Amiliki
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,085
- 1,005
Leo ndio nimestuka na kuanza kujiuliza wapi yalipo yale magari ya akina Mringo na wenzake ambayo yalifikia mahali cha kutukosesha amani ya usalama wa watoto wetu kwa kila dakika kupita mitaani huku Kimara yakifanya biashara ya Maji? Tulizoea kuyaona magari mengi sana ya kuuza maji ambapo leo ni vigumu sana kuyaona yakifanya biashara hiyo.
Kila mwenye pesa yake wakati huo Kimara hakuwa ameona biashara nyingine ya kufanya zaidi ya kuuza maji maana ndiyo biashara iliyokuwa maarufu sana na inatoka sana huku Kimara.
Leo hii wengi wameshabadilisha matumizi ya magari yale kwa kukosa wateja kwani tatizo la Maji Kimara limepungua kwa kiwango kikubwa sana kama si kukaribia kwisha.
Je waliomtangulia akina Keenja, Ngula n.k walishindwa kabisa kuona kwamba hiki kitu kinawezekana kiasi cha kuwaruhusu akina Diwani(CCM) Mringo kupata utajiri kwa biashara hiyo huku wakifanya kila jitihada maji yasipatikane Kimara ili wao wauze?
Heko JJ. Mnyika, Mbunge wangu.