Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
Wanandoa wengi wa hapa TZ wa siku hizi wanakuwa na uzao wa watoto 2 na ikizidi sana 3 siyo kama wazamani ambapo walikuwa na uzao wa watoto 10 na zaidi. Hii inasababishwa na nini hasa. Maana hata wenye uchumi mkubwa na mzuri sana sana huishia 3 ni kwa nini?
Kimbweka,
Pamoja na maelezo yaliyotolewa na wadau, ni jambo muhimu sana kuhakikisha unapanga uzazi. Kuna sababu nyingi ila uchumi (na hali ya maisha inayoutegemea) unabeba sehemu kubwa. Pamoja na kuwa sisi tulizaliwa karibia 10, siwezi (labda niwe kichaa) kujaribu huo mchezo. Hata kama kifedha najiweza, sitaweza kuwahudumia hao watoto katika mambo yote muhimu. Zamani kazi ya baba ilikuwa kuzaa tu na mama na watoto walitunza mashamba ili kuhakikisha chakula kinapatikana. Kwa hiyo watoto walikuwa ni nguvu kazi pia. Sasa hivi kazi ya kulea ni ya baba na mama.
Halafu hata kama ningependa, isingewezekana kwa sababu wife ana uwezo wa kupata watoto kama 5 au 6 kabla yakufikia menopause. Kwa hiyo hii inaendana na hali ya maisha kama ilivyotoea Ulaya Miaka ya 1800 (soma Marthusian theory). Afrika ya sasa ni kama Ulaya ya miaka 1800 kwa hiyo si suala la kuiga. Ni forces zinazotokana na maendeleo ya kiuchumi.