Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,627
- 40,785
Tanzania sio Nchi Pekee duniani yenye wanyama hai na mazingira mazuri ya kuvutia watalii.
Kuna nchi mbali mbali duniani ambazo hazina wanyama wala mazingira mazuri ya kuvutia lakini zinapata watalii kwa mamilioni kwa mwaka.
Mfano Mzuri ni Nchi kama Ufaransa watu wanakwenda pale kuangalia tu ule mnara unaoitwa Eifel Tower wine nzuri na mambo mengine.
Uingereza wana lile daraja lao la London (london bridge) , Makasri ya Zamani ya kifalme (windsor castle), Morocco fukwe za jiji la Cassablanca, Misri Mapiramidi n.k.
Kuna nchi pia zenye mbuga za wanyama kama Kenya, Afrika Kusini, Namibia etc.
Hivyo basi kwakua sisi tuna wanyama hai na mazingira mazuri ya utalii hiki kisiwe kitu pekee cha kujivunia bali tutafute upekee na katika upekee huo tuubrand na kututambulisha katika huo tusibweteke kwa kuwa na wanyama hai tu. Inabidi tufanye zaidi ya hapo.
Sekta ya utalii ni ngumu sana na haiwezi kutufanya washindi kwa kutengeneza filamu pekee.
Nchi kama Thailand haina wanyama lakini ina watalii kwa mamilioni kwa mwaka wanaofuata starehe katika mji wa Pataya.
Misri hawana wanyama ila wana mapiramidi ambayo kwa upekee wake huvutia watalii lukuki.
Sisi Tanzania ukiachana ma Wanyama hai na mazingira mazuri tuna nini cha ziada cha kuwafanya watu wasiende huko kwenye mapiramidi au kuponda raha huko Thailand wakaja kwetu kuangalia wanyama hai.
Ni muda sasa tukatengeneza upekee wetu ili tujitofautishe na wengine na hatimaye kuwin soko la utalii, bila kufanya hivyo tutabakia na wanyama hai na mazingira mazuri yasiyokuwa na msaada kwetu.