Salaam ndugu zangu.
Ni juzi tu UDOM wametoa majina ya watu wa kwenda kufanya usahili kwa kada za wanataaluma na waendeshaji. Kilichonifurahisha kuhusu UDOM kwa mara hii ni hiki; wametoa mambo ya ubaguzi wa vyuo, kwa kada za wakufunzi wameita watu waliokuwa na vigezo kutoka karibia vyuo vyote hapa Tanzania. Nimeona walioitwa kwenye usahili kwa kada za ukufunzi kutoka chuo cha mipango, St. Jonh's University, RUCO, MUCCoBs, St. Augustine n.k.
UDOM wameonyesha utofauti na chuo kama UDSM ambao wanaubaguzi sana, mana hata ukisoma Mzumbe basi jua huwezi kuwa mhadhiri wa UDSM! wao wanaamini product zao tu, lakini si kweli kwamba wanafunzi wao ndiyo bora kuliko wanaosoma vyuo vingine. Haya mambo yamekuja kugundulika baada ya tume ya utumishi wa umma kusimamia usahili kwenye taasisi za Umma! Kwa mfano, asilimia kubwa ya watu walioajiriwa na tume ya utumishi wa Umma kama assistant lectures au tutorials kwenye vyuo vya Umma kama CBE, IFM na IRDP hawajatokea UDSM! Kuna baadhi ya interview wanafunzi waliosoma UDSM walikuwa wanagalagazwa hadi unakuta hakuna mtu hata mmoja aliyepita kwenye written interview.
Vijana ambao mwanzo walikuwa hawapewi nafasi toka vyuo kama IAA, TIA na IFM wamekuwa waking'aa sana! Na subirini muone hao watakaoenda kupambana uko UDOM jinsi vijana kutoka vyuo vingine watakavyoong'aa! Hongereni UDOM kwa kutaka kupima uwezo wa wafanyakazi wao kwa kuangalia qualifications zao na si chuo walichotoka!