MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 816
Mh Mnyika amebakisha huku kwetu Changanyikeni. Bado tunachanganywa na kuchanganyikiwa na shida ya maji
Atafika tu, hajamaliza hata nusu ya miaka 5 mliyompa!
Mh Mnyika amebakisha huku kwetu Changanyikeni. Bado tunachanganywa na kuchanganyikiwa na shida ya maji
Amkeni Watanzania mradi wa maji Dar... hauhusisiani na Mbunge yeyote.Mh Mnyika amebakisha huku kwetu Changanyikeni. Bado tunachanganywa na kuchanganyikiwa na shida ya maji
Mh Mnyika amebakisha huku kwetu Changanyikeni. Bado tunachanganywa na kuchanganyikiwa na shida ya maji
Wewe inaonekana hauishi kwenye jimbo la Ubungo.......biashara ya maji ipo palepale.....tena mara 17 zaidi ya bei ya Dawasco.........na sababu za kutopatikana ziko wazi........tumejaribu kumshauri mbunge wetu lakini bado anapiga siasa..........anyway shida ya maji bado ipo palepale......ninasubiri kumuadabisha....ndiyo uwezo nilionaoLeo ndio nimestuka na kuanza kujiuliza wapi yalipo yale magari ya akina Mringo na wenzake ambayo yalifikia mahali cha kutukosesha amani ya usalama wa watoto wetu kwa kila dakika kupita mitaani huku Kimara yakifanya biashara ya Maji? Tulizoea kuyaona magari mengi sana ya kuuza maji ambapo leo ni vigumu sana kuyaona yakifanya biashara hiyo.
Kila mwenye pesa yake wakati huo Kimara hakuwa ameona biashara nyingine ya kufanya zaidi ya kuuza maji maana ndiyo biashara iliyokuwa maarufu sana na inatoka sana huku Kimara.
Leo hii wengi wameshabadilisha matumizi ya magari yale kwa kukosa wateja kwani tatizo la Maji Kimara limepungua kwa kiwango kikubwa sana kama si kukaribia kwisha.
Je waliomtangulia akina Keenja, Ngula n.k walishindwa kabisa kuona kwamba hiki kitu kinawezekana kiasi cha kuwaruhusu akina Diwani(CCM) Mringo kupata utajiri kwa biashara hiyo huku wakifanya kila jitihada maji yasipatikane Kimara ili wao wauze?
Heko JJ. Mnyika, Mbunge wangu.
Wewe inaonekana hauishi kwenye jimbo la Ubungo.......biashara ya maji ipo palepale.....tena mara 17 zaidi ya bei ya Dawasco.........na sababu za kutopatikana ziko wazi........tumejaribu kumshauri mbunge wetu lakini bado anapiga siasa..........anyway shida ya maji bado ipo palepale......ninasubiri kumuadabisha....ndiyo uwezo nilionao
hapana, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.. Mh. Mnyika pamoja na jitihada zake lkn suala la maji bado ni suala tete. Jimboni kwa Mh bado tatizo la maji ni endelevu..hasa maeneo ya Mbezi Msuguri, Bwaloni, St. Anne na Masaki, nk ni kweli hayana maji hata ule mgao wa mara moja kwa mwezi. Istoshe, hakuna dalili za upatikanaji wa maji pengine mpaka magamba watoke madarakani... manake kwenye kikao cha bunge kilichoisha Mh. Mnyika alitaka kuleta motion bungeni juu ya maji, hasa 'bomba la mchina' lkn spika akisaidiana na Prof aliyeshindwa kuendesha wizara wakamchakachua! Nafikiri wananchi hatuna budi sasa kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo la maji sisi wenyewe au tuendelee kusubiri hadi 2015
huyo ndo JJ, sikujali usingizi wangu kukesha kwa ajili ya kulinda kura zake...
kimara ipi mkuu mbona tembon.kwa msuguri.kibanda cha mkaa.suka.stop ove.bunyokwa.king'ongo.bwalon na nk bado watu wanafanya biashara sana tu.na maji hakuna
Mh Albedo
Kama unaishi jimbo la Ubungo usingeniuliza hilo swali......kukupa uelewa mzuri ni hivi....kwa kiasi kikubwa Ubungo hakuna shida ya maji yaani hakuna mtu anayekufa kwa kukosa maji...ila shida ya ubungo ni kupatikana maji kwa bei kubwa mno....mara 16 ya bei ya DAWASCO na sababu za kupata kwa gharama kubwa hivyo inajulikana......hata mh wetu anajua....kuna wakati nilisema hapa jamvini kuwa tutamuuliza mh wetu amelipwa ngapi na wafanyabiashara wa maji wengi walipiga kelele hapa......kama nivyokueleza mwanzo kama unaishi jimbo la Ubungo usingeniuliza hilo swali ambalo karibu kila mwaUbungo anajua jibu lake
2015 ya nini??? Amekuwa akitueleza michakato na mipango isiyoisha......haina matokeo.....kama ameshindwa kutatatua tatizo la maji jimboni angeitisha kikao na kuishtaki serikali kwetu tujue cha kufanya....lakini hajafanya hivyo hadi sasa...lakini bado anayo nafasi......kama hakufanya utafiti kwanini alichaguliwa basi ajue 90% ya kura alizopata ni kutokana na kero ya maji ambayo aliahidi kuitatua.....huku ubungo kwa taarifa yako barabara tunachangisha mafuta kwa kupitia serikali ya mtaa tunaomba greda tunarekebisha barabara siku zinaenda tena wakati mwingine bila hata mbunge wetu kujua.....tunamuachia muda afanye majukumu mengine mazito.....lakini hili la maji....tena miundo mbinu ipo....tunasikitika sana tunapoyakosa.......anyway wana Ubungo hawapigii kura JF
mtanzania1.unaish ubungo ipi mm hapa ndio natoka job nasubiri gari la maji hapa kibanda nikajiuliza wanao sema kuna maji vp .jf tuwe wakweli sote ni wa tz tunajenga nyumba1 sio cdm na ccd