanakudharau nope! Wao wanaona ni haki yao kuandamana na kudai wanachodai. Na wao saikolojia yao wanaamini nchi yao ni ya kidemokrasia

27. Hasira za polisi au vyombo vya dola kufikiri vimedharauliwa na hasira zisizo halali kabisa kwani hakuna wananchi wanaodharau askari wao, jeshi lao, au vyombo vya dola;

28. Isipokuwa Polisi na vyombo vya dola wanataka kutumia kanuni za kijeshi kwa wananchi wanaoamini utawala wa kidemokrasia.
Kutokuelewana huko ndio kunatokeaga mvurugano.

29. Sio tuu katika sakata hilo lililopita. Hata katika masakata mengine.
Zipo hadithi Unakuta baadhi ya wanajeshi wanataka kuishi mtaani kama wanajeshi kwa kutumia falsafa za kijeshi mtaani jambo ambalo wakati mwingine inaripotiwa ikileta shida. Kwamba Mjeshi au Askari anataka ukiongea naye uwe kama unaongea sijui na nani jambo ambalo sio sahihi kabisa.

30. Nikielekea kumaliza, Vyombo vya dola, askari polisi na wengine tukio kama hili lisijirudie. Tunapofanya kazi tusifanye kuonyeshana umwamba, kukomoana, hayo sio maadili ya kazi. Hivyo kilichofanyika hata kama ni kudhibiti uhalifu ulikuwa na ukatili na unyama uliopitiliza.

31. Hii inaweza kuleta matokeo mabaya na kuleta chuki na dhana potofu kuhusu kazi ya uaskari ambayo mimi kama Mtibeli naamini na kujua ni moja ya kazi njema na nzuri katika maisha ya viumbe. Kumbuka hata malaika wa mbinguni ni Askari na wanajeshi.
So ni muhimu kila askari kutafakari na kufanya wajibu wake. Ili kuifanya kazi ya uaskari iheshimiwe na mtu akipita asione aibu kujitambulisha kwa watu kubwa yeye ni Askari Polisi.

32. Mwisho, hakuna namna sahihi ya watu kudai haki zao zaidi ya maandamano. Kuzuia maandamano ni kutengeneza ufa mkubwa wa watu kutafuta njia nyingine ngumu zaidi ambazo sio salama kwa taifa.

33. Ni muhimu maandamano yapewe ulinzi na askari ili kupunguza madhara.
Lazima ijulikane kuna watu wanamadai yao. Ni muhimu kuyasikiliza ili tuende pamoja. Tusiende mbali tukawaacha wengine nyuma wakinung'unika.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster.
Kwa sasa Dar es salaam
Moja ya sababu ni chawa kama wewe kutetea uhuni, uhalifu, ukiukaji wa haki za binadamu.
 
Mafanikio yake ni ile kuonekana yalifanyika

Lakini tukirudi kwenye malengo ni kwamba yamefeli.

Kwa sababu swali litaulizwa, kwa nini watu waandamane?
Kisha litafuata, je madai ya maandamano yamejibiwa walau dai hata moja? Au malengo yamefikiwa?

Ni kwamba hayajafikiwa.
Bado unaendelea kudhihirisha ujinga wako. I am sorry if I have offended you to call you "mjinga". But under this scenario, it's the correct word to use it to describe you..

Kwamba madai ya maandamano yamejibiwa ama la, ni udhihirisho wa wazi kuwa, hufikiri vyema kabla ya kusema/kuandika...

Nikuulize swali: Unafahamu kisa cha mgogoro kati ya wana wa Israel (wananchi/watawaliwa vs utawala wa serikali ya Farao wa Misri ya kale upande mmoja, na upande mwingine Mungu mwenyewe kupitia mtumishi wake Musa) kilichorekodiwa kwenye Biblia kwenye kitabu cha Kutoka...?

Sina shaka yoyote kuwa unakifahamu kisa hiki. Unalifahamu tukio hili la kihistoria lililotunzwa vizuri ktk Biblia kwa ajili ya kizazi cha leo na kinachokuja kujifunza..

Kwa ufupi sana, ni kuwa, wana wa Israel walikuwa na madai yao ya kutaka haki zao za kiuchumi, ikiwemo serikali iondoe sera zake za kuwanyanyasa na kuwanyonya, kuwaonea na kubwa zaidi walidai serikali kuondoa zuio la haki yao ya kuabudu Mungu wao iliyokuwa imenyimwa kwao na serikali ya Farao..!

Baada ya kutumia njia mbalimbali kudai haki zao kwa muda mrefu ikiwemo maombi ya kumlilia Mungu wao na Mungu wetu leo, hatimaye Mungu Yehova alisikia kilio chao na kuamua kushuka ili kuwakoa. Tunajua Mungu ni Roho, na sisi wanadamu hatuwezi kumuona ktk umbo, bali hutafuta mwili wa mtu safi na kisha kuingia humo ili kutenda kazi na kusudi lake kwa wanadamu. Aliingia kwa binadamu aitwaye Musa. Akampa nguvu na mamlaka yake ya ki - Ungu...

Honestly, vita ya wokovu na ukombozi ilikuwa kali kwelikweli kati ya Jeshi la Mungu likiongozwa na Kamanda Musa dhidi ya serikali ya Farao na Jeshi lake. The devil never surrender easily..!

Majaribio 9 yalifanyika kumtaka Farao awaachie wana wa Mungu. Kila jaribio lilisababishwa athari kubwa na mbaya ikiwemo vifo vya watu, wanyama, uharibifu wa mali za watu na za umma kwelikweli kwa utawala wa Farao, wananchi na taifa zima la Misri.

Jaribio la 1, 2 hadi la 8 yaliumiza nchi ya Misri sana na wananchi wake lakini Mfalme Farao alikuwa na moyo ngumu kwelikweli kukubali mabadiliko waliyokuwa wanayataka watu. However, kuwa kwake na moyo mgumu haikuwa kikwazo kwa Mungu kutimiza kusudi lake. Ilikuwa ni kusubiri majira na wakati sahihi wa kumfuta kabisa huyo shetani na utawala wake..

Chawa na waandishi uchwara wachambuzi wengi tu wa habari wa Farao ndani ya Misri (kama ulivyo wewe leo Robert Heriel Mtibeli) waliandika na kufanya uchambuzi wao mbalimbali iliojaa dhihaka na kebehi kwa Musa na wananchi wake kushindwa kumtikisa Mfalme Farao ktk harakati zao..

Hakujua kuwa, ukombozi huenda kwa steps moja baada ya nyingine na kila step ikizalisha aina fulani ya matokeo chanya au hasi..

Finally, the final and the last bombshell (pigo la 9) lilimshukia Mfalme Farao na kummaliza na kuufuta kabisa alama zote za utawala wake na Israel akakombolewa. Yeye mwenyewe Farao, Jeshi lake lote na silaha zake zote; mabomu, bunduki, magari ya deraya, magari ya vita, farasi na wapanda farasi waliangamizwa na watu ambao hawakuwa hata na silaha yoyote ya kushikika mikononi mwao..!

#Maana ya simulizi hii kwako ni ipi?

Ni kwamba, unaweza usipate majibu ya madai ya wananchi instantly sasa. Lakini majibu yako tayari, nayo ni kuthibitika, kuanguka na kufutika kabisa kwa utawala wa CCM na serikali yao very soon. Hili limeshafanyika. Itadhihirika wazi muda si mrefu, Amini au Usiamini lakini utaona kwa macho yako muda si kitambo na utanyamaza kimya...

Kwa hiyo forget about kufanikiwa au kutofanikiwa kwa maandamano sasa (kwa maoni na mtazamo wako), though kwa hakika hata katika step hii ya kwanza, yapo mafanikio. Na laiti ungejua kuwa, tukio hili limeu - shake ufalme wa shetani na miungi ya utawala wa CCM na sasa wako kwenye desperation, hofu na woga usioelezeka kirahisi kwao, basi usingethubutu kuja na propaganda yako hii...

Lakini for sure kabisa, sisi wengine tunaelewa vyema kuwa, hofu na woga wao hawa viumbe chini Idd Amini Mama ni halali kabisa kwa kuwa hicho wanachokiogopa na kukihofia kwa HAKIKA KABISA KINAKWENDA KUWAPATA..!

Step by step, TUNASHINDA!
 
Watu sijui mnatumia makalio kujenga hoja? Maana sielewi.

Yaani kutoka kuambiwa "hakuna mtanzania hata mmoja mwenye uthubutu wa kuandamana...." mpaka kufikia hatua ya kuogopa hata kutaja idadi ya vifo, yet unaita ni KUFELI!!!. Shame on you
Maandamano maandamano maandamano kiukweli kwenye mzani ni kama yalifanikiwa
 
Father wewe akili zako kidogo zile ulibakiwa nazo anazo mkeo! Ndiposa kusema wewe kichwani umebeba mimavi mtupu ubongo hakuna tena.
 
Jamaa yng ushakuwa fala ninakushauri acha kuzungumzia yale maandamano jikte kwny mambo mengne maana uwezo wa kuandka mambo mengne unao, ukumbuke watu wana uchungu sn na damu iliyomwaga kshetani vile we bdo unaleta porojo humu. Ktendo cha watanganyika kutoka kwa mara ya kwanza toka tumepata uhuru tena kwa lengo la kuiangusha serikali hilo tu ni mafanikio hata libibi la zenj lilisema hakuna nywinywinywi akna muliro walitamba sn lakn watanganyika walitoka hlo tu ni mafanikio makubwa second time waktoka ujue n hatari sn maana uwoga utakuwa haupo tn na mbinu ztakuwa nyng wapo watatoka kwa hasira ya kufiwa nk patachmbika kwaiyo we kaa kwa kutulia maana wewe hukuandamana ila upo unabeza walioandamana tafadhari bhana.
 
Kumbe we ni mpumbavu ivi..
KWA NINI MAANDAMANO OCTOBER 29 YALIFELI?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kwanza nitoe pole kwa yote yaliyotokea. Waliathiriwa na kuathirika kwa kuuawa, kujeruhiwa na kuharibiwa biashara zao.

2. Niliandika uzi kueleza namna gani maandamano ya October 29 yatakavyofeli. Sikuandika kwamba hayatofanyika. Hivyo wale mnaoninukuu basi wekeni kumbukumbu zenu sahihi.

3. Kimsingi nilijua maandamano ya October 29 yasingezidi masaa sita. Na ndivyo ilivyokuwa. Kama mtakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa maandamano yatafeli(kumaanisha yatakuwepo ila hayatafanikiwa) na yakijitahid basi hayazidi masaa sita.

4. Hapa nitaandika kama mchambuzi. So wasomaji kazi yenu ni kusoma. Sitawaamulia namna ya kufikiri, kuelewa, kupokea na kutoa maoni yenu.

5. Nitaeleza kwa nini maandamano ya October 29 yalifeli sio kwa sababu ya kusikia au kuhadithiwa au kuota bali nikiwa shahidi na shuhuda kwa kilichotokea.

6. Sitampendelea mtu wala sitamuonea Mtu. Nitaeleza kichambuzi. Sehemu ya makosa ya waandamanaji nitasema, sehemu ya makosa ya Askari pia nitasema.

7. Hoja za kufeli maandamano nilishazitoa kabla ya maandamano. Lakini hoja chache ndizo zilizojitokeza na kuyafanya yasifanikiwe kwa ground.

8. Hoja ni kama ifuatavyo;
a) Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwa Waandamanaji.
Hii hoja niliitaja kabla ya maandamano na nilisema itakuwa moja ya hoja zitakazofelisha maandamano.

Siku ya maandamano waandamanaji walikuwa na maslahi na malengo yaliyopishana na kukinzana.
I) Wapo waliokuwa wanataka reforms na mabadiliko ya kweli ya nchi. Hawa walikuwepo. Na niliwasikia.

ii) Wapo waliokuwa wanahitaji Kumtoa Rais Samia suluhu Ikulu. Hawa mpango wao ulikuwa kufika Ikulu na kumng'oa Rais. Walikuwa wakiimba hivyo na kusema na walikuwa wanahakika mpaka usiku wangekuwa wamefika Ikulu.

iii) Wapo ambao walikuwa wanahitaji Watu waliotekwa na kupotezwa.

iv) Wapo ambao walikuwa wanaandamana kama mchezo fulani hivi wa maonyesho. Unaweza kushangaa lakini watu hao walikuwepo. Na niliwaona.

v) Wapo ambao walikuwa na matatizo mengi ambayo hayaelezeki. Hawa walikuwa wakilia tuu. Waliiona huenda siku hiyo ingekuwa siku ya mabadiliko ya matatizo yao.

vi) Wapo ambao kwao hiyo ilikuwa fursa ya kufanya Uhalifu kwa kuvunja na kuiba mali za watu. Watu hao walikuwepo.

Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwenye maandamano kuliyafanya yadhibitiwe.

Nilieleza hapa kwenye uzi wangu wa MY SIDE: matukio ya uhalifu yalifanya waandamanaji kugawanyika na kupungua wengine wakarudi nyumbani. Siongei kukisia au kutunga kama zile riwaya zangu. Hapa nazungumzia kilichotokea.

b) Ukosefu wa Uongozi wakati wa maandamano.
Watu wengi wenye malengo hasa ya kiharakati na kutaka mabadiliko bila kiongozi ni ngumu sana kufanikiwa.

I) Yalifeli kwa sababu hakukuwa na chain of command. Hapakuwa na kiongozi wa kutoa maelekezo na kufuatwa.
Hapakuwa na good organization wakati wa maandamano.
Kila mtu alijifanyia anavyojua. Wengine waliimba, wengine walirekodi, wengine walirusha mawe, wengine walichoma moto, wengine walikuwa wanavamia.

ii) mara kadhaa kulikuwa na mabishano baina ya waandamanaji. Wengine wakisema tufanye hivi wengine hapana jamani tusifanye. Wengine wakikataza uharibifu wengine wakishadadia uhalifu na wengine wakifanya.

iii) Kila barabara ya waandamanaji ingepata viongozi huenda mambo yangeenda vizuri. Na viongozi wapatikane siku ya tukio.

iv) ukosefu wa viongozi tafsiri yake ni kushindwa kufanikisha malengo ya maandamano bila kujali kama yalikuwa na nia njema au mbaya.

c) Kundi la Wahalifu liliharibu muelekeo wa maandamano na kuyafanya yafeli kwa haraka.

i) Niliandika maandamano yalianza kidogo kidogo saa tatu kuelekea saa nne.
ii) Mpaka saa nne na nusu maandamano yalikuwa hayana uhalifu na fujo zile za kutisha. Hata Jeshi la Wananchi JW lilikuwa linalinda raia.
Kwa ambao hamkuwepo hata nyie mliona kwenye video ambazo zimepostiwa mitandaoni.

iii) Wahalifu hasa Wezi na wachoma vituo vya mwendokasi, vituo vya mafuta, vituo vya kuhesabia kura n.k. hawa ndio walibadilisha upepo wa tukio zima.
Hayo yalianza saa tano kuelekea saa sita ambapo yalidumu kwa takribani masaa matatu. Kwa kukata kata. Yaani sio ile non stop.

iv) Hivyo kulikuwa na wahalifu wa maslahi yao binafsi yaani kuiba vitu. Lakini kulikuwa na wahalifu wa kutaka kukomoa serikali na watu fulani hawa ndio walichoma vituo vya mwendo kasi na wengine nyumba za ccm, na watu kadhaa mashuhuri.

9. Askari na Polisi nao hawawezi kukwepa Lawama katika tukio hili.

10. Wao ndio wamesomea kazi hiyo na wanaowajibu wa kulinda watu na mali zao.

11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu.

13. Kama walivyofanya JW wakati wa asubuhi kusaidia waandamanaji waandamane ila kwa usalama bila kuumizana, kuharibu mali na kuleta vurugu hata polisi nao wangeweza kufanya hivyo.

14. Hapakuwa na sababu ya kuuana kwa kiwango kile kama hatua sahihi tangu dakika za awali zingefanyika.

15. Polisi wamekosea pakubwa kutumia nguvu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi.

16. Viongozi wa serikali, vyombo vya dola vinapaswa kujua kuwa saikolojia ya Wananchi ni tofauti na saikolojia ya Polisi au Maaskari.

17. Niligundua pia moja ya madhara Makubwa yamesababishwa na tatizo la tofauti za kisaikolojia baina ya Askari na wananchi.

18. Askari na vyombo vya dola wao saikolojia yao inaongozwa kwa kufuata Amri ya mkubwa bila kujali uhalali wake.
Ila saikolojia ya wananchi au raia hawaongozwi na kwa kufuata amri bila maelezo. Utawala wa kiraia unajenga saikolojia ya kuhoji, kutoa maoni na ikiwezekana kupinga ikiwa amri sio halali.
Hao ni wananchi.

19. Hivyo Polisi anavyomchukulia Rais Samia ni tofauti na raia wa kawaida anavyomchukulia Rais Aamua.
Polisi humchukulia Rais kama Boss wake, mkuu wa kazi na Amir jeshi Mkuu.
Wakati mwananchi humchukulia Rais kama kiongozi aliyemchagua ambaye anamlipa pesa kupitia kodi asimamie rasilimali za nchi ikiwemo watu(yeye)

20. Raia haoni shida kumkosoa Rais au kiongozi yeyote wa nchi kwa sababu kisaikolojia mwananchi anajua yeye ndiye amemuweka pale.
Wakati Polisi Rais akikohoa tuu kidogo atafanya tuu bila kuuliza bila kusita.

21. Polisi, vyombo vya dola ni muhimu kuelewa kuwa mazingira yenu ya kazi hayahusiani na mazingira ya wananchi wengine ambao sio Polisi.
Utawala wa kiraia hasa kwa nchi yenye demokrasia kama yetu ni tofauti na utawala wa kijeshi wa kupokea amri tuu.

22. Lazima tuelewe kuwa Kama Polisi na vyombo vya dola vitaleta mambo yao ya kijeshi kwa raia wananchi wengi watazidi kuumia sana kwani jeshini ndio hakuna ukosoaji, hasa kumkosoa na kumpinga kiongozi aliye juu yako.

23. Rais Samia kama kiongozi wa nchi pia ni muhimu kuelewa kuwa yeye ni Amir jeshi lakini hatakiwi kutumia kanuni za jeshi kwa wananchi wa kawaida.

24. Ili kuondoa mgongano kati ya utawala wa kijeshi na utawala wa kiraia ni vizuri utulivu, hekima, utu na uzalendo vitangulizwe mbele.

25. Kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unaposema watu wasiandamane kwa kutumia koti la kijeshi ni kuleta maumivu, mauaji na majeraha kwani lazima wapo wananchi ambao wao hawakusikilizi kama Amri jeshi mkuu bali wanakusikiliza kama raia mwenye cheo cha urais.

26. Sasa Amir jeshi umesema watu wasiandamane. Watu wakafanya hivyo. Automatically utaona wanakudharau jambo ambalo sio lazima liwe kweli.
Sio kwamba wanakudharau nope! Wao wanaona ni haki yao kuandamana na kudai wanachodai. Na wao saikolojia yao wanaamini nchi yao ni ya kidemokrasia

27. Hasira za polisi au vyombo vya dola kufikiri vimedharauliwa na hasira zisizo halali kabisa kwani hakuna wananchi wanaodharau askari wao, jeshi lao, au vyombo vya dola;

28. Isipokuwa Polisi na vyombo vya dola wanataka kutumia kanuni za kijeshi kwa wananchi wanaoamini utawala wa kidemokrasia.
Kutokuelewana huko ndio kunatokeaga mvurugano.

29. Sio tuu katika sakata hilo lililopita. Hata katika masakata mengine.
Zipo hadithi Unakuta baadhi ya wanajeshi wanataka kuishi mtaani kama wanajeshi kwa kutumia falsafa za kijeshi mtaani jambo ambalo wakati mwingine inaripotiwa ikileta shida. Kwamba Mjeshi au Askari anataka ukiongea naye uwe kama unaongea sijui na nani jambo ambalo sio sahihi kabisa.

30. Nikielekea kumaliza, Vyombo vya dola, askari polisi na wengine tukio kama hili lisijirudie. Tunapofanya kazi tusifanye kuonyeshana umwamba, kukomoana, hayo sio maadili ya kazi. Hivyo kilichofanyika hata kama ni kudhibiti uhalifu ulikuwa na ukatili na unyama uliopitiliza.

31. Hii inaweza kuleta matokeo mabaya na kuleta chuki na dhana potofu kuhusu kazi ya uaskari ambayo mimi kama Mtibeli naamini na kujua ni moja ya kazi njema na nzuri katika maisha ya viumbe. Kumbuka hata malaika wa mbinguni ni Askari na wanajeshi.
So ni muhimu kila askari kutafakari na kufanya wajibu wake. Ili kuifanya kazi ya uaskari iheshimiwe na mtu akipita asione aibu kujitambulisha kwa watu kubwa yeye ni Askari Polisi.

32. Mwisho, hakuna namna sahihi ya watu kudai haki zao zaidi ya maandamano. Kuzuia maandamano ni kutengeneza ufa mkubwa wa watu kutafuta njia nyingine ngumu zaidi ambazo sio salama kwa taifa.

33. Ni muhimu maandamano yapewe ulinzi na askari ili kupunguza madhara.
Lazima ijulikane kuna watu wanamadai yao. Ni muhimu kuyasikiliza ili tuende pamoja. Tusiende mbali tukawaacha wengine nyuma wakinung'unika.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster.
Kwa sasa Dar e
Taikun wa kutoa kinyeo
 
Yale hayakuwa maandamano ulikuwa uhalifu, japo ulipelekea vifo kwa watanzania wenzetu hata wasiohusika.
Yangekuwaje maandamano na wakati jeshi la polisi lilishakataza na kutangaza vita kwa watakaotaka kuandamana siku hiyo? Muda wote viongozi wa dini walikuwa wakihubiri amani huku jeshi la polisi wakitoa vitisho vya hali ya juu.
 
Janja credibility yako imeshakufa naona unatapatapa

Ungebaki tu na zile nyuzi zako za kuwafikisha wanawake kileleni

Hizi mambo zina wenyewe
 
Nawaza hivyo pia, aachane na uandishi wa habari za siasa. Ajikite kwenye mambo ya kijamii zaidi maana kwenye siasa amefeli sana.
 
"11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu."

Yani polisi waliyokuwa wanakataza hayo maandamano na kutoa vitisho wakati wote kiasi kwamba hadi wewe mwenyewe ulitumia kigezo hicho kuwa ni moja ya sababu ya watu wataogopa kutoka kwenda kuandamana.
 
Back
Top Bottom