Kwa hili nani alaumiwe?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
422
1,000
"Naomba mia, naomba hela ya kula, shikamoo! Mzazi leo nimelala nikihesabu mapaa na mitambaa panya. Naomba msaada! Nisaidie...." Hayo ndiyo maneno yanayotawala kundi ambalo linaendelea kuwa kubwa la kizazi cha leo. Kundi hilo limesahaulika kana kwamba jamii haioni. Ni lugha inayosikika na inayoendelea kuenea katika miji mikubwa na midogo, na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko ya watu. Ukitaka kujua ni nani wanaotoa kilio hicho kila kukicha, basi siku moja ubahatike kukutana na mtoto mmojawapo kati ya kundi la watoto wanaoitwa wa mitaani utayaamini hayo yanayosemwa.

hali hiyo waliyonayo siyo kwamba wameitaka iwasibu, la hasha! Imewapata kutokana na mlolongo wa mambo yanayochangia hali hiyo kutokea. Kuayaeleza yote mengine nitayatia chumvi, lakini umaskini kutamalaki katika familia zetu ni mojawapo. Aidha uzazi usiotarajiwa na pengine katika umri mdogo, ukosefu wa elimu, kuvunjika kwa ndoa na kubwa zaidi gonjwa la UKIMWI lililotapakaa nalo limeongeza tatizo hili kuwa kubwa.

Kilio cha kundi hilo kingesikilizwa kungekuwa na ahueni, lakini wapi? Watoto hao wanaambulia kubakwa na kulawitiwa. Tiba zenyewe hawapati, na kuhusu elimu kwao inakuwa ni njozi za ni vigumu kutekelezwa. Hatimaye, kundi hilo linapokosa matumaini, basi dawa za kulevya, pombe na wizi vinakuwa ndilo kimbilio lao.

Kila mwananchi, wewe na mimi tunapowaona wahusika hao tunamtupia fulani mpira huo, kwamba ndiye mwenye uwezo na wajibu wa kumiliki tatizo hilo. Kasumba hiyo haiwezi kumaliza janga hilo. hatuna budi sote tuliokusanyika kwenye kona tuone kama kila mmoja wetu anawajibika kuiondoa hatari hii. Kukaa pembeni na kubaki kuoneshea kidole na kukandia wengine tu ati fulani ndiye mwenye jukumu la kutunza kundi hilo si sahihi. Hivi ndivyo tusemavyo eti, "Serikali ndiyo yenye jukumu hilo". Lakini serikali ni pamoja na sisi sote. Waswahili husema, "Mchelea mwana kulia, mwishoni hulia yeye".

Tuchukue hatua stahiki sasa kuokoa kizazi hiki.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
9,750
2,000
Shida zilikuwepo tangu enzi za Yesu na mtume Mohammad (SAW), zipo mpaka leo na zitaendelea kuwepo hata kesho.

Kama upo katika position nzuri, msaidie binadamu mwenzio kwa moyo mmoja.

Changamoto ya kusaidia watu pia ni hii moja. Haiwezi kujua ni nani mwenye shida ya kweli na nani ni msanii tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom