Kwa hili la Wafanyakazi wa Ndani, Serikali inakosea sana

Career ya uhudumu wa nyumbani kwa afrika siyo kazi,na haitoweza kuchukuliwa kama kazi! Tunawachukulia kama wasaidizi,wanakuwa sehwm ya familia zetu ndo maana tunaishi nao pale tunapoishi,tunakula nao kile tunachokula etc,malipo tunachowapa siyo mshahara ni kama ahsante na posho kwa kutusaidia,kwa maisha yetu kinatosha sana sababu hana majukumu mengine ya kutumia kiasi hicho zaidi ya kutuma nyumban kununulia vitu binafsi visivyo vya ulazima!!kama mnataka iwe kqzi serious basi tukubaliane pia alipe kodi,ajigharamie huduma zake za msingi ikiwemo chakula etc mwisho wa siku hqta ukimlipa 300,000 haitomtosha!
Kuna housegirls wengine na ma houseboy maboss wao wanawathamini sana
Maana wameshaona umuhimu wao kwao

Ova
 
Waafrika ni wabinafsi na wanapenda kuambiwa uwongo ndio wanafurahi. Kuna wafanyakazi ambao Kwa Mwezi wanakosa akiba 50,000/- baada ya matumizi yote ,lakini house girl anaipata akiwa tayari ameoga, amekula Kwa Mwezi mzima,amefua, amepata ,Matibabu ,amelala nyumba ambayo halipi Kodi, amekunywa maji ,umeme anatumia , anaanglia TV na taka taka za nyumba zimelipiwa na zimezolewa na sungusungu wameshalipwa Kwa ajiili ya ulinzi.
Inategemea na status yako uliyokuwa nayo...
Mtu anakupikia,anakufanyia ulinzi
Anakuendesha lazima umuheshim
Sana na kumthamini

Ova
 
Mwisho wa siku ukipanga Mahesabu mshahara unaomlipa h/girl unakuwa mkubwa kuliko hata unaolipwa wewe mwenye nyumba
Huyo house girl,house boy,mlinzi wa nyumbani lazima umthamini
Ni sawa na kusema maisha yako,
Yako mikunoni mwao

Ova
 
Imebidi ni~log in ili kuweka mawazo yangu kwenye uzi huu: bongo kuna kawaida ya kutatua changamoto bila kufikiria kwa kina(ref: uamuzi wa watawala kupandisha bei ya mafuta ya taa ili ikaribiane na ya diesel ili kuzuia uchakachuaji!).
Si sawa mdada wa kazi kufanya kazi hadi usiku wa manane, lakini sikubaliani na wenye mtazamo kuwa elfu 30, 40 ni ndogo!
Mimi huwa naichukulia kuwa ni hela anayoweza kuweka akiba baada ya matumizi yote ya lazima....
Malazi, chakula, mavazi, matibabu, hadi kwa wengine nauli ya kwenda kwa wazazi wake na kurudi ni juu ya mwajiri. Nakumbuka home madada wa ndani walikuwa ndio watumiaji wakubwa wa tv kuliko wanafamilia. Familia nyingi mno zina wasaidizi wa ndani wanaoishi nao kawaida mno. Tatizo kubwa ni kuwa kwa wengi wanakuwa kwenye ule umri wa mabadiliko ambao hata watoto wa familia tu ni pasua kichwa!
Hivi hili wazi la wasaidizi wa ndani kulipwa tuseme laki mbili ni ili akapange na kujitegemea wakati wengi wao kiumri wanatakiwa kuwa chini ya malezi au ni vipi?!

Yan hawa watu wanajitoa ufahamu mambo yote unamsimamia wala pesa yake haikuhusu lbd anunue pedi mana had mafuta ya kupaka ni kwako
 
Wabongo tunawasema wahindi wanalipa hela ndogo ila sisi wabongo tungekuwa na uchumi wa kueleweka tungelipa hela ndogo kushinda wahindi.
 
Una hoja ya kimsingi SANA, mf., mshahara wa 40'000 kwa mwezi kiukweli haotoshi kabisa- Huu ni utumwa uliokithiri. Kufanya kazi isiyo na maslahi bora wala ukomo wa muda wa kazi kwa siku yahitaji moyo wa ki-MUNGU. Hawa wadada wataendelea sana kuwa makatili endapo waajiri wao wasipo watengenezea maslahi bora na kujaliwa kwa dhati- Hakuna shortcut kwenye hili
Na huo wenyewe kuna baadhi ya watumishi wa umma wanashindwa pia kulipa kwa wasaidizi wao majumbani kiukweli mkuu kazungumza hoja ya maana sana Mama Gwajima tafadhali popote ulipo toa neno
 
Watesaji wa kubwa ni Wanawake wenzao.Kwa Sasa hata ndugu hawataki kukaa na watoto wa ndugu yao.
Dunia shetani anatawala Sasa ,Kwa hiyo hata mshahara ungekua mil. Moja Bado ukatili ungekuwepo. Utu umepotea kabisa. Miaka 50 ijayo patakua na migahawa ya supu ya nyama za watu.
Duuu hatari
 
Back
Top Bottom