Kwa kasi ya Mchina na Electric Vehicles (EV), sio muda tutapishana nazo Dar

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,094
49,859
Wakuu, tukubali magari ya umeme yanazidi kuongezeka kwa kasi sana ndani ya hii miaka mitano. Na inavoelekea yatazidi kuongezeka maradufu. Mfano tu angalia hii chart nimeitoa Wikipedia.

Global_plug-in_car_sales_since_2011.png

Sasa kwa rate hii, nina imani na Tanzania sio muda tutaonesha ubabe wa kuagiza hizi chuma.

Mchawi ni gharama na Watu kuogopa issue ya mafundi.

Tukianza na gharama, sasa imekua sio issue tena.

Makampuni makongwe kama Tesla, wana offer gari mpya kwa bei kubwa sana unakuta Model 3 inauzwa $60,000/= mpya. Ukinunua used ndio unakuta $35,000/= kabla ya TRA. Bado yamoto sana.

Hawa Wachina BYD wamekuja kusolve issue ya bei kwa kutuletea gari mpya hadi ya $13,000/= imagine.

Hawa jamaa mwaka jana wameajiri mainjinia zaidi ya 20,000 kwenye Research & Development Department tu. Hii inamaanisha vitu vingi vizuri vipo njiani.

Mwaka huu 2024 wamekuja na hii gari BYD e2 Honor Edition kea bei ya $13,000/= tu.

BYD_e2_facelift_01_China_2023-04-17.jpg
arenaev_003.jpg
arenaev_005.jpg

Theoretically hadi sasa ikiwa full charge inatembea Kilometa 400, Motor 70kW, Battery 4.9kWh, maximum speed ni 130 kph, Output power 94HP, uzito wake 1340 kg, Fast Charge 0.5 hours na Slow charger 6 hours izo ni baadhi.

Sasa kama serikali yetu sikivu kupitia TRA wakafanya mchakato kama walivyohaidi kwamba magari ya umeme yatakua na ushuru bure basi itapendeza sana.
Screenshot_20240316-114053.png

Watu watajiripua, tutaenjoy magari mazuri bila makelele mengi njiani na eco friendly.

Pia serikali ingeanza kwa kuonesha mfano kwa kuingiza mabasi ya Mwendokasi yawe ya umeme na magari ya baadhi ya mashirika yawe ya umeme, mfano posta delivery ya mizigo mjini.
 
Mwanangu Mad Max sijui unapendea nini haya magari!! Japokuwa ulimwenguni unaenda kwenye EV's kwangu Mimi bado natamani combustion engine ziendelee kutengenezwa..
haya magari ya UMEME Kwa maisha yetu ya kiafrica naona kama bado sio rafiki kwetu, ndiyo maana kampuni ya Toyota wamependekeza Kwa manufacturers wawekeze kwenye hydrogen fuel( eco friendly) pia ni zero emissions kama UMEME Tu

Technology ya hydrogen fuel ni kama ilivyo petroleum na diesel engine.... Najua baada ya miaka 10 mbele Tanzania tutakuwa tunatumia magari ya kichina kwasababu ya bei zake chini pia serikali Yao wamedhamiria kuteka soko lote la Asia, Latin America na Africa Kwa kuingiza magari yao
 
Aisee, sijui kuhusu Hydrogen ila gari la umeme lina mzuka wake. Sijawahi kuendesha, ila kuna week nilikua na Prius zile za 2010 ambayo ni Hybrid.

Sasa ukiiwasha ukawa unaendesha slow hafu ukaweka EV mode aisee inakuambia Ready ila engine iko OFF pale ni full umeme. Ile experience ilinibadirisha kabisa issue ya ICE kabisa. Yaani gari inaenda ova inavutwa hausikii kelele no sauti ya exhaust yaani kimyaa.

Nikasema hapa sasa Tesla itakuaje? Imagine unaendesha Model 3 gari ndani ilivyo, unachaji chuma inaenda kilometa 500+ hamna kubadirisha engine oil wala gearbox oil sijui.

images (7).jpeg

Pia hivi vidude ndani viko plain simple hadi raha. Sipendi magari yapo complicated ndani ova cockpit ya F22 Raptor.
 
View attachment 2936143

Dunia ndiko inakoelekea huku hatuna ujanja wa kukataa magari ya UMEME Acha tuendelee kutafuta pesa Tu ya kununua
 
Kuna pesa nyingi ikitokea vijana kwenda kusoma na kuelewa mifumo ya hizi gari za umeme na hizi hybrid.
Mwanzoni kabla hata mafundi wengi hawajazinduka lazima upige vibunda vya kutosha.
Tatizo investment hatutaki wengi. Mtu ukasome kazo course ya kudeal na hybrid na EV hafu urudi utawashika sana. Mfano sahivi nishaziona sana Prius, Aqua, Honda Fit na Insight ambazo ni Hybrid
 
Aisee, sijui kuhusu Hydrogen ila gari la umeme lina mzuka wake. Sijawahi kuendesha, ila kuna week nilikua na Prius zile za 2010 ambayo ni Hybrid.

Sasa ukiiwasha ukawa unaendesha slow hafu ukaweka EV mode aisee inakuambia Ready ila engine iko OFF pale ni full umeme. Ile experience ilinibadirisha kabisa issue ya ICE kabisa. Yaani gari inaenda ova inavutwa hausikii kelele no sauti ya exhaust yaani kimyaa.

Nikasema hapa sasa Tesla itakuaje? Imagine unaendesha Model 3 gari ndani ilivyo, unachaji chuma inaenda kilometa 500+ hamna kubadirisha engine oil wala gearbox oil sijui.

View attachment 2936143

Pia hivi vidude ndani viko plain simple hadi raha. Sipendi magari yapo complicated ndani ova cockpit ya F22 Raptor.
Aisee. I can imagine. Nina 0 exp na EV.

Sijui itakuaje pale mji mzima hakuna sauti za gari ila gari zinapita, na hawa ndugu zetu wa boda wakiletewa za umeme ndo itakuwa kuvunjana bila makelele maana hutamsikia akija huko na maspeed.
 
Hahaha hizi za engine bado zipo zipo sana. Ila kuna baadhi ya nchi wana mikakati kufika 2030 hakuna gari la engine kuuzwa au kua imported. Kwahiyo yaliyopo yatabaki ivo ivo hadi yachakae.

Pia kuna mahala nimesoma baadhi ya nchi Ulaya magari ya umeme yanapewa offa mfano free parking au nusu Bei, kwenye vivuko (mfano Kigamboni) wanapita bure au kwa discount, wakati wenye engine wanazidi ongezewa Makodi.
 
Tatizo investment hatutaki wengi. Mtu ukasome kazo course ya kudeal na hybrid na EV hafu urudi utawashika sana. Mfano sahivi nishaziona sana Prius, Aqua, Honda Fit na Insight ambazo ni Hybrid
Ni sahihi mkuu, mafundi wakiji update ku deal na hizo motor watapiga marundo sana kabla wajuaji hawajaingilia kati, ni kazi ambayo mtu anakuja na gari unamuambia bei huku umeketi kwenye kiti na umeweka miguu juu ya meza huku unabofya na simu.

Wabongo walivyo lala utashangaa wachina wanatoka kwao Asia huko wanakuja fungua garage ya kufanya maintenance za EV hapa bongo.
 
Hahaha hizi za engine bado zipo zipo sana. Ila kuna baadhi ya nchi wana mikakati kufika 2030 hakuna gari la engine kuuzwa au kua imported. Kwahiyo yaliyopo yatabaki ivo ivo hadi yachakae.

Pia kuna mahala nimesoma baadhi ya nchi Ulaya magari ya umeme yanapewa offa mfano free parking au nusu Bei, kwenye vivuko (mfano Kigamboni) wanapita bure au kwa discount, wakati wenye engine wanazidi ongezewa Makodi.
Watuletee huku Africa hayo magari maana 20230 karibia nchi zote za ulaya watakuwa wanatumia EV's
Nahisi combustion engine yatakuwa cheap zaidi 2030 maana hayatakuwa na soko zaidi ya huku Africa
 
Hydrogen is one of the most abundant element and is the future of energy in transportation.
EV is just another scam like others..ukifuatilia ev vehicles Zina uharibifu zaidi wamazingira kwa kupima vyanzo vya betri zake, disposal na upatikanaji wa madini yanayotumika katika uundani wake na source ya umeme unaotumika.

Toyota hili wamelitambua mapema..
 
Watuletee huku Africa hayo magari maana 2030 karibia nchi zote za ulaya watakuwa wanatumia EV's
Nahisi combustion engine yatakuwa cheap zaidi 2030 maana hayatakuwa na soko zaidi ya huku Africa
Mchawi bei ya uendeshaji. Ukikaa na gari la Engine miaka mitatu na mwenzako wa umeme, kwa matumizi yanayokaribia kuendana, Wa gari la Umeme anasave saaaaaaaana.
 
Mchina anarahisisha maisha
Tuanze na gas cng cars ,magari ya umeme Kwa Tanzania hayafai kwanza gharama pili cost ya replacement ya betri mtohani .Sababu hiyo betri ni kama ya simu tu Ina expire baada ya muda kubadili betri mpya Bei yake karibu nusu ya hei ya kunumua hiyo gari ya umeme

Ndio maana hizo chart mleta mada kaweka ni za nchi Tajiri tu ndiko mauzo yameongezeka sana
 
Hydrogen is one of the most abundant element and is the future of energy in transportation.
EV is just another scam like others..ukifuatilia ev vehicles Zina uharibifu zaidi wamazingira kwa kupima vyanzo vya betri zake, disposal na upatikanaji wa madini yanayotumika katika uundani wake na source ya umeme unaotumika.

Toyota hili wamelitambua mapema..
Hapo nimekuelewa kwenye issue ya mazingira. Ila mchawi imebaki muamko wa Makampuni katika utengezaji wa hayo magari. Mfano nilisoma makala flani hadi 2023 magari ya Hydrogen (FCEVs) yalikua Elfu 70 tu barabarani.
 
Hahaha hizi za engine bado zipo zipo sana. Ila kuna baadhi ya nchi wana mikakati kufika 2030 hakuna gari la engine kuuzwa au kua imported. Kwahiyo yaliyopo yatabaki ivo ivo hadi yachakae.

Pia kuna mahala nimesoma baadhi ya nchi Ulaya magari ya umeme yanapewa offa mfano free parking au nusu Bei, kwenye vivuko (mfano Kigamboni) wanapita bure au kwa discount, wakati wenye engine wanazidi ongezewa Makodi.
Nchi zinazoongozwa na watu wasiotegemea magari kukusanya kodi. Hapo lazima watu mtaachana na petrdisel
 
Aisee, sijui kuhusu Hydrogen ila gari la umeme lina mzuka wake. Sijawahi kuendesha, ila kuna week nilikua na Prius zile za 2010 ambayo ni Hybrid.

Sasa ukiiwasha ukawa unaendesha slow hafu ukaweka EV mode aisee inakuambia Ready ila engine iko OFF pale ni full umeme. Ile experience ilinibadirisha kabisa issue ya ICE kabisa. Yaani gari inaenda ova inavutwa hausikii kelele no sauti ya exhaust yaani kimyaa.

Nikasema hapa sasa Tesla itakuaje? Imagine unaendesha Model 3 gari ndani ilivyo, unachaji chuma inaenda kilometa 500+ hamna kubadirisha engine oil wala gearbox oil sijui.

View attachment 2936143

Pia hivi vidude ndani viko plain simple hadi raha. Sipendi magari yapo complicated ndani ova cockpit ya F22 Raptor.
Mchina ka copy Kwa testla kila kitu aided😂
 
Back
Top Bottom