Kwa nini imekuwa hv

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Wanandoa wengi wa hapa TZ wa siku hizi wanakuwa na uzao wa watoto 2 na ikizidi sana 3 siyo kama wazamani ambapo walikuwa na uzao wa watoto 10 na zaidi. Hii inasababishwa na nini hasa. Maana hata wenye uchumi mkubwa na mzuri sana sana huishia 3 ni kwa nini?
 
tatizo sio kuzaa taizo kulea, hata kama watu wanakipato, kwa sasa hakuna mwanamke wa kukaa ndani na kulea watoto, unaposema watoto kumi ina maana mama anakuwa ni mimba na kulea tu.
 
tatizo sio kuzaa taizo kulea, hata kama watu wanakipato, kwa sasa hakuna mwanamke wa kukaa ndani na kulea watoto, unaposema watoto kumi ina maana mama anakuwa ni mimba na kulea tu.

siyo anatoa watoto 10 kwa mpigo. Na kama ni kulea hao 2 ama wa3 hawalei? Sidhani kama kulea ni sababu ya msingi. Maana hao waliokuwa wanazaa 10 walikuwa wanafanya kazi haswaa, kulima, kuteka maji, kusanya kuni, kupika, nk na waliweza kulea pia. Hawa wa siku hizi watashindwaje?
 
........uzazi wa sasa hivi unasumbua sana kutokana na haya madawa ya uzazi wa mpango....... hii inapelekea wanandoa kuzaa watoo wa 2 au3. .
 
........uzazi wa sasa hivi unasumbua sana kutokana na haya madawa ya uzazi wa mpango....... hii inapelekea wanandoa kuzaa watoo wa 2 au3. .

Kinachosumbua si dawa za uzazi wa mpango pekee. Kuna matatizo tofauti ya kimaumbile hasa via vya uzazi kwa wanawake na wanaume
 
Ukiachana na maisha ya sasa kuwa ya hali ya juu, Zamani wamama wengi wenye idadi hiyo ya watoto walikuwa wamama wa nyumbani au walimu ambao hawapo busy sana na mihangaiko ya maisha. siku hizi ndani ya nyumba wote tunakimbiza pesa. sasa wewe kama kila siku una mimba au mtoto mchanga utafanya muda gani kazi nyingine?
 
........uzazi wa sasa hivi unasumbua sana kutokana na haya madawa ya uzazi wa mpango....... hii inapelekea wanandoa kuzaa watoo wa 2 au3. .

lakini wapo wasiotumia madawa ila watoto 2 tu na hawazidishi
 
Ukiachana na maisha ya sasa kuwa ya hali ya juu, Zamani wamama wengi wenye idadi hiyo ya watoto walikuwa wamama wa nyumbani au walimu ambao hawapo busy sana na mihangaiko ya maisha. siku hizi ndani ya nyumba wote tunakimbiza pesa. sasa wewe kama kila siku una mimba au mtoto mchanga utafanya muda gani kazi nyingine?

ina maana wa zamani walikuwa hatafuti pesa? Na waalimu wasio bize ni wepi hao? Sidhani kama ni sababu! Na hata siku hizi wapo wa mama wa nyumbani lakini hawazidishi wtt 3
 
Kinachosumbua si dawa za uzazi wa mpango pekee. Kuna matatizo tofauti ya kimaumbile hasa via vya uzazi kwa wanawake na wanaume

asante mkuu je waweza kutuchanganulia hayo matatizo na jinsi ya kukabiliana nayo?
 
Nadhani ni kuiga mambo ya kizungu tu.mana siku hizi mtu ukiwa na watoto zaid ya wa3,unaonekana wa kizamani,ni mambo ya kwenda na wakati tu.
 
Nadhani ni kuiga mambo ya kizungu tu.mana siku hizi mtu ukiwa na watoto zaid ya wa3,unaonekana wa kizamani,ni mambo ya kwenda na wakati tu.

inavyoelekea wazungu wanaturisisha kila kitu! Hehehe ukisasa huo
 
Hebu basi wewe zaa watoto wasio na idadi ndipo utajua kama kuna sababu ya kuzaa watoto wachache ama la!
 
becoz of antchrist obama the prezidaa...ni somo refu kueleweka,but only knw thiz for the moment.
 
Hebu basi wewe zaa watoto wasio na idadi ndipo utajua kama kuna sababu ya kuzaa watoto wachache ama la!

Ukisema watoto kumi unamaanisha idadi yao ni 10, Sasa wasio na idadi ndiyo nini????? Sijakuelewa!!!! Hapa tunataka kujua sababu za msingi, si kwa ubaya huenda kwa upande mwingine ina maana nzuri tu! Tena ningependa kujua kwenu mlizaliwa wangapi na kama ulikuwa wa 7 je? Wangezaa 2 wewe ungekuwepo?
 
Wanandoa wengi wa hapa TZ wa siku hizi wanakuwa na uzao wa watoto 2 na ikizidi sana 3 siyo kama wazamani ambapo walikuwa na uzao wa watoto 10 na zaidi. Hii inasababishwa na nini hasa. Maana hata wenye uchumi mkubwa na mzuri sana sana huishia 3 ni kwa nini?

hao wazamani kuwa na watoto wengi ilikua ufahari hawakujali watawatunzaje, sasa hebu imagn maisha ya sasa unaishi chumba kimoja uswahilini utazaa 10 uwalaze wapi? uwalishe nn? Kwa maisha ya sasa acha tu wazae wawili wanawatosha kabisa
 
Zamani kulikuwa hakuna magonjwa, chakula kilikuwa kingi, elimu ilikuwa bure na hata kuishi watu walikuwa wanaishi maisha marefu kuliko sasa. Sasa hv ukibeba mimba ukizaa salama ushukuru mungu unaweza ukabeba mimba ukaumwa sana mpaka uctamani kubeba nyingine, au ukabeba mimba wakati wa kujifungua ukala kisu na mtoto ukakosa (na hii sasa inawatokea watu wengi sana cjui ni kwa nini). Hata elimu kwa sasa ni gharama kubwa sana c kwa masikini wala tajiri na kikubwa zaidi wote baba na mama wanakimbiza pesa na walezi wa watoto wanapatikana kwa tabu, kuwameintain ni gharama kubwa pia na hawakai sana kwa waajiri wao ni wepesi kudanganyika. Zamani ulikuwa unaweza kuomba ruhusa kazini ukakaa hata mwezi unaangalia watoto kama huna mlezi sasa hivi thubutu kama kibarua hakijaota mizizi na kikiota mizizi baba nae anaanza kukuona mzigo
 
Back
Top Bottom