Kwa kina kaka wenzangu wa JF..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kina kaka wenzangu wa JF.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ambassador, Jul 28, 2010.

 1. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Makaka sometimes inabidi nasi mara moja moja tuwe tunayatia mapenzi chachu hata kwa kufanya kakitu kadogo kuonyesha kuwa unamsaidia wife. Sio unakuta kaka mwingine yeye anachojua ni kufanyiwa tu kila kitu mfano:

  1. Unaamka asubuhi unamuamsha wife akakuwekee maji kwenye ndoo (na yanatoka bombani na ni master bedroom)
  2. Akuwekee dawa ya meno kwenye mswaki (asipoweka utaoga kisha utatoka kuja kuulizia mswaki wako)
  3. Unatoka bafuni (hapo utakuta pant yako umeivua umeitupia kwenye sink unasubiri aje aifue!)
  4. Ukitoka alishakupigia pasi, alishabrashi viatu unavaa, unakunywa chai alokuandalia kisha huyooo funguo za gari zi wapi na ukifika ndani ya gari ni honi mtindo mmoja anakuchelewesha, na asipokimbia na viatu mkononi unamuacha anakwenda ofisini kwa daladala au akifanikiwa kuingia kwenye gari basi utamsema njia nzima.

  MCHANA KUTWA HATA KUMPIGIA SIMU YA SALAMU AU SMS YA I MISS YOU!

  5. Ukirudi jioni ukute chai yako mezani na maji bafuni
  6. Utizame TV huku ukisubiri chakula au usome magazeti yako
  7. Ukishakula huyooo kitandani unalala huku ukisubiri yeye aje ashushe neti na kukufunika shuka!
  8. Aingie kitandani baada ya kumaliza kazi zake umdake tayari kwa chakula cha usiku.

  Life continues.......!

  Kwa style hii kweli unategemea mkeo atakuwa na mapenzi na wewe? Si atajihisi hana tofauti na huyo housegirl jamani!

  Mara moja moja ukimsaidia kushusha net au hata kumpigia na yeye pasi I tell you ataikumbuka kwa muda mrefu na moyo wake kukongwa vilivyo!!

  Tafakari, kama imekutachi chukua hatua......!
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wewe unamsaidia wife wako hizo kazi?
  By the way ni ushauri mzuri, nitaufanyia kazi nikishaoa!
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye bluu mdau yaelekea waishi Nyanda za Juu Kusini au Kanda ya Kaskazini....maana huku mikoa ya Pwani kuna joto sana na watu hawana tabia ya kunywa chai mchana au hata jioni.
   
 4. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusoma hii habari nimegundua mke wangu ana raha sana karibu asilimia 75 ya ulivyosema mimi uwa navifanya mwenyewe mpk kuweka net na gari kila mtu ana lake na mm wakati naondoka asubuhi yy uwa kautundika usingizi chai nakunywa ofisini. Nadhani itabidi nianze kumwamsha asubuhi awe ananiwekea dawa kwenye mswaki ili mradi kumsumbua hasije kuniona mume ***** bure
   
 5. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Of course, zaidi ya hayo.....!
   
 6. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Usimsumbue shemeji yangu kwa nia tu ya kujionyesha wewe kidume. Natumai shem atakuwa atakuwa anakupenda sana na kukurespect pia. Kazi kusaidiana, sio wewe ufanye zote au umtupie zote shemeji akufanyie.
   
 7. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huu ujumbe ni generic, kama wewe unaandaliwa kahawa, rubisi, mbege, madafu etc inaaply tu.
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280

  Well. Inategemea unaishi ktk mazingira gani. Hivi ni vitu vidogo sana ndani ya nyumba na sio issue sana kwa mtizamo wangu. Kama house maid yupo hivyo viatu, kupiga pasi nk lazima mama afanye?

  Mume ndie mwezeshaji wa yote kuanzia chakula, ada za watoto , matibabu , na gharama za familia kwa ujumla .Msaada anaoupata kwa mama na maid wake ni appreciation kwa jasho loote analotoka kuwaweka walivyo.

  Sasa kama baba nae ataanza kuchemsha maji ya kuogea jikoni , apige pasi, adeki nyumba n.k what will be the the woman responsibility in the family?

  Hayo mambo mengine ni ya kuiga tu na ambayo nao yamewashinda. Too theoretical to be precise. A good wife won't let the husband to do house chores. A just married couple may think that is a sign of love, in my opinion it is rather the opposite .
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Naomba kule ta hoja ikiwa namba 1, 4 na 5 vinafanywa na house girl wenu na vyote vilivyobaki ndo wavifanya wewe.....................?

  Swali la nyongeza, Mh Teamo.................(kumbe hajafika hapa)
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Labda mimi niulize katika staili tofauti,.... Hivi wanaume na wanawake wa namna hiyo bado wapo katika dunia hii na hasa hasa katika mazingira ya mjini?

  Wife wangu hana obligation ya kufanya lolote kati ya hayo isipokuwa kuna mengine mengi tu mimi namfanyia yeye au tanafanya wote mfano 3, 4 na 7.
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Ambassador, kwa hisani ya watu wa marekani....wewe ni he ama she? tuanzie hapo kwanza...
   
 12. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,751
  Trophy Points: 280

  hivi bado kuna wanaume wa aina hii katika kizazi hiki???
   
 13. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huyo make au robot... nadhani mke ni mwenzako wa maisha na ni vema kusaidiana pale panawezekana.... japo kuna wanawake wengine wakishapata msaada wa kazi fulani huwa'wanajisahau' na kudha ishakuwa wajibu wa kidume na hapo ndo tatizo huanza. Atadeka, na ukiomba ufanyiwe hiki, atakuambia mbona mara ya mwisho ulifanya wewe!!
   
 14. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  I wonder ! Just Grab ur Sweetie and go somewhere to have fun , Life is too short enjoy to the fullest every minute u have on earth !!
   
 15. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ndoa ni makubaliano. Kama mamaa yuko tayari kufanya hayo yote, mzee ukapata haki yako shida iko wapi?
   
 16. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,542
  Likes Received: 2,240
  Trophy Points: 280
  Mfamaji umenena!Ila inaelekea Mr Ambassador inaelekea huko nyuma ilikuwa tabia yako umepata kanseling unaona utuletee matrio uliyopata huko kwa akina Tgnp!!Mimisina chakuongezea Kwani Mfamaji kamaliza:focus:
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Na bado kuna wanawake wa namna hiyo? Tena wanafanyakazi na kuingiza kipato? Naona mleta mada amechanganya mandhari. Kwa uswazi inawezekana! Ila kwa couple ambayo wote wanafanyakazi hadi wana uwezo wa kusafiri hii kitu haiwezekani tena hata mke akipenda kufanya hivyo!

  Ulianza vizuri tu (blue) ila hapo kwenye red umeharibu. Inaonekana una-support suala la kusaidiana katika ndoa ila bado unaamini kuwa kazi za ndani zote ni wajibu wa mwanamke. Hapo bado kuna katatizo kadogo!
   
 18. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Umesoma subject vizuri Kaizer?
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  namshukuru my sweet darling ananisaidia ingawa sio kwa 100% lakini lazima sifa na utukufu nimrudishie mwenyezi mungu kwa hili
  Kuna wakati naambia wife leo tulia majukumu ya hapa nakusidia ...woooh wakati mwingine huwa nashangaa moyoni nashindwa kuyatoa mdomoni..nisije haribu na msaada ukakoma:tea::A S-heart-2:
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hivi wanawake wa hivyo bado wapo?
  Mimi wa kwangu kutachimbika nikimfanyia hayo....
   
Loading...