Kwa mara ya kwanza Rais Samia kamgusa Mzee Jakaya Kikwete?

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Kurejeshwa Makalla ndani ya mfumo mwaka 2021 na kuwa RC Dar es Salaam tukubali ama tukatae ipo nguvu ya ushawishi wa JK ilitumika kumshawishi Rais Samia.

Ieleweke, Makalla ni swahiba na mwandani lialia wa Jakaya Kikwete na duru zilitabanaisha baada ya JPM kumfuta kazi Makalla kipindi kile mwana Msoga aliumia ki aina.

Ukweli ni kwamba, Makalla hana uwezo wa kuongoza kwa nafasi ya Mkuu wa Mkoa kwa sababu ni mswahili na mtu mwenye taralila nyingi huku utendaji ukiwa sifuri! Kwa ufupi, ni mjanja mjanja tu asiye na maarifa ya kuongoza.

Ni wazi sasa, huenda Rais Samia ameamua ampe Dar es Salaam mtoto wa zao lao yeye na Magufuli ndugu Chalamila na kumshusha mpendwa wa JK.

Kutolewa Dar es Salaam na kutupwa Mwanza ni sawa na kushushwa japokuwa majukumu ni yaleyale.

Je, ni mwanzo wa zao la JPM na Rais Samia kupewa sehemu nyeti?

Ni wazi hilo ni jaribu la kwanza kwa watu wa timu JK kutoswa.

Mda utasema.
 
Kurejeshwa Makalla ndani ya mfumo mwaka 2021 na kuwa RC Dar es Salaam tukubali ama tukatae ipo nguvu ya ushawishi wa JK ilitumika kumshawishi Rais Samia.

Ieleweke, Makalla ni swahiba na mwandani lialia wa JK na duru zilitabanaisha baada ya JPM kumfuta kazi Makalla kipindi kile mwana Msoga aliumia ki aina.

Ukweli ni kwamba, Makalla hana uwezo wa kuongoza kwa nafasi ya Mkuu wa Mkoa kwa sababu ni mswahili na mtu mwenye taralila nyingi huku utendaji ukiwa sifuri! Kwa ufupi, ni mjanja mjanja tu asiye na maarifa ya kuongoza.

Ni wazi sasa, huenda Rais Samia ameamua ampe Dar es Salaam mtoto wa zao lao yeye na Magufuli ndugu Chalamila na kumshusha mpendwa wa JK.

Kutolewa Dar es Salaam na kutupwa Mwanza ni sawa na kushushwa japokuwa majukumu ni yaleyale.

Je, ni mwanzo wa zao la JPM na Rais Samia kupewa sehemu nyeti?

Ni wazi hilo ni jaribu la kwanza kwa watu wa timu JK kutoswa.

Mda utasema.
Acheni kumlisha rais Dkt Samia maneno. Hayo ni mabadiliko ya kawaida na kumbuka Mwanza ni ngome muhimu kuelekea 2025, inahitaji mtu makini kama Makalla. Hivyo Makalla kapandishwa na hajashushwa maana anaenda kutafuta kura za rais 2025 kanda ya ziwa.
 
KWA MAANDIKO yako ya hivi karibuni !sibezi wazo lako!

Inaonekana you are well informed !

Nilipoona mgomo kariakoo kwenye Base ya makusanyo ya kodi nikajua hii ishu ni ya kupika hasa katika wiki hizi za misiba na sintofaham ya kutohudhuria KWA WENYE CCM misibani!!

Ngoja tuone!
 
Makonda, apewe TU, some people here are very stressful. Tena angewa DSM. Ningeshukuru
Makonda hawezi rudishwa serikalini ni miongoni mwa vijana idiot kabisa kuwahi kutokea. Hawa ndiyo waliharibu sana na kumharibia Dkt Magufuli enzi zake, yaani Makonda anapaswa kufungwa na akina James Dotto wajinga sana wale. Walidhani wao ni zaidi ya raia
 
Aliharibu nini kwa mfano?
 
Acheni kumlisha rais Dkt Samia maneno. Hayo ni mabadiliko ya kawaida na kumbuka Mwanza ni ngome muhimu kuelekea 2025, inahitaji mtu makini kama Makalla. Hivyo Makalla kapandishwa na hajashushwa maana anaenda kutafuta kura za rais 2025 kanda ya ziwa.
😂😂😂😄😄😀😅🤣🤣🔥🔥
 
Humu ndani ndo maana Samia alisema huwa akisoma anacheka sana....
Yaani mtu anaandika gazeti based on assumptions za kichwa chake na watu wanaanza kubishana au kumuunga mkono...
Yoote haya Samia ukute na yeye anasoma Kama story Tu za kubuni ndo maana akisoma anacheka ..
 
Humu ndani ndo maana Samia alisema huwa akisoma anacheza sana....
Yaani mtu anaandika gazeti based on assumptions za kichwa chake na watu wanaanza kubishana au kumuunga mkono...
Yoote haya Samia ukute na yeye anasoma Kama story Tu za kubuni ndo maana akisoma anacheka ..
Uzi uishie hapa kifupi mleta uzi katoa mambo ya kufikirika akidhani ni kweli na watu wanakanyagana kusupport na kupinga.
 
Back
Top Bottom