Baada ya kuweka mtego kwa mchumba wangu nimegundua huko mbeleni naweza kumchoma kwa gunia la mkaa nikaishiwa kufungwa jela
Zikiwa zimebaki siku chache tuhitimishe safari yetu ya uchumba na kuingia kwenye ndoa takatifu lakini naamua kuvunja mahusiano ,najua ndugu jamaa na marafiki watashangaa lakini nahisi kuua huko mbeleni
Iko hivi mwaka mmoja na miezi miwili tuliingia kwenye mahusiano na binti au mwanamke miaka 25 kwa lengo la kuoana na ilikuwa imebaki miezi 4 tufunge ndoa
Najua kwa umri huo hawezi kukosa ex maana si bikira na sikuwahi kumuuliza historia ya maex wake maana haileti maana
Siku moja niliamua kupitia account zake za mitandao ya kijamii ingawa niliperuzi kwa comments za marafiki zake walizokuwa wakizitoa alipokuwa akipost picha nikagundua kupitia comment zile jamaa Fulani atakuwa ex wake maana zile comments zilikuwa si za kawaida
Basi nikachukua picha ya yule jamaa nikatengeneza account whasap kwa namba nyingine ya asiyoijua kuwa ni yangu
Nikajifanya ex wake nikamtext akajibu tena kwa kuniita jina la ex wake huyo si ni baada ya kuona picha yake
Akawa analaumu kwa nini nilimuacha bila sababu na nataka nini kwake?
Nikajifanya kumuomba msamaha na nikimkumbusha tumetoka mbali naye,hakuendelea kujibu akakaa kimya
Turudi Mimi mwenyewe ili niamini huyu mwanamke ana msimamo na hawezi kurudiana na ex wake nikafanya jambo
Jambo lenyewe nikasafiri ghafla na sikumuaga na nikazima simu na sikuwa online kwenye mitandao ya kijamii
Usiku nikajifanya ex wake nikaanza kukomaa turudiane,akawa anakataa,nilikomaa naye kuanzia saa 5 hadi saa 9 akawa amekataa
Katika maongezi yale ya siku hiyo ndo nikagundua jamaa amewahi kumpiga ujauzito wakachomoa
Basi kesho yake saa 8 mchana nikamuona online nikamfuata tena ,awamu hii hakuwa na nyodo akawa anajibu kwa ulaini
Nikachochea moto wa kubembeleza ,akanambia atanijibu baadae
Ikawa usiku kama saa 7 hivi nikawa namuona online muda mrefu bila kumtext ,akanitext "Mambo" nikareply haraka sana,nikamuuliza hujalala akajibu bado
Nikarudi kwenye mada ya kurudiana .Daah! Unajua akakubali na amesahau kuwa ni mke wa mtu wa hivi karibuni
Ila akanipa masharti kuwa tutarudiana na hata kama anaolewa mapenzi yetu yataendelea kama kawaida ila niwe na nidhamu kwenye ndoa yao,nimheshim mume wake,nikifanya hivyo hawataachana licha ya kuolewa,nikamwambia poa ,akaomba nimpe mchango wa harusi kama laki moja .
Moyo wangu umeamia sana kwa huyu mwanamke,nimerudi mjini nikawa hewani na kuomba msamaha wa kupotea siku mbili ila nawaza sana
Naamua kuvunja mahusiano .
Ushauri wenu jamani,kumbe kuna umuhimu wa kuoa bikira ,kumbe maex hawaachani?