CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,815
- 9,057
Tanzania ni nchi ambayo 80% ya wananchi wake wanategemea kilimo.
Katika bajeti ya wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi,bajeti ya maendeleo mwaka 2016/2017 ilitengewa Tsh.101,527,497,000/= yaani billion 101.5 Ambapo billion 23 ni fedha za ndani na billion 78.5 ni fedha za Nje(wahisani)
Mpaka sasa fedha zilizotoka kwenda Kwenye miradi ya maendeleo ni Tsh.2,251,881,250/= yaani billion 2.25 ,Hii ni Sawa na 2.22% yaani fedha za maendeleo zilizotolewa na serekali hii kwenye bajeti ya maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi ni asilimia mbili tu(2.22%)
Wewe Kama Mwananchi ungependa Mimi Kama Mbunge niishauri nini serekali yetu.
Maana kazi ya Mbunge ni kuishauri na kuisimamia serekali.
Mwl Marwa Ryoba Chacha Mb Serengeti