Ni hakika kuwa mifuko ya pensheni iko mingi hapa Tanzania.
Kila mfuko umekuwa ukijitahidi kubuni namna bora ya kuvuta wanachama. Mbinu niyngi zimekuwa zikitumika, zikiwamo hata zisizokuwa na ukweli, ili muradi tu, wapatikane wanachama na kuendelea kuchangia.
Hata hivyo, bila kuwa na hisa wala maslahi binafsi, napenda kuweka wazi kuwa PSPF ni mfuko unaostahili sifa kubwa kutokana na namna unafanya kazi.
Hawa PSPF wamekuwa wakija na ubunifu wa aina mbalimbali na katika uchunguzi wangu, nimeona hawa ndiyo wanaongoza kwa kuwapa wanachama wao kile kinachostahili.
Mengi yamekuwa yakifanywa, lakini hili la kutoa mafunzo kwa wastaafu watarajiwa, kwa kweli ni jema na hakika linaleta faraja.
Hongereni sana PSPF.