Kwa mujibu wa Katiba Lissu amepoteza sifa ya kugombea Urais na Ubunge 2020

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
KWA MUJIBU WA KATIBA LISSU AMEPOTEZA SIFA YA KUGOMBEA URAIS NA UBUNGE 2020.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255 784 482 959 .

Ndugai anasema moja kati ya makosa mawili yaliyopelekea Lissu kufutwa ubunge ni kosa la kutojaza taarifa za mali na madeni.

Kosa hili kwa mujibu wa ibara ya 67(2)( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ibara hiyo imeeleza kuwa mbunge yeyote anakosa sifa za kuendelea kuwa mbunge au kuchaguliwa kuwa mbunge ikiwa atakuwa amekiuka ama kuvunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Zaidi, ibara hiyo imeweka wazi kuwa, mtu huyo ataendelea kukosa sifa ya kuwa mbunge au kutochaguliwa kuwa mbunge katika kipindi cha miaka mitano tokea siku alipovunja sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Maana yake ukiivunja Sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo 2019 basi tunahesabu miaka mitano tokea leo 2019 ambayo itakuwa hadi 2024(kama sijakosea hesabu) ndipo sasa unakuwa na sifa tena ya kuweza kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge. Kwahiyo Lissu atakosa sifa hii ya kuwa au kugombea tena ubunge hadi 2024.

TWENDE KWENYE URAIS.
Ibara ya 39( 1 ) ( d ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha wazi kuwa moja ya sifa kuu ya kugonbea kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano ni kuwa na sifa ya kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Maana yake, ili uweze kuwa na sifa ya kuwania kiti cha rais lazima kwanza uwe na sifa za kuwa mbunge au Mjumbe Baraza la Wawakilishi, na unapokosa sifa ya kuwa mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi basi unakosa pia na sifa ya kuwania kiti cha Rais.

Kwahiyo kama Lissu amepoteza sifa ya kuwa mbunge hadi 2024 basi amepoteza pia sifa ya kuwania kiti cha Rais hadi 2024 kadhalika.

Hivyo basi Lissu hataweza kugombea ubunge hadi hiyo 2024, lakini pia hataweza kugonbea urais hadi 2024.

Hii ndio Calculation ya Kisheria na ndio ukweli hadi itakapotamkwa vinginevyo na vyombo vyenye mamlaka.
 
tuaachie mahakama itaamua kama suala la lisu watalipeleka mahakamani lkn atayashind yote kamanda lisu mungu yupo upande wake
 
kwa Prof.Kabudi kwenye sheria Tundu Lissu lazima akae chini na kurudi upya darasani.

..wako wanasheria wengi wabobezi kuliko TL.

..lakini ni wachache sana wenye msingi na dira ya kimaadili, na ujasiri wa kutetea haki kama TL.

..wengi wanasukumwa na ambitions za kupata utajiri, vyeo, au mamlaka. Lakini TL kinachomuongoza ni kutetea HAKI.

..TL ametetea wanyonge nchi hii akiwa hana cheo wala ulinzi. Ameanza harakati hizo akiwa kijana mdogo aliyetoka chuo kikuu.

..Vijana wana mengi ya kujifunza toka kwa TL.
 
kwa Prof.Kabudi kwenye sheria Tundu Lissu lazima akae chini na kurudi upya darasani.
Akigeuka huku kwa mwanasheria mkuu wa serikalib profesa wa Sheria professa kilangi akigeuka huku anakutana na waziri wa Sheria na katiba na mwalimu wa zamani chuo kikuu Dr mahiga akigeuka mambo ya nchi za nje anakutana na profesa wa Sheria profesa kabudi patamu hapo
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom