Kwa hili, PSPF ni mfuko bora zaidi

Kwa hili, PSPF ni mfuko bora zaidi

Mimi ni shuhuda, kweli PSPF wanastaili pongezi kwa huduma zao mbalimbali ikiwemo malipo ya kila mwezi kwa Wastaafu bila kuchelewesha, hakika ni TULIZO LA WASTAAFU.
 
viazi tu hao mke wangu kajifungua mpk mtoto anatembea hawajamlipa fao la uzazi ukiwauliza wanapiga story za utapeli ukisikia matangazo yao kama pepon hamna kitu wezi hao kaa nao mbali
 
PSPF hawana dhamira ya kuwakwamua wachangiaji wake.

lazima wabadilike kulingana na wakati wa sasa, kama hakuna fao la kujitoa basi waangalie namna nyine ya kuwasaidia wafanya kazi ili wajikwamue kimaisha.

haiwezekani unampa mtumishi mafao yake karibia anakufa, nguvu hana ndio mnampa mafao yake hiyo si haki.

wekeni utaratibu wa kutoa mikopo(cash) iwasaidie wanachama kujiendeleza kibiashara sio kuwakopesha nyumba, wengine wanataka kufanya biashara wapeni mikopo.

PSPF BADILIKENI!
 
Kwani sijatoa sababu? Hilo la kuwalipa Wastaafu pensheni zao kila mwezi bila kuchelewesha sio sababu?
 
Kwani sijatoa sababu? Hilo la kuwalipa Wastaafu pensheni zao kila mwezi bila kuchelewesha sio sababu?
Wawalipe wafanyakazi wastaafu wa utafiti TARO na TALIRO kama guidelines za SSRA inavyopendekeza ndio tutawaona wana tenda haki. Wengi wa wafanyakazi waliokua utafiti wamekatwa miaka 7 bila maelezo. Wengi wao wameshakufa bila kupata haki zao. Hata Ukiwaandikia barua hawajibu. Hili ni shirika la serikali kweli? Hichi kiburi wanakitoa wapi? Hawastahili hizo sifa.
 
Wewe naona unaleta tu promo ya PSPF, hakuna jipya kwa hao jamaa. Chenga sana
 
YAANI C PSPF WALA LAPF WOTE WAZUGAJI TU.WANAWASUMBUA SANA WAKE ZETU JUU YA FAO LA UZAZI
 
Back
Top Bottom