Kwa kadi ya Makonda, CCM inaelekea kuvurugika!

Kwa kadi ya Makonda, CCM inaelekea kuvurugika!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,643
Reaction score
14,642
Kwa uteuzi, matamshi na hasa kama kuwaumbua viongozi wakuu nchini, Makonda anaenda kukisambaratisha chama CCM.

Kwa sasa Makonda kampa Waziri Mkuu miezi sita kutekeleza majukumu yake.

Kiprotokali Makonda ni mdogo sana, hawezi kumwamrisha Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anasimamiwa na Mama Samia kama Mwenyekiti wa CCM na kama Rsis wa nchi.

Na hata ndani ya chama, kuna vikao mahsusi ya kuzungumzia utendaji wa serikali, vikao hivyo havijatumika.

Sasa, aidha Makonda katumwa na Mama Samia, au ni kiherehere chake tu.

Lakini kwa vyovyote kutakuwa na consequences.

Wanaokuwa lambasted hadharani sitegemei kuwa watakaa kimya.

Chama kinaenda kusambaratika na 2025 si mbali.
 
Kwanza mi naona yupo sahihi kidogo ataludisha watu kwene majukum yao,, kama hujuw mama anaona haya kuwaeleza wasaidiz wake,, akaona amtumie makonda kuwanyoosha, usione makonda analopoka tu,, unazan yupo kizembe tu et? Like msiba kipnd kile,,
 
Deep state wanaakili sana!

Baada ya kumtumia konda boy enzi zile na kufanikisha sasa wanamtumia tena kwa mara nyingine wanamtumia kumalizia mission nyingine!!!

Taharuki atakayozua itasababisa kuleta hofu ya kisiasa na kiutawala na awam ambayo itabidi mabaka watishie kuingia mzigoni kabla ya hapo Busara pekee itakua kuitosa namba sita baharini Ili bahari itulie na itatulia baada ya namba sita kutoswa!!

Maoni huru haya ya mlipa kodi.asiekwepa!!
 
Hivi nyie mnaijua CCM vizuri kabisa, hachana kabisa na mikakati yao ya kichama, jamaa wanajua Sana kutengeneza drama za siasa na hapo ni mwanzo tu.

Jamaa ni hatari Sana kwenye kuwaadaa wananchi, mikakati yao ni hatari utawaona wanatupiana mabango jukwani lkn lengo lao wao ndo wanalolijua kwaufupi salute to CCM.
 
Protocol gani? Hakuna mtu mkubwa TZ zaidi ta CCM, je waziri mkuu anacheo gani CCM je mkubwa kuliko Paul makonda?

Wew Paul makonda bosi wake ni Mwenye kiti, makalu, katibu wa CCM basi?.Uchaguzi wa Rais,wabunge. PAUL MAKONDA NI ndio wanao pendekeza wagombea mpaka Rais
 
Back
Top Bottom