MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za Uchaguzi Mkuu tokea tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Ieleweke kuwa Mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitumia jumla ya Shilingi 534,499,415,599/= katika zoezi zima la Uchaguzi Mkuu. Pesa kati ya hizo zilitolewa na Washirika wa Maendeleo ambao ni Umoja wa nchi za Ulaya, Uingereza na Marekani kupitia mradi wa DEP unaosimamiwa na UNDP ambapo pia walitoa vifaa kwa ajili ya uchaguzi na pia ukarabati wa Kituo cha Kuchakata taarifa za Wapiga Kura (Data Processing Center).
Kuanzia sasa mpaka Uchaguzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) inatarajia kutumia shilingi bilioni 331.7 kukamilisha zoezi la Uchaguzi Mkuu ambapo fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.
Hii itakuwa ni dhana ya kujitegemea ambayo faida yake ni kuwa na uhuru wa kuamua namna ya kuendesha uchaguzi bila kuingiliwa kimaamuzi na Wanaochangia gharama za Uchaguzi!