Kwa mujibu wa Katiba Lissu amepoteza sifa ya kugombea Urais na Ubunge 2020

..wako wanasheria wengi wabobezi kuliko TL.

..lakini ni wachache sana wenye msingi na dira ya kimaadili, na ujasiri wa kutetea haki kama TL.

..wengi wanasukumwa na ambitions za kupata utajiri, vyeo, au mamlaka. Lakini TL kinachomuongoza ni kutetea HAKI.

..TL ametetea wanyonge nchi hii akiwa hana cheo wala ulinzi. Ameanza harakati hizo akiwa kijana mdogo aliyetoka chuo kikuu.

..Vijana wana mengi ya kujifunza toka kwa TL.
Tundu tumbo mbele kamanda
 
Umbumbu wa maccm kakisome vzr uwe umetiwa hatihani na hukumu ya mahakama,bunge sio mahakama.
 
Hivi awamu ya 5 kuna katiba!!!! Hivi kuna katiba inayosema kada wa ccm asimamie uchaguzi wa ubunge, udiwani au urais?????? Hivi sisi watanzania ni wajinga na wapumbavu kiasi gani!!!!! Ashakum si matusi!
 
Bashir Yakub,

..maelezo yako ni mazuri.

..Je, kwenye suala la TL alitakiwa achukuliwe hatua na Tume au Bunge?

..Je, kabla ya kuchukuliwa hatua alitakiwa apewe nafasi ya kujitetea au hakuna nafasi kama hiyo kwa makosa yanayohusiana na kujaza fomu ya maadili?
Mkuu serikali ya chama cha cowards inafanya mambo yake kwa kuvizia vizia.
 
Akigeuka huku kea mwanasheria mkuu wa serikalib profesa wa Sheria profess kilangi akigeuka huku anakutana na waziri wa Sheria na katiba na maalimu wa zamani chuo kikuu Dr mahiga akigeuka mambo ya nchi za nje anakutana na profesa wa Sheria profesa kabudi patamu hapo
Endelea basi! Akienda kwenye madini ana kutana na Profesa Ossoro, akirudi kwenye uchumi yupo Profesa Lipumba!
Kwi kwi kwi! Hakika mna timu matata na imara kama ile ya Makonda inayoitwa Taifaccm Stars!
 
Endelea basi! Akienda kwenye madini ana kutana na Profesa Ossoro, akirudi kwenye uchumi yupo Profesa Lipumba!
Kwi kwi kwi! Hakika mna timu matata na imara kama ile ya Makonda inayoitwa Taifaccm Stars!
Mkuu hivi kwanini usikishauri chadema kujikita kueneza sera na mipango mujarabu kuhusu nchi yetu kuliko hivi vihoja vyenu mnavyodandia humu jf?
Tofauti yenu na ccm iko wapi hasa?
 
..nadhani TUME YA MAADILI inatakiwa kufanya MCHAKATO WA HAKI kabla ya kufikia uamuzi kuwa TL amekiuka sheria ya maadili na hastahili kugombea ubunge kwa miaka 5.

..Nawakumbusha Andrew Chenge alivyosumbuana na Tume ya Maadili lakini kitendo hicho hakikupelekea kuzuiwa kugombea ubunge.

KWA MUJIBU WA KATIBA LISSU AMEPOTEZA SIFA YA KUGOMBEA URAIS NA UBUNGE 2020.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255 784 482 959 .

Ndugai anasema moja kati ya makosa mawili yaliyopelekea Lissu kufutwa ubunge ni kosa la kutojaza taarifa za mali na madeni.

Kosa hili kwa mujibu wa ibara ya 67(2)( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ibara hiyo imeeleza kuwa mbunge yeyote anakosa sifa za kuendelea kuwa mbunge au kuchaguliwa kuwa mbunge ikiwa atakuwa amekiuka ama kuvunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Zaidi, ibara hiyo imeweka wazi kuwa, mtu huyo ataendelea kukosa sifa ya kuwa mbunge au kutochaguliwa kuwa mbunge katika kipindi cha miaka mitano tokea siku alipovunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Maana yake ukiivunja Sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo 2019 basi tunahesabu miaka mitano tokea leo 2019 ambayo itakuwa hadi 2024(kama sijakosea hesabu) ndipo sasa unakuwa na sifa tena ya kuweza kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge. Kwahiyo Lissu atakosa sifa hii ya kuwa au kugombea tena ubunge hadi 2024.

TWENDE KWENYE URAIS.
Ibara ya 39( 1 ) ( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha wazi kuwa moja ya sifa kuu ya kugonbea kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano ni kuwa na sifa ya kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Maana yake, ili uweze kuwa na sifa ya kuwania kiti cha rais lazima kwanza uwe na sifa za kuwa mbunge au Mjumbe Baraza la Wawakilishi, na unapokosa sifa ya kuwa mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi basi unakosa pia na sifa ya kuwania kiti cha Rais.

Kwahiyo kama Lissu amepoteza sifa ya kuwa mbunge hadi 2024 basi amepoteza pia sifa ya kuwania kiti cha Rais hadi 2024 kadhalika.

Hivyo basi Lissu hataweza kugombea ubunge hadi hiyo 2024, lakini pia hataweza kugonbea urais hadi 2024.

Hii ndio Calculation ya Kisheria na ndio ukweli hadi itakapotamkwa vinginevyo na vyombo vyenye mamlaka.
Hilo litatokea ikiwa kuna ukweli wowote kwenye Tuhuma ya kukiuka maadili ya umma , HAIWEZI KUTOKEA KWA SABABU MAGUFULI KASEMA KUPITIA NDUGAI , NEVER EVER !
 
Kwani marekani na uingereza alikoenda kuhutubia alienda akiwa kabebwa kwenye machela?
Aliyeleta mada hajui lolote.

Kujaza fomu ya maadili ni jukumu la mbunge ambaye yupo kazini. Mbunge mgonjwa wakati wote akiwa mgonjwa yupo exempted na wajibu wa mbunge ambaye yupo kazini ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya bunge na kamati.

Kesi ya TL ni moja tu, ni mgonjwa au siyo mgonjwa? Akithibitisha kuwa alikuwa mgonjwa na spika alikuwa anajua, kesi ya maadili itakuwa nayo imekufa.
 
Hii Sheria imemnyoa Tundu Lisu kiduku original

Hapo jiwe atafurahi maana hawezi siasa za ushindani. Anaogopa dhahama iliyomkuta JK uchaguzi wa 2010 dhidi ya Slaa. Jiwe hata alipokuwa mbunge hakuwa na historia ya kushindana kwa hoja zaidi ya kupita kwa hujuma. Hii ndio unaambiwa Yanga ni timu kali kishenzi, lakini siku ya mechi na simba wanaifanyia hujuma ili Yanga ipate point za mezani! Hii hofu yote ndio inadhihirisha ccm inajidanganya yenyewe kuwa inakubalika wakati inaujua ukweli.

Ni hivi akikubali kushindana na Lissu aandae kufanya mauji ya kimbari, na Lissu akifanyiwa hila ili asigombee ni kuwa kamuogopa.
 
Akigeuka huku kea mwanasheria mkuu wa serikalib profesa wa Sheria profess kilangi akigeuka huku anakutana na waziri wa Sheria na katiba na maalimu wa zamani chuo kikuu Dr mahiga akigeuka mambo ya nchi za nje anakutana na profesa wa Sheria profesa kabudi patamu hapo

Nguvu ya ccm ni moja tu, vyombo ya dola na kundi la watu wasiojulikana . Kinyume na hapo ni aibu ya karne.
 
KWA MUJIBU WA KATIBA LISSU AMEPOTEZA SIFA YA KUGOMBEA URAIS NA UBUNGE 2020.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255 784 482 959 .

Ndugai anasema moja kati ya makosa mawili yaliyopelekea Lissu kufutwa ubunge ni kosa la kutojaza taarifa za mali na madeni.

Kosa hili kwa mujibu wa ibara ya 67(2)( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ibara hiyo imeeleza kuwa mbunge yeyote anakosa sifa za kuendelea kuwa mbunge au kuchaguliwa kuwa mbunge ikiwa atakuwa amekiuka ama kuvunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Zaidi, ibara hiyo imeweka wazi kuwa, mtu huyo ataendelea kukosa sifa ya kuwa mbunge au kutochaguliwa kuwa mbunge katika kipindi cha miaka mitano tokea siku alipovunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Maana yake ukiivunja Sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo 2019 basi tunahesabu miaka mitano tokea leo 2019 ambayo itakuwa hadi 2024(kama sijakosea hesabu) ndipo sasa unakuwa na sifa tena ya kuweza kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge. Kwahiyo Lissu atakosa sifa hii ya kuwa au kugombea tena ubunge hadi 2024.

TWENDE KWENYE URAIS.
Ibara ya 39( 1 ) ( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha wazi kuwa moja ya sifa kuu ya kugonbea kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano ni kuwa na sifa ya kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Maana yake, ili uweze kuwa na sifa ya kuwania kiti cha rais lazima kwanza uwe na sifa za kuwa mbunge au Mjumbe Baraza la Wawakilishi, na unapokosa sifa ya kuwa mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi basi unakosa pia na sifa ya kuwania kiti cha Rais.

Kwahiyo kama Lissu amepoteza sifa ya kuwa mbunge hadi 2024 basi amepoteza pia sifa ya kuwania kiti cha Rais hadi 2024 kadhalika.

Hivyo basi Lissu hataweza kugombea ubunge hadi hiyo 2024, lakini pia hataweza kugonbea urais hadi 2024.

Hii ndio Calculation ya Kisheria na ndio ukweli hadi itakapotamkwa vinginevyo na vyombo vyenye mamlaka.
Umeweka na Namba kabisa ili uteuzi ukufikie Kwa Haraka
 
Back
Top Bottom