Kwa hili wazo Vodacom,Tigo,Airtel na Halotel Mnasemaje? Tufaidike sote

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Wadau. Mimi ni mmoja ya watu ambao huwa tunapata muda wa kufikiri. Mara nyingi nikiwa nmeshamaliza kazi zangu za ujenzi wa Taifa. Nmekula na Kunywa napata angalau masaa kadhaa ya kufikiri.

Nmekuja pata ideas kadhaa za namna ya kufanya kazi na haya makampuni ya Simu. Sasa wasiwasi wangu ni je nifanye nini ili nisije ongea nao wakaiba Idea yangu na kuifanyia kazi mimi nikabaki kusema tu "ilikuwa ya kwangu hii"

Naomba tuelimishane namna ambayo naweza either wauzia idea au fanya nao kazi pasipo wao kuniibia. Tufaidike sote. Nami nina familia na ninatumia kichwa changu kufikiri.
 
Back
Top Bottom