Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Mkuu pili pili zangu zimekumbwa na bacteria wilt mche unakuwa Kama umemwagiwa maji ya moto unasinyaa matunda yanaanguka na baadae mche unakufa na pia ukiangalia matunda yanakuwa na rangi nyeusi kanakwamba yamepigwa na jua kali na baadae yanaoza nifanyeje kiongozi
 
Miche inakuwa kama kama hizo picha
Screenshot_2018-03-02-12-01-04.png
Screenshot_2018-03-02-11-59-31.png
Screenshot_2018-03-02-11-57-07.png
 
Avoid kutonesha mimea,piga copper based fungicide izuie spread kwa hewa na kupitia wounds,dawa ya kutibu hakuna pole sana ndugu yangu acha kulima mazao ya jamii ya solanacea kama nyanya,ngogwe,hoho etc
 
Miti yangu ya miparachichi baadhi huanza kunyauka hadi inspukutisha majani yote na kubaki kijifito tu,baadaye huanza kuotesha majani upya,na mengine haioteshi tena,nini ufumbuzi wa changamoto hii?
 
Miti yangu ya miparachichi baadhi huanza kunyauka hadi inspukutisha majani yote na kubaki kijifito tu,baadaye huanza kuotesha majani upya,na mengine haioteshi tena,nini ufumbuzi wa changamoto hii?

Maneno matupu sio rahisi kufahamu tatizo,mmea ni kama binadamu huwezi pata tiba sahihi kwa kuelezea tu,tuma hata picha.
Tazama kama inawadudu pia tazama maji kama yanatosha yaani unanyesha au ndio mpaka mvua ije.

Vingi vinaweza sababisha die back kwenye mmea huenda mazingira,wadudu au ugonjwa
 
kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo cha mboga,matunda,maua,viungo na dawa.Wataalam na wakulima tukutane hapa
ni muda gani muafaka kufanya kilimo cha vitunguu? kitunguu kipi bora kwenye soko kati ya chekundu na cheupe? ekari moja gharama za kuandaa shamba mpaka kuvuna kitunguu zaweza fika tsh ngapi?
 
ni muda gani muafaka kufanya kilimo cha vitunguu? kitunguu kipi bora kwenye soko kati ya chekundu na cheupe? ekari moja gharama za kuandaa shamba mpaka kuvuna kitunguu zaweza fika tsh ngapi?

Muda hubadilika sehemu na sehemu kutegemea na soko,vile vile aina ya kitunguu hutegemea soko lako ila kwa Tanzania vyekundu bora zaidi kwa soko letu.
Gharama za shamba kwa ekari uwe na atleast milioni mbili
 
thank you ndg na upatikanaji wa mbegu ??? kariakoo ni sehemu bora kununua mbegu ....wadaresalama nawaogopa saaaaana
 
thank you ndg na upatikanaji wa mbegu ??? kariakoo ni sehemu bora kununua mbegu ....wadaresalama nawaogopa saaaaana

Watakujibu wenyeji vyema mimi sio mwenyeji kabisa na dsm,ila itapendeza ukinunua mbegu kampuni husika au wakala wao direct
 
Nafaka kawaida hazina faida kubwa labda milioni moja au mbili kwa ekari sema zina risk ndogo kulinganisha na mboga mboga
 
Back
Top Bottom