Kwa jinsi RC Makonda anavyotukanwa sasa na Wakenya huko Mitandaoni Kwao nashauri Siasa isiingizwe Michezoni

Wahadzabe hawafananishwi na wagogo... mhadzabe akianza tabia za kigogo inatia mashaka sana...
Jiongeze si kila kitu utafuniwe...
Ni upuuzi wa kiwango cha unayemuhusudu maishani mwako, kujenga hoja kwa kunasibishwa na kabila la mtu, hasa hoja za kimantiki!
 
Tatizo la serikali ya awamu hii ni kuingiza siasa za ki-CCM kila mahali wakidhani ni sifa kumbe ni ujinga tu. Expertism is replaced with stupid politics!
 
Mtiririko wa uandishi wake utauelewa ingawa anajitahid kutofautisha
Na hata id na avatar vinajieleza huwa anapenda sana kutumia hivyo vitu
Umetumia microscope gani kung'amua hilo mkuu maana huo utaalamu natamani ningekua nao ili niwe nawatambua watu flani wenye "vitambulisho" zaidi ya kimoja?
 
Ndani ya Dakika 55 tokea Filimbi ya mwisho ipulizwe na Kumalizika kwa Mtanange kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania ambapo Tanzania ( Taifa Stars ) tumefungwa kama kuna Kiongozi wa Tanzania ambaye sasa anatukanwa, kudhihakiwa na kukashifiwa katika Mitandao ya Wakenya hadi anatia huruma basi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda.

Nashauri naomba kuanzia sasa Viongozi hawa wa Siasa nchini Tanzania wasiwe wanahusishwa au wanajiingiza katika Siasa huku wakiwa bado wanazitumikia hizo Nyadhifa zao kwani pale wakiwa wanatukanwa sidhani kama hayo Matusi huwa yanaishia tu Kwao bali huja hadi na kwa Sisi Wananchi wa kawaida tu ambao hatuna hatia yoyote ile.

Makonda Siku zingine uwe unaacha kuwa na Kiherehere, Dharau na Sifa kwa unazidi tu Kuumbuka.
Si na wakenya tu,hata wabongo wenziye katuudhi sana.Mtu mwenyewe "yupo yupo" tu na misifa yake unategemea timu ifanikiwe???!!!! Eti "mungu" wa dar es salaam! Haya sasa na uungu wake.
 
Back
Top Bottom