Mi nadhani uliowataji wala hawatoroki.Wapinzani gani mnaowagawa watanzania kwa kueneza chuki, ukabila ukanda na udini.Mmekuwa mkidanganya watu kuwa eti Moshi na arusha zinabaguliwa eti hakuna viongozi wa juu, huku mkisahau kuwa mbegu ile ingekuja kuwaangamiza. Tuliwaonya kwa kuishambulia kanda ya ziwa na wasukuma mlijua mnajiimalisha. Sasa angalia kanda ya ziwa Ndiyo inaongoza kuikimbia chademaktk kipindi cha wiki mbili. Tulisema tulisema na tutasema kwamba mmechagua wenyewe sehemu kisu kinatakiwa kuchinja.Watanzania hawataki kusikia ubaguzi hawajafika huko. Mnasema miradi mikubwa intends kanda ya ziwa. Nenda Arusha ukaone shughuli inayoendelea ya kuwaletea wananchi mradi mikubwa ya maji kupitia benki ya dunia. Angalia barabara iliyokamilika ya kutoka Tengeru hadi Sakina na bado mkandarasi huyo huyo kapewa mkataba mpya chapu chapu .Barabara inaanzia Maji chai kupitia Njiro hadi .........HAlafu watu wanashinda kwenye keyboard kuponda. Lake zone mmewatesa sana kwa miporojo yenu, Protas Masha Kitilya TOROKENI MJE.Mtachoshwa na wachonganishi wasio itakia mema nchi
.....Acha ufisi.maji unakopi uzi woote kuweka upupu wako ili iweje??Kwani li Upinzani likifa tunapata hasara gani ? HATULITAKI LI UPINZANI LINATUMIA HELA NYINGI MNO ZA RUZUKU
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.
Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.
Wasalaam.
Paskali
Anaimarisha Upinzani bila kuelewa!
“When the going gets tough, the tough get going”Anaimarisha Upinzani bila kuelewa!
Masha kweli ni mjinga tena mchumia tumbo kabisaaaa.Hata siku Mbowe akaacha chadema akarudi ccm utasema hivyo hivyo kuwa na yeye mwanzo alikuwa ccm hana impact yoyote.
Hakuna mpinzani ambaye hajawahi kuwa CCM as of now, so wote ni wale wale. Wapinzani wote ni wanachama wa ccm wa zamani, ifike mahali chadema ikiri kwa sasa hali yao sio nzuri, hawana sera, hawana agenda na wajipange kuliko kuwakashifu kila anayetoka mkisahau kila mtu anao uhuru wa kujiunga na kuhama chama muda wowote anaotaka akiamua bila hata kutoa sababu.
Majuzi tu mlikuwa mnamsifia Masha wakati wa uchaguzi EA, leo mnamtukana. Ndio maana chama hakiwezo kuwa na member wanaojitambua maana wengi ni watukanaji na wakashifu watu tu
JPM hajawahi kuchukia ufisadi wakati yeye in sehemu ya ufisadi. Anachukia kuona watu wanafaidika kama alivyosema mwenyewe kuwa anapenda kuona tukiishi kama mashetaniWanabodi,
Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.
Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.
My Take.
- Jee CCM imara, ina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania?.
- Jee kuna uukweli kuwa rais Magufuli hana nia njema na upinzani Tanzania, ndio maana alisema kamwe hatateua wapinzani kwenye serekali yake?.
- Uteuzi wa Mama Anna na Prof. Kitila, ni uteuzi wa hongo ili kuisambaratisha ACT, na sasa kazi kuisambaratisha Chadema, ndio imeanza?.
- Jee ni kweli Viongozi wa upinzani wanaohamia Chadema, wamenunuliwa?.
- Jee katazo la rais Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ya kitaifa, inawezekana halina nia njema na upinzani?.
- Jee ni kweli rais Magufuli, anaendelea kutumia rasilimali za taifa kuitangaza CCM katika mikutano ya kiserikali, au ya kichama inayofanyikia kwenye venue za serikali, hivyo kugharimiwa kwa fedha za umma?.
- Kama katiba ya nchi, rais Magufuli aliyoapa kuilinda, inaruhusu mikutano ya kisiasa, lile katazo lake kuzuia mikutano hiyo, lina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania.
- What does Mhe. rais Magufuli stand to loose kama ataruhusu shughuli za kisiasa nchini kuendeshwa kwa mujibu wa katiba?. Yaani anapata nini kuzuia mikutano?.
- Kwa watu wenye uwezo wa kosoma nia njema iliyoko ndani ya moyo wa mtu kupitia facial expressions mtu anapozungumza, jee kuna nia jema kuhusu upinzani nchi Tanzania katika awamu hii?.
- Kwa vile upinzani nchini Tanzania, upo kwa mujibu wa katiba, jee mtu yoyote mwenye nia ya kuudhoofisha upinzani nchini Tanzania, ana nia njema kweli na taifa hili?. Inawezekana kwa mtu kuwa na nia njema na maendeleo ya taifa, at the same time, ukafifisha demokrasia kwa kudhoofisha upinzani?.
Kazi ya upinzani Zaidi ya kutaka kwenda ikulu, pia kuisimamia serikali kule bungeni kupitia mawaziri mbadala, kusimamia matumizi ya fedha za umma kupitia oversight committee, ili kujihakikishia serikali inasimamiwa ipasavyo, Tanzania tunahitaji kuwa na upinzani imara, kama juhudi za rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, uzembe, ubadhirifu na ufisadi, matokeo yake ni kuua upinzani, kwa wapinzani kukosa hoja za kuendelea kuwa wapinzani, hivyo kuamua kujiunga na CCM kumsaidia Magufuli, jee ni nini mustakabali wa Tanzania yenye upinzani hafifu?.
Jee Tumeanza safari ya kuelekea nchi ya chama kimoja cha siasa?, na uchaguzi wa rais 2020, utakuwa ni uchaguzi wa rais kweli au litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini rais wa Tanzania hadi 2025, ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli?. If this is case for 2020, kwa umasikini wetu nchini Tanzania, do we real need to spend so much kufanya igizo hili?. Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Wasalaam.
Paskali
CCM ndiye baba, bahati mbaya wamekuwa wabinafsi, wasiopenda wenzao washiriki siasa kama wao wanavuoshiriki. Ingawa kwa sasa wanajiona wanafaidika na hali hiyo lkn wanaweka rehani mustakabali wa nchi yetu kwa kuwabana wenzao wakati wao wanafanya siasa kama kawaida.Huu si wakati wa kumjadili magufuli wala ccm,ingependa kama ungejadiliwa upinzani,lakini kwa mahaba yalivyowazidi mnawajadili ccm kana kwamba ccm wanajali upinzani ukifa
Sawa CCMHata siku Mbowe akaacha chadema akarudi ccm utasema hivyo hivyo kuwa na yeye mwanzo alikuwa ccm hana impact yoyote.
Hakuna mpinzani ambaye hajawahi kuwa CCM as of now, so wote ni wale wale. Wapinzani wote ni wanachama wa ccm wa zamani, ifike mahali chadema ikiri kwa sasa hali yao sio nzuri, hawana sera, hawana agenda na wajipange kuliko kuwakashifu kila anayetoka mkisahau kila mtu anao uhuru wa kujiunga na kuhama chama muda wowote anaotaka akiamua bila hata kutoa sababu.
Majuzi tu mlikuwa mnamsifia Masha wakati wa uchaguzi EA, leo mnamtukana. Ndio maana chama hakiwezo kuwa na member wanaojitambua maana wengi ni watukanaji na wakashifu watu tu
Subiri Kafulila apewe uDC, Katambi nae atapata uteuzi, Slaa kashapata.Kuna tofauti kubwa kati ya kenge na mamba