Kwa Mwigulu watanzania tuna Waziri Mkuu Kivuli

Kwa Mwigulu watanzania tuna Waziri Mkuu Kivuli

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Poleni sana watanzania kwani tumepata waziri mkuu kilaza kuwahi kutokea, yaani anachokifanya ni upuuzi kiwango cha lami. Ameshindwa kabsa kuelewa kuwa kauli za viongozi ni dira ya taifa.
images (100).jpeg

Ni kauli ambazo zinapaswa kutia moyo, kujenga matumaini na kuzungumzwa kwa umakini mkubwa na sio kuropoka tu kama mtoto mdogo. Sio mara ya kwanza kushuhudia Mwigulu akitema shudu masikioni mwa watanzania huku tukishuhudia matamko ambayo badala ya kutoa mwanga, yanazalisha sintofahamu na hofu.
images - 2025-12-08T195519.149.jpeg

Ni masaa machache tu tumepata kusikia, kauli ya Waziri Mkuu kuitaka jamii ya Watanganyika “kutotoka nje” siku ya tarehe 9, kauli ambayo imeibua mjadala mzito na maswali makubwa kuhusu uhalali, mantiki na hekima ya uongozi wa juu serikalini.
images - 2025-12-08T195528.378.jpeg

Waziri Mkuu ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi. Ni sauti inayotegemewa kuwa tulivu, yenye mizani na heshima. Lakini pale anapotoa matamko yanayoonekana kuwa ya kuamrisha bila msingi wa kisheria, bila maelezo ya kina, bila mkakati wa usalama au sababu ya wazi, inawafanya wananchi kujiuliza: Je tunaye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au “Waziri Mkuu kivuli” anayetoa amri zisizoelezeka?
images - 2025-12-08T195554.228.jpeg

Wananchi wana haki za kikatiba za kutembea, kufanya shughuli zao na kuendelea na maisha bila hofu. Kauli za kuwataka “wabaki ndani” bila tamko la dharura la kitaifa, bila sheria maalum kufuatwa, si tu zinapingana na misingi ya utawala bora bali pia zinadhalilisha hadhi ya ofisi ya Waziri Mkuu. Je ni lini kutoka nje kukawa suala linalosubiri kibali cha mtu mmoja? Je wananchi wanaofanya shughuli zao za kila siku – wafanyabiashara, wakulima, madereva, wagonjwa wanaohitaji hospitali – wanapaswa kusitisha maisha yao kwa tamko lisilo na mantiki?
images - 2025-12-08T195628.950.jpeg

Hili linatosha kuonesha changamoto kubwa ya uongozi wa juu: ukosefu wa busara, ulevi wa mamlaka, na utoaji wa matamko ya kubana uhuru wa raia bila kujali athari zake. Kwa sasa tuna Waziri Mkuu wa ajabu kuliko hata watangulizi wake, amezidiwa busara mbali sana na kina Mheshimiwa Kassim Majaliwa pamoja na Mheshimiwa Mizengo Pinda.
images (100).jpeg

KATIKA HILI WATANZANIA NI KWELI NA NI WAZI TUNA WAZIRI MKUU ZERO BRAINER KABSA!
 
Atakuwa anajuta nafsini kwake. Majaliwa ndio waziri mkuu wa mwisho Tanganyika.
 
The Peter Principle, contends that, in a hierarchy, people are sooner or later promoted to positions which they are no longer skilled to handle. This is their “level of incompetence.”
 
Nchi imegeuka kama kinyesi cha nguruwe cha ajabu mashekhe ubwabwa wanaunga mkono wakati nyama hawalagi.
 
Atakuwa anajuta nafsini kwake. Majaliwa ndio waziri mkuu wa mwisho Tanganyika.
Jamaa limekuwa kama Zuzu yaani lilikuwa linaongea kama limekatwa kichwa
 
Back
Top Bottom