rushanju
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 3,131
- 4,620
Mimi ni mfanyakazi wa Serikali na ni mtumishi wa muda mrefu nimebakiza miaka mitatu kustaafu. Mkewe wangu nae ni mfanyakazi wa Serikali ila yeye alibaki Dar. Tumetenganishwa kwa nguvu na hili la Dodoma. Tumebahatika kupata watoto.
Baadhi ya watoto wetu wako kwenye ndoa na wengine wako vyuoni nasi. Mke wangu bado ana miaka 13 kazini kabla ya kustaafu. Majuzi amenitembelea hapa Dodoma, alifika akiwa anajisikia vibaya na tukafanya utaratibu wa kwenda hospital. Tulikutana na Dr mstaarabu na akatushauri tupime Ukimwi kwa pamoja.
Majibu yalitoka na mke wangu akiwa Chanya + tulipima tena hospital nyingine na bado ilibaki vilevile. Sasa nabaki najiuliza, jamii itatuelewaje? Watoto watatuelewaje? Wakwe watatuelewaje? Nimekata tamaa na nimebaki bila majibu.
Jamani wenzangu mkae mkijua kuwa hili limetokea kwangu, ukweli wenyewe wengi mko kwenye maisha hayo. Serikali imefanya makosa makubwa sana kutenganisha ndoa za watu kwa makusudi. Watoto wengi walioko mitaani hawana maadili kwa kukosa malezi ya baba na mama.
Hapa tunajenga taifa au tunabomoa. Nimebaki njia panda. Nimfukuze? Nimuue? Au nifanyeje. Huu ni utumishi Serikalini au ni utumwa serikalini. Nimeshindwa kula hata kazini sijaenda. Mke wangu karudi Dar nae sijui anaenda kujiua!
Mbali na lawama kwa mke wangu bado zigo la lawama nawatupia Serikali kwa kukatisha ndoa yangu na pengine itakatisha maisha ya mke wangu aliyeondoka kwa kuchanganyikiwa. Hili la Dodoma linaonekana kama masihara lakini ni janga kubwa sana. Tumejichimbia kaburi kimzaha.