Kwa nini imekuwa hv

hao wazamani kuwa na watoto wengi ilikua ufahari hawakujali watawatunzaje, sasa hebu imagn maisha ya sasa unaishi chumba kimoja uswahilini utazaa 10 uwalaze wapi? uwalishe nn? Kwa maisha ya sasa acha tu wazae wawili wanawatosha kabisa

Yaani wapo wenye uwezo mkubwa na majumba yao na miradi mbali mbali wala hawafikirii saaana pa kuwalaza wala kuwalisha lakini wanaishia watoto 3 tena hata usiseme uswazi maana huko hata watano (5) wanazaa yaani Vice versa kwa hiyo sababu ya uswahilini na uchumi sijaona kama ya msingi maana matajiri ndiyo wanaongoza kwa idadi ndogo ya watoto wa 2 au 3
 
Zamani kulikuwa hakuna magonjwa, chakula kilikuwa kingi, elimu ilikuwa bure na hata kuishi watu walikuwa wanaishi maisha marefu kuliko sasa. Sasa hv ukibeba mimba ukizaa salama ushukuru mungu unaweza ukabeba mimba ukaumwa sana mpaka uctamani kubeba nyingine, au ukabeba mimba wakati wa kujifungua ukala kisu na mtoto ukakosa (na hii sasa inawatokea watu wengi sana cjui ni kwa nini). Hata elimu kwa sasa ni gharama kubwa sana c kwa masikini wala tajiri na kikubwa zaidi wote baba na mama wanakimbiza pesa na walezi wa watoto wanapatikana kwa tabu, kuwameintain ni gharama kubwa pia na hawakai sana kwa waajiri wao ni wepesi kudanganyika. Zamani ulikuwa unaweza kuomba ruhusa kazini ukakaa hata mwezi unaangalia watoto kama huna mlezi sasa hivi thubutu kama kibarua hakijaota mizizi na kikiota mizizi baba nae anaanza kukuona mzigo

Hapo kwenye red ndipo nahitaji kupajua maana mmmmh
 
Yaani wapo wenye uwezo mkubwa na majumba yao na miradi mbali mbali wala hawafikirii saaana pa kuwalaza wala kuwalisha lakini wanaishia watoto 3 tena hata usiseme uswazi maana huko hata watano (5) wanazaa yaani Vice versa kwa hiyo sababu ya uswahilini na uchumi sijaona kama ya msingi maana matajiri ndiyo wanaongoza kwa idadi ndogo ya watoto wa 2 au 3

Matajiri wanaongoza kwa watoto wachache kwani hata matunzo ya watoto hao gharama zake hawezi kuzaa watoto wengi, shule wanazosoma chakula wanachokula, starehe wanazowapa na bado wenzetu matajiri wanawawekea akiba watoto wao ili hata ikitokea bahati mbaya wamekufa watoto wanakuwa angalau na pa kuanzia. Kwa hiyo wanazaa watoto wachache ili wawape malezi bora na si bora malezi
 
Mapori yapo kibao ila nikuiga uzungu maana hata wenye uwezo wanzaa wa wili!
 
Hakuna anayeiga uzungu kwa kuzaa watoto wachache ni hali halisi. Kama unata uishi maisha waliyoishi baba zako zaa watoto wengi, tena sasa hivi mabadiliko ni mengi. Watoto wengi ni mzigo mkubwa usiobebeka. Sema wazungu walistukia mapema. Wenye kipato kikubwa ndo wanajua balaa la umaskini kuliko maskini wenyewe. Kwa hiyo wenye kipato siku zote wanafanya juu chini ili kipato chao kiendelee kuongezeka na si kupungua. Ukishapata kipato, kurudi kwenye umaskini ni sawa na kufa. Mojawapo ya mbinu ya wenye kipato kuhakikisha hawaanguki (au hata wakianguka waanguke vizuri) ni kudhibiti ukubwa wa familia.

Kwa hali ilivyo sasa hivi watoto wawili (replacement level) ni sahihi kabisa. Binadamu si mbwa au kuku. Lazima tupange. Zamani watu walikuwa wanakwambia wanazaa wengi ili wengine wakifa wengine wabaki. Siku hizi malezi ni bora, vifo vya watoto vimepungua mno. Ukizaa wawili uwezekano mkubwa ni watakua wote. Sasa hivi watu wanafikiria nikifa nitawaachaje wanangu! Ule ujinga wa kila mtoto anakuja na riziki yake unazidi kupungua kwani sasa tunajua riziki ya mtoto iko kwa wazazi wake!
 
Matajiri wanaongoza kwa watoto wachache kwani hata matunzo ya watoto hao gharama zake hawezi kuzaa watoto wengi, shule wanazosoma chakula wanachokula, starehe wanazowapa na bado wenzetu matajiri wanawawekea akiba watoto wao ili hata ikitokea bahati mbaya wamekufa watoto wanakuwa angalau na pa kuanzia. Kwa hiyo wanazaa watoto wachache ili wawape malezi bora na si bora malezi

Mie nimesoma na watoto wa matajiri tena wenye asili ya kiasia na tulikuwa tunagonga msosi wa shule na walikuwa wawili tu kwa hiyo hii bado haijakaa penyewe akilini
 
Hakuna anayeiga uzungu kwa kuzaa watoto wachache ni hali halisi. Kama unata uishi maisha waliyoishi baba zako zaa watoto wengi, tena sasa hivi mabadiliko ni mengi. Watoto wengi ni mzigo mkubwa usiobebeka. Sema wazungu walistukia mapema. Wenye kipato kikubwa ndo wanajua balaa la umaskini kuliko maskini wenyewe. Kwa hiyo wenye kipato siku zote wanafanya juu chini ili kipato chao kiendelee kuongezeka na si kupungua. Ukishapata kipato, kurudi kwenye umaskini ni sawa na kufa. Mojawapo ya mbinu ya wenye kipato kuhakikisha hawaanguki (au hata wakianguka waanguke vizuri) ni kudhibiti ukubwa wa familia.

Kwa hali ilivyo sasa hivi watoto wawili (replacement level) ni sahihi kabisa. Binadamu si mbwa au kuku. Lazima tupange. Zamani watu walikuwa wanakwambia wanazaa wengi ili wengine wakifa wengine wabaki. Siku hizi malezi ni bora, vifo vya watoto vimepungua mno. Ukizaa wawili uwezekano mkubwa ni watakua wote. Sasa hivi watu wanafikiria nikifa nitawaachaje wanangu! Ule ujinga wa kila mtoto anakuja na riziki yake unazidi kupungua kwani sasa tunajua riziki ya mtoto iko kwa wazazi wake!

Kwani wa zamani walikuwa siyo binadamu bali ni mbwa au kuku? na wa leo ndiyo binadamu? Angalia usitusi wazee wako mukulu
 
ndio ujue kwamba kila kitu kimebadilika sasa na sio kama zamani kuna kila aina ya purukushani katika maisha ya sasa

Afadhali hukusome ualimu maana ningekuwa mwanafunzi wako ningetoka kapa ingawa ni jiniazi
 
maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua huwezi kurupuka kubeba mambo yatayokushinda badae sijakata kuna watu wanazaa kila siku je matunzo ya hao watoto yakoje au basi tu tukaujaze ulimwengu
 
jiniazi!!!!!!!!!!!!!!

jiniazi unaewaza kuzaa watoto wengi zama za leo

Kama wasingezaliwa 10 na kwa maana jiniazi alikuwa wa 7 na wangezaliwa 2 baaasi yeye asingezaliwa na tungekosa mchango wake leo katika kuvurumusha gurudumu la maendeleo
 
Ukianza kuzaa na miaka 35 utazaa mara ngapi kabla hujafikia au kukaribia menopause.

Sababu zipo nyingi na zinatofautiana kutoka kwa familia moja kwenda nyingine. Kimsingi nyakati hizi watu wengi wanachelewa kuzaa, wengine wanaogopa kuzaa, wengine wanaogopa kulea, wengine majukumu ya ujenzi wa uchumi wa taifa ni kipaumbele zaidi ya kuzaa wana wengi, wengine wamepata wenzi wasio waaminifu hivyo ndoa haziwi stable kuwezesha kuzalishana etc.
 
mimi nadhani ni kutokana na mabadiliko ya mfumo wa sayansi na technology ambao umebadilisha life style ya watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu bila kuasahau utandawazi yani kila kitu tunaigakutoka nje
 
Ukianza kuzaa na miaka 35 utazaa mara ngapi kabla hujafikia au kukaribia menopause.

Yah hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu za msingi maana enzi zile wasichana /. wanawake walikuwa wanaolewa katika umri mdogo sana na uwezo wa kuzaa watoto wengi ni mkubwa mpaka wafikiapo uzeeni
 
Mi nadhani ni kwenda na wakati wenyewe wanasema. Angalia mtu ana watoto wawili au mmoja na mkewe wa ndoa, lakini ana wengine 2-3 na vimada, sasa unajiuliza inakuwaje ???
Si kwamba ni ugumu wa maisha, na ndio hawa hawa wenye uwezo tunaosema.
 
Duh Chumba cha pili anaongezamo mmmh anyway sijafanyia kazi hilo:hand:
 
kuzaa watoto wachache sio fasheni bali inatokana na aina ya maisha tunayoishi sasa, kama alivyosema mchangiaji mmoja huko juu kuwa siku hizi utakuta wamama wengi si wamama wa nyumbani wanafanya kazi za maofisini au biashara za kuzunguka nchi mbalimbali hivyo kama atakuwa anazaa mara kwa mara itakuwa taabu kufanya shughuli zake

kingine ni kuwa gharama za malezi ya watoto hasa mijini kwa miaka hii ni kubwa mno hasa kuwawezesha kielimu ndio maana utakuta mtu anakuwa na watoto wachache ili aweze kuwamudu ktk malezi na masomo mpk watakapoweza kusimama wenyewe.

Pia uelewa wa watu umekuwa mkubwa siku hizi na masuala ya kupangilia (planning) yamechukua nafasi kubwa ktk maisha hivyo utakuta watu wana-plan kuwa na watoto wachache ili waweze kupata fursa zote kipindi cha makuzi yao

Kupnga uzazi ni moja ya ishara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwani mtu anapanga kuwa na idadi ya watoto kutokana na uwezo wake ili waweze kupata fursa na kukua katika mpangilio mzuri

tofauti na zamani wazazi walikuwa wanazaa watoto ili kuongeza nguvukazi katika familia na baada ya mabadiliko ya tabia nchi na kilimo kukosa tija imesababisha watoto kuwa mzigo kwa wazazi wao ndio maana wazazi wasasa hawataki kufanya makosa kama waliyofanya wazazi wao kwa kuzaa watoto wengi na kushindwa kuwasomesha na kuwawezesha hivyo kuongeza tegemezi katika ukoo
 
Zamani kulikuwa hakuna magonjwa, chakula kilikuwa kingi, elimu ilikuwa bure na hata kuishi watu walikuwa wanaishi maisha marefu kuliko sasa. Sasa hv ukibeba mimba ukizaa salama ushukuru mungu unaweza ukabeba mimba ukaumwa sana mpaka uctamani kubeba nyingine, au ukabeba mimba wakati wa kujifungua ukala kisu na mtoto ukakosa (na hii sasa inawatokea watu wengi sana cjui ni kwa nini). Hata elimu kwa sasa ni gharama kubwa sana c kwa masikini wala tajiri na kikubwa zaidi wote baba na mama wanakimbiza pesa na walezi wa watoto wanapatikana kwa tabu, kuwameintain ni gharama kubwa pia na hawakai sana kwa waajiri wao ni wepesi kudanganyika. Zamani ulikuwa unaweza kuomba ruhusa kazini ukakaa hata mwezi unaangalia watoto kama huna mlezi sasa hivi thubutu kama kibarua hakijaota mizizi na kikiota mizizi baba nae anaanza kukuona mzigo

Maty,

Mengine umesema kweli ila hapo kwenye red umekosea. Chance ya mtoto kuishi hadi kufikai miaka 5 ni kubwa zaidi leo kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Pia uhakika wa chakula bora (siyo chakula tu) ni mkubwa leo kuliko huko nyuma.

Kwenye blue... hayo ni matatizo ya mimba za ukubwani. Mwanamke aliumbwa kuanza uzazi baada ya kuvunja ungo (around 15 years). Sasa wengine wanaanza kuzaa baada ya kufikisha miaka 30. Hiki ni kipindi hatari sana kwa mambo ya uzazi. Maelezo yako mengi ila medically siyo salama kuzaa inapofikia umri wa kuanzia 35. Hata nchi za Magharibi wanalo hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom