Habari wana JF
Kumekuwa na uwepo wa matukio ya kikatili na Unyanyasaji yanayofanywa na watoto /mabinti wanaoitwa wafanyakazi wa ndani
Nimekaa nikawaza sana, binafsi sikuoni kosa la hawa mabinti ila Serikali ndio inafanya siasa inayoharibu kizazi hiki na Kijacho. Kwa kifupi hawa watoto ni watu waliopigwa na Maisha.
Kuna vitu viwili Serikali ingefanya kuweza Kusaidia hawa Watoto na Jamii kwa Ujumla :-

- Hii ajira ya wafanyakazi wa Ndani ilasimishwe. Hapa pawekwe kima cha Chini cha Kueleweka mfano 250K. Umri uzingatiwe na Watu wasaini mikataba na asiruhusiwe kukaa mtu na mtu wa kazi bila Mkataba hii itafanya hii ajira isiwe ya watu waliopigwa Maisha na itaboresha ufanisi katika Ajira hii. Ni ukweli kwamba hawa watoto wananyanyaswa pia na Hawalipwi. Hii Ajira haijakaa sawa kabisa, hivi Mtu anae ingiza kipato cha chini ya 500K anawezaje mmiliki mfanyakazi wa Ndani? Atamlipa nini? Zaidi ya kumzungusha tu
- Hawa Mabinti/watoto Wanahitaji kusaidiwa kimaisha na kimatibabu. Kwa nature ya hii ajira ilivyo hakuna mzazi yeyote anaeweza mtoa mtoto wake akamfanyie kazi za ndani mzazi mwingine. Hivyo ni ajira ya Watoto waliotelekezwa, waliopigwa na maisha, waliotoroka kuja mjini etc .. Kwa kifupi ni watoto walio kwenye maisha Magumu na wengi wao tayari athari ya Afya ya akiri hasa PTSD -post traumatic stress disorders. Hivyo ni group la watoto Serikali inabidi liangaliwe kwa jicho tofauti sio ajira za Ndani.