Kwa mtaji wa 25 million nifanye biashara gani?

Kama utaona yakufaa fanya hivi:

1. Nunua pikipiki 5 jumla ni milioni 10. Wape vijana kwa mkataba wa kisheria wakupe elfu 10 kwa siku baada ya Mwaka unamwachia pikipiki. ( uwape mkataba wa kisheria akipoteza anakulipa) kwa siku ni 50000 sasa itakuwa 50000×365 = 18,250,000

Faida kwa mwaka ni 8,250,000. Kwa mwezi ni kama 687,500.

2. Fungua M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money & Halopesa mahali vibanda viwili pia usajili laini hapo hapo. Kibanda cha kwanza mtaji 2mil, makadirio ya commission 350,000 (mfanyakazi laki, kibanda 50,000, umebaki na 200,000)
Kwa hiyo vibanda viwili baada ya kodi na mishahara yao makadirio ya faida ni 200,000 × 2 = 400,000 Fanya 350,000 incase of anything.

Milioni 6 Iliyobaki: 3mil weka M-Pawa au fixed account ikulinde.

Milioni 3 nyingine fungua kaduka fulani kadogo lakini ka wadhifa weka vyakula au bidhaa za urembo (au yoyote isiyooza) Soma soko lakini 'ANZIA SOKONI' Hapo utapata hela ya kula daily, vocha, home kuacha elfu 5 kama una familia.

Kwa haraka haraka utakuwa umetengeneza mshahara 687,500 (pikipiki) + 350,000 (M-Pesa n.k) = 10337500 yaani milioni kila mwezi.

Kumbuka mtaji wako uko pale pale ndugu. Kila la heri na shetani asipite huko maana kazidi.
 
Kaka hizo hela nyingi sana tuliza akili utakuwa tajiri ndani ya mwaka tu usilete ushikaji wala kuhonga idea ziko nyingi sana za kukutoa kiufupi kila biashara INA faida nzuri tegemea na uwekezaji na jinsi ya kufanya hiashara kamwe usiruhusu mawazo ya MTU eti panda mbegu vuna mbegu au kubet
Mafanikio mema
 
Nyie mnaomuita muomba ushauri pm sio poa kabisa, hamjui kama mkimshauri hapa hapa jukwaani wengi watafaidika kupitia uzi wake? Na wewe mleta uzi wakishakupa hizo nondo huko pm zikopi na upesti hapa jukwaani tufaidike sote.
 
Mkuu tuliza akili alafu ukitaka kuanza nikushauri usiweke pesa yote 25m, anza kwa kutake risk maybe 10 million then ukiona ina develop, invest moja katika iko kitu last kama ukiweza tembea maeneo kutana na watu physical wakupe changamoto ya biashara zao, mbinu ya kufika na namna ya kuepuka vishoka wanaomaliza mtaji.
 
Kila la kheri but kuwa makini na masuala ya PM. Pia epuka appointment ya man to man hizo 25m zinaweza kuchukuliwa saa sita mchana ukajuta, sidhani kama kuna ushauri/idea ya biashara ya siri mtu aweke public Watanzania wenzake wafaidike hata kama hawana mtaji leo kesho watapata tayari wakiwa na wazo/business plan
 
Mandison,

Nunua Boti maalum za kuweza kuwaopoa Wanadamu / Maiti zilizo katika mifuko ya Sandarusi na zimefungwa mawe makubwa ya Fatuma ambazo mara nyingi huwa zinaelea Coco Beach, Kawe Beach, Kunduchi Beach na Mbweni Beach Mkuu utapata sana faida kwani utakuwa unalipwa na wenye Ndugu au Mamlaka husika ambazo hazina hizo Boti maalum.
 
Sijawahi kufanya biashara ya aina yeyote isipokuwa nimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 25/-m ambazo nafikiria kujiajiri kwa kufanya biashara.

Naomba wazoefu wa Jiji la Dar mnipe ushauri juu ya biashara ya kufanya tafadhali.
Biashara za mazao zinalipa sana, na kwa mtaji huo naamin unatosha kabisa kuanza biashara hiyo lakini biashara zipo nyingi, cha msingi angalia wewe unapenda nini maana itakuwa rahisi kukifanya na kukisimamia ili upate faida zaidi
 
Ningekua ndio mimi, ningewahi TMT pale Jangid Plaza Oysterbay Dar es Salaam.
Napiga pindi la week moja, then natupia mpunga wooote JP
 
Back
Top Bottom